Siitazami ajali ya ndege kama wengi mnavyoitazama, yawezekana kuna makubwa nyuma yake

Huu ni uzembe na kuchezea uhai wa watu

Hivi watu wa CONTROL na Airport kwa ujumla walishindwa nini kuandaa emergence rescue team wakati ndege ipo hewani mara baada ya kutokea hitilafu?

Unawezaje kumuelekeza Rubani kwenda ziwani halafu ndegee inakaa 2 hrs kwenye maji bila kuokolewa.

Ni wakati wa jeshi na serikali kujiimarisha kwenye upande wa dharura, ajali haiwezi kutokea mjini kabisa alafu hakuna team yoyote iliyofika kuokoa, tuache kusubiri maafa ilo tutoe pole tunaweza kuzuia na kupunguza athari
 
Hivi hizo ndege za kampuni ya Prescion Air hazina kisanduku cheusi. Black box? Inaonyesha Kila mtu anatoa maoni yake chanzo Cha ajali. Tuziachie mamlaka zitupe taarifa rasmi badala ya kutulisha matango pori.
Unamjua mtu anaitwa Majaliwa Kassim Majaliwa?
Kashakurupuka uko kaongea bila utaalamu kisha utarajie majibu ya black box upewe yaliyo sahihi. Kwanza hayatopatikana mapema sidhani kama tunaweza soma hiyo black box mpaka iende nje ya nchi. Pili hii ajari inaigusa ofisi yake lazima apindishe mambo kujiokoa.

Tume ya uchunguzi anaunda yeye na uongo ni jadi yake hata awe msikitini. Sina imani na lolote analogusa
 
Chief ni sawa, silaumu ajali ilivyotokea.

Tatizo ni namna ya utoaji taarifa.Kuna mizaha mingi sana kwenye mambo ya kuumiza kama hayo Chief.

Tuwe wakweli kuna baadhi ya Viongozi kama hao wasilete michezo michezo na maisha na taarifa.

Angalia jinsi tu Wananchi wa kawaida walivyosimama na baadhi ya Askari waadilifu.

Linapotokea tatizo kubwa kama hilo tuwajibike kwa Hekima.
 

Aiseee inasikitisha sana kama ni kweli ilikuwa itilafu kwenye tyres na watu wa towers kuwaingiza chaka marubani.
 
Mi bado siielewi taarifa zinatofautiana sana juu ya idadiii ya watu waliokuwa ndani ya ndege walianza kwakusema majeruhi 26 waliokufa 19 jumla yake 45 lakin sasa waliokufa 19 majeruhi 24 sa sijui ipi ni ipi hapa🤷‍♂️
Iko hivi:

Waliokufa ni 19

Majeruhi ni 24 abiria, 1 ni Mvuvi na 1 ni mfanyakazi wa Airport Jumla 26

Mvuvi alijeruhiwa kwenye harakati za Uokoaji

Staff wa Airport alipata pressure akaanguka

Ufafanuzi huu umetolewa na RC Chalamila
 
Pia nadhani rubani ana mchango wake katika ajali hii, kwa nini asingeenda kutua Mwanza baada ya kuona hali ya hewa siyo nzuri?
 
Hivi vi sub airport havina control tower mzee baba
Lkn unapoint za msingi kwenye sired yako
 
Noted ✔️
 
Laiti tungekuwa na private investigators bao hawapo bias tungepata mengi sana.

Lakini kikubwa umeweka hoja za msingi sana. Tunawezaje sasa kupata majibu?
 
Maswali yako yote yatapata majibu.
Tusiamini katika conspiracy theories kila wakati.
 
Pia nadhani rubani ana mchango wake katika ajali hii, kwa nini asingeenda kutua Mwanza baada ya kuona hali ya hewa siyo nzuri?
Mkuu, Kuna vitu vingine vinaweza visisemwe, Ila nahisi wakati anataka kutua Mara ya pili, mafuta ya kwenda Mwanza hayakutosha, yawezekana Bukoba ndege ingejaza mafuta hapo, so ikabidi aipeleke ndege ziwani maana mafuta ya kuwarudisha Mwanza hayatoshi, Ila hayo ni mawazo yangu tu, taarifa kamili tutaipata baada ya uchunguzi kufanyika

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Pengine swali la msingi hapa ni je why haipiti miaka mitano lazima ziwa victoria liondoke na watu?kuna Siri gani?...kuna matambiko ya damu tunafanya? Sisi si ndo nchi ambayo albino wanauwawa kutafuta Utajiri?..
Unategemea kwa ukubwa wa ziwa Victoria mpaka kuzungukwa na nchi tatu za afrika mashariki.. probability ya kupata ajali ndani ya ziwa itakuwa ni sawa na probability ya ajali kupatikana kwenye beseni sio?..



Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Laiti tungekuwa na private investigators bao hawapo bias tungepata mengi sana.

Lakini kikubwa umeweka hoja za msingi sana. Tunawezaje sasa kupata majibu?
Nimeona hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…