DOKEZO Sijalipwa malipo yangu ya Vita ya Kagera, kila nikifuatilia naambiwa hakuna anayedai

DOKEZO Sijalipwa malipo yangu ya Vita ya Kagera, kila nikifuatilia naambiwa hakuna anayedai

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nikirejea tamko la Waziri wa Ulinzi katika Bunge la Tanzania tarehe 13 -06-2024, siku ya Alhamisi. Bunge la 12 kikao cha 15. Taarifa ya Waziri ya Ulinzi katika taarifa yake moja ni wanajeshi wote waliopigana katika vita vya Kagera wote wameishalipwa.

CPL NGUSSA GULINJA 692 DET ni mmoja wa wastaafu wa jeshi waliopigana katika vita ya Kagera mwaka 1978-1979. Anadai Baada ya vita kuisha aliondoka Uganda kurudi Tanzania mnamo 06-03-1980. (Barua imeambatanishwa).

Anauliza kwa mamlaka husika, je mafao yake ya vita ya Kagera kwa mujibu wa Waziri yamepotelea wapi?

Anaomba msaada ili apate haki zake za kimsingi (barua na medali ya vita iimeambatanishwa)

NB. COMPUTER No 4253480 Hii ni namba ya malipo.

Barua ya Vita ya KAGERA 1978-1979.jpg
 
Attachments

Nchi ya ajabu kweli. unamrusha hata hao waliojitolea mhanga kufa kuitetea nchi? bila aibu wanasiasa mnalipana miposho na mishahara minono watoto wenu wanasoma nje.mnawasahau hata hao waliotete nchi? GENERAL MABEYO ULIFANYA MAKOSA MAKUBWA KUTOKUICHUKUA NCHI,hivyi vyama vya UKOMONIST HAVINA HURUMA NI MASHETANI HAWAAMINI KATIKA SANDUKU LA KURA WANAAMINI KTK UBABE UPORAJI NA UDIKTETA.katika maeneo mbalimbali duniani hasa west afrika wameondolewa kwa MAPINDUZI.Angalia vijana wako wanalia maisha magumu stahiki zao hawajalipwa.HI LAANA UTABEBA
 
Tatizo ktk utumishi wa umma utakuwa tu na thamani kabla ya kufa au kustaafu. Ukifa au kustaafu wewe ni takataka, ndo maan watumishi wengi ni corrupt sababu wanajua mbali na mishahara yao midogo, huko mbeleni wasipoweka mazingira mazuri watajuta km ilivyokutokea wewe. Wanaoiba hukaa kimya hata wakidhulimiwa mafao.

Pole sana hii ndo Tz, na fikiria ulirudi salama vipi km ungefia huko unadhani familia wangepata hata mia mbovu?
 
mheshimiwa Mwigulu Nchimba, nisaidieni kumwita, alipe mtu wa watu ale chake angali hai
Swali linakuja kwa wadaiwa hao walioko madarakani vita ya Kagera walikuwa na umri gani? Hawawezi kumsaidia mtu ambaye hawajui thamani yake, inaumiza Sana shemeji yangu alikuw mifugo, katembea ofisi karibu zote.hama.alichoambulia hadi umauti umemkuta kaacha faili ndani
 
Yaaan nchi ya kipumbafu sana hii ...bibi yangu had anakufa hakuwahi kupata mafao yake... Licha ya kupewa kila document na kuambiwa asubl mafao alikaa karibu miaka 3 hakuna hela ...... Manyoko!! Zao...
 
Kuna mambo yanashangaza sana nchi hii.
Binamu yangu alishiriki kikamilifu Vita vya Kagera mwanzo mwisho, tena alikuwa kikosi cha mizinga.
Huyu bwana alitumikishwa tena baada ya vita huko msumbiji kwa mkataba mfupi, baada ya hapo akatimuliwa jeshini ....
Hadi leo yupo yupo tu cha pombe, hana usaidizi wowote kutoka Serikali iliyomtumia ujana wake zaidi ya misaada ya wanandugu.

Haijulikani alifanya kosa gani huko jeshini hadi kustahiri kufukarishwa kiasi hicho? 😲
 
Naskia huruma nikiona mstaafu anadai haki yake na hakuna wa kumsikiliza.Viongozi msiposikiliza wenye shida katika haya maisha maisha yajayo hakuna atakayewasikiliza zaidi ya shetani mtakae ishi nae milele
 
Nikirejea tamko la Waziri wa Ulinzi katika Bunge la Tanzania tarehe 13 -06-2024, siku ya Alhamisi. Bunge la 12 kikao cha 15. Taarifa ya Waziri ya Ulinzi katika taarifa yake moja ni wanajeshi wote waliopigana katika vita vya Kagera wote wameishalipwa.

CPL NGUSSA GULINJA 692 DET ni mmoja wa wastaafu wa jeshi waliopigana katika vita ya Kagera mwaka 1978-1979. Anadai Baada ya vita kuisha aliondoka Uganda kurudi Tanzania mnamo 06-03-1980. (Barua imeambatanishwa).

Anauliza kwa mamlaka husika, je mafao yake ya vita ya Kagera kwa mujibu wa Waziri yamepotelea wapi?

Anaomba msaada ili apate haki zake za kimsingi (barua na medali ya vita iimeambatanishwa)

NB. COMPUTER No 4253480 Hii ni namba ya malipo.

View attachment 3180297
Huyo mheshimiwa Tax nami nilimsikia akitoa maelezo hayo Bungeni, yakanigusa na kunishangaza sana!

Mpaka nikaanza kufikiri kuwa, ndani ya Serikali kuna watu maalumu kwa ajili ya kupotosha ukweli na kukandamiza haki za watu, sijui huwa ni kwa maslahi ya nani!

Madai hayo ya huyo askari mstaafu yana ukweli usiotia shaka.

Ukweli ni kwamba, baada ya vita vya Kagera kumalizika mwezi July 1979, Serikali ya Nyerere iliingia mkataba wa kiulinzi na mafunzo ya kijeshi kwa Serikali ya Uganda ya Binaisa kwa miaka miwili, mkataba uliokuja kumalizika mwezi June mwaka 1981.

Ilipofika mwaka 1980, mwezi March, jeshi liliamua kuanza kuwarejesha kidogo kidogo nyumbani baadhi ya askari wake kwa uchache.

Na mwaka 1981 mwezi March shughuli za kuwarejesha nyumbani askari wote 40,000 waliokuwa nchini Uganda kwa mkataba niliouelezea zilianza.

Pale Mwanza Kizumbi palijengwa Centre kubwa kwa ajili ya mapokezi na malipo.

Askari tuliokuwa maeneo ya mbali nchini Uganda, mfano mimi nilikuwa Kasese(Rwenzori mtn) kwa wakati huo, sote tulisogezwa mjini Jinja kwa ajili ya maandalizi ya kurejeshwa nchini.

Ilipofika mwezi May, sikumbuki tarehe, kazi rasmi ya kuwasafirisha askari kwa kutumia meli ya Mv Viktoria ikaanza.

Mimi main first yangu ilisomwa na kusafiri na kufika Mwanza mwezi June 1981 na kukuta mapokezi makubwa Mjini Mwanza na utaratibu wa malipo ukawa umeandaliwa kwa mchanganuo ufuatao:
Wale waliokuwa mobilized (Polisi, Magereza na Mgambo) walipigiwa mahesabu ya mishahara kwa vyeo vyao kwa muda waliokaa Uganda, wakalipwa na kurejeshwa makwao ama kwenye vituo vyao vya kazi vya awali.

Kwa sisi wanajeshi waajiriwa wa Jwtz hatukulipwa chochote pale Mwanza, bali tuliandaliwa tu usafiri na kurejeshwa kwenye vikosi vyetu vya awali tulivyoondokea kwenda vitani kwa maelezo kwamba stahiki zetu tutalipwa vikosini mwetu.

Tulipofika vikosini, tuliandaliwa Aquitance rolls za malipo ya malimbikizo ya mishahara yetu kwa idadi ya miezi tuliyokuwa vitani, kama vile mobilized walivyofanyiwa kule Mwanza.

Baada ya hapo hakuna malipo yoyote ya vita kwa askari wa muda ama askari wa kudumu yaliyotolewa mpaka leo.

Miaka ya karibuni kwenye utawala wa Kikwete ndiyo tukasikia Mheshimiwa Rais Museveni wa Uganda alitoa ruzuku ya fedha ama shukurani kwa askari wote walioshiriki vita vya Kagera vya kumng'oa Amin, lakini mpaka leo habari hizo zimebakia kuwa ni tetesi tu.

Kwa hiyo majibu ya mheshimiwa Waziri kuwa askari wote wa vita walikwisha kulipwa yalitushangaza sana, kwani malimbikizo ya mishahara yetu ya nyuma hayakuwa ni malipo ya vita.

Na wengi wetu tulioshiriki vita hivyo takribani miaka 50 sasa, tayari walikwishapoteza maisha kutokana na jambo lenyewe hilo kuwa ni la miaka mingi sana.

Pia utaratibu alioutangaza kwa wale wote walioshiriki vita hivyo, lakini wakakosa sifa za penshini, wote wataunganishwa kwenye pensheni, sijaona hatua yoyote kuchukuliwa nadhani ni kubuy time ili nature itende jambo hilo liishe kimya kimya.
 
Nchi ya ajabu kweli. unamrusha hata hao waliojitolea mhanga kufa kuitetea nchi? bila aibu wanasiasa mnalipana miposho na mishahara minono watoto wenu wanasoma nje.mnawasahau hata hao waliotete nchi? GENERAL MABEYO ULIFANYA MAKOSA MAKUBWA KUTOKUICHUKUA NCHI,hivyi vyama vya UKOMONIST HAVINA HURUMA NI MASHETANI HAWAAMINI KATIKA SANDUKU LA KURA WANAAMINI KTK UBABE UPORAJI NA UDIKTETA.katika maeneo mbalimbali duniani hasa west afrika wameondolewa kwa MAPINDUZI.Angalia vijana wako wanalia maisha magumu stahiki zao hawajalipwa.HI LAANA UTABEBA
Una uhakika gani General Mabeyo na utawala wa kijeshi wangefanya vizuri kuliko utawala wa sasa?

Acheni ku fetishize utawala wa kijeshi nyie.
 
Pole sana mkuu.. kipindi waziri anatoa tamko nilisema humu kuna mashujaa wetu wengi bado hawajalipwa.. pesa zimepigwa juu kwa juu
 
Back
Top Bottom