Siitazami ajali ya ndege kama wengi mnavyoitazama, yawezekana kuna makubwa nyuma yake

Hiyo ni kwako mkuu.

Wapo ambao biashara na pesa kwao zina thamani kuliko hata uhai wa mama zao, sembuse mpinzani wake kibiashara.
 
Kwa jinsi serikali ilivyoshughulikia hili suala hata mimi napata mashaka juu ya hii ajali.
 
Mimi sio mtaalamu ila kwa jinsi nilivyosikia wahanga ni wazi katika mizunguko iliyofanya muda hakuwa na mafuta ya kutosha katika jaribu la mwisho ni wazi ndege ilikuwa haina mafuta ndio ikazima na ilikuwa ina approach runway mimi nadhani kuna kiuzembe fulani lakini wataalamu watakuja na report na kama sio mafuta itakuwa instruments imefail sababu sio rahisi kuikosa runaway kwa kuwa ndege zina GPS ila hili la mafuta nadhani lina ukweli nahisi sababu walisema walizunguka sana Bukoba sasa walijaza kiasi gani na walitembea kiasi gani..
 
Inawezekana upo sahihi mkuu, ila waliopona katika ajali bado sijasikia hata mmoja akimuongelea shujaa majaliwa. Nimemsikiliza mama mmoja BBC anasema alikaa seat za nyuma na aliyefungua mlango ni muhudumu wa ndege...
Sasa mhudumu wa ndege si alikuwa ndani, af isitoshe mlango wa nyuma wa ndege ulikuwa haujaguswa na maji kabisa maana uko karibu na kibawa cha nyuma mwisho ambako eneo hilo still lilikuwa hewani. Its likely dogo alipanda akawa anauvuta mlango kwa nje.
 
Ukiniuliza sababu hata mimi nitakujibu ni likely ndege ilikuwa ina run low on fuel kwa maana waliweka wese la kidebe hali ya hewa ikawa sio rafiki ikawalazimu wazuge zuge hewani ila sasa walikuwa wanatembelea reserve kwa maana taa ya wese ilikuwa inawaka toka wameanza ku roam.

Mwisho ndio rubani anaambiwa akaitue Mwanza akicheki wese halitoboi akawaambia control room wakasema bora akaidondoshee kwenye maji tu haina jinsi. Maana anageishusha kwenye mawe ya Mwanza yale asingetoka mtu ingekuwa balaa zito.
 
Ndege haikuwa na mafuta ile. Sidhani kama kuna ishu ingine zaidi
 
Kuna mambo mawili, tyre ziligoma ama wese la kurudi Mwanza lilikuwa halimfikishi.
Itakuwa ni tairi ziligoma kutoka na siyo hali ya hewa kama tulivyoelezwa. Ingekuwa hali ya hewa, angeweza kwenda hata Chato! Sema business!
 
Unadhani wataiacha, wanaweza kusingizia hata imeliwa na mamba 😂😂😂 kama ile engine ya Scania pale mto Wami.
wahuni wanaweza kuiiba mchezo ukaishia hapo hahahahaha
 
Dogo alipigwa na kamba akazimia 😂😂😂 hii story imekaa kimchongo sana
 
You're genius as I'm 😎

Wazo langu la kwanza lilikuwa ni kuishiwa mafuta.

Nikawaza pia nguvu za giza, wale watoa makafara, niliwawaza sana

Nikawaza hasira ya Mungu kwamba mlitaka muingie ibadani, japo God ni wa rehema muda wote.

Nikawaza wale pia wajitoa mhanga, na vile tunawaleta akina mjomba huku tuiharibu hii precision ili tuje na ndege zetu.

Nikawaza yule dada aliyekuwa anaenda kutambulishwa, mchaga na mhaya its parallel never meet.

Nikasikia idadi ya wahanga na halisi pia havina uhusiano? nani kazidi, ndege siyo treni kwamba kajichomeka.

Pia nikasikia watu waliofariki walivyoumia sana sana nikasema nini kilikuwa ndani ya ndege?


Nikashangaa boss alivyotoa machozi as if was something to avoid why these?

Kijana Majaliwa sasa alivyokuwa analia pale anapewa ili milioni ya mwanzo, as if anasema I was supposed to do more.

Yote ndani ya yote tumpe MUNGU HESHIMA NA UTUKUFU.
 
Hivi ile video mama anaeelezea kutokea ajali mara sehem nyingine anasema sio ajali ni zoezi, ni video ya ajali ya juzi au ni ya zamani kidogo? Maana nitandaoni kuna mengi, hiyo video ilisambaa siku ya ajali bukoba.
 
Aliyenishangaza ni yule wa Juzi aliyesema yeye alijiokoa lakini jina lake ni miongoni mwa wale marehemu walioagwa na kusafirishwa
 
Hii kitu inachanganyà na waliookoka hawatasema.

Mimi nikawaza hilo la mafuta..... jibu nikaona hapana hii ndege wana bei zao kubwa wanaweza kuweka mafuta ya bajeti?

Kwa nini rubani alikuwa akizurula kyaka huko kote kwa nini hakurudi mwanza?

Au ni kweli ndege ilipata shida angani akashindwa jinsi ya ku land?

Au ni kweli kuwa tires za ndege zilishindwa kutoka ndo akaona hata akienda mwanza tatizo ni lile lile bora aipeleke ziwani kuzima ingine kuepuka mlipuko akitua nchi kavu?

Kwa nini yule mtoto azuiliwe kuvunja kioo?

Hali ya hewa ilikuwa mbaya? Nooo angerudi mwanza

Ushirikina? Kwamba yule binti asiolewe? Roho zile zote zife kisa mtu mmoja asiolewe? Huruma iko wapi hapa duniani kwa nini haya mateso yote ewe Munngu? Watu tunachukiana kiasi hiki?

Kama hii ajali ina chembe chembe za ushirikina basi umenikumbusha kitu, siku zilizopita kulitokea ajali kijiji kimoja huko, kwenye hilo gali kulikuwemo dada mmoja, basi shuhuda wa kwanza alipofika akamuona huyo dada maana anajulikana akampigia simu kaka yake wa damu ni tajiri akimwambia alete gari dada yake kaumia sana, nasikia alifurahiya habari hiyo akamjibu wengine wote wapone huyo afe na kweli gari lote walipona kasoro dada yake.

Ewe Mungu nusuru bukoba majanga makubwa yanatokea bukoba, mara tetemeko, mv bukoba, sasa ndege jaman.
 
Majibu yatapatikana kutoka chumba cha kuongozea ndege, kupitia mawasiliano ndani ya lisaa 1 kabla ya ajali kutokea. Yale majadiliano, yataonyesha hali halisi ya kilichotokea.
Majadiliano una uakika kwa sasa yapo? Yashapotezwa kaa kwa kutulia.
 
Na tumjadili pia yule aliyeambiwa kuwa sasa umekua kafanye kazi.

Si tulimuona akiabudu kuleee pia yule yuko huko huko kanda ya ziwa,

Je, ndo amekua kwa damu zote hizo?

Mbona pia katazo la kubomoa mlango alilitoa yeye? nini alikuwa anawaza?
 
Ama chato kiwanja hakifanyi kazi maana pale ni chap tu angeenda ama nae alikua analazimisha kushuka pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…