Huyo mheshimiwa Tax nami nilimsikia akitoa maelezo hayo Bungeni, yakanigusa na kunishangaza sana!
Mpaka nikaanza kufikiri kuwa, ndani ya Serikali kuna watu maalumu kwa ajili ya kupotosha ukweli na kukandamiza haki za watu, sijui huwa ni kwa maslahi ya nani!
Madai hayo ya huyo askari mstaafu yana ukweli usiotia shaka.
Ukweli ni kwamba, baada ya vita vya Kagera kumalizika mwezi July 1979, Serikali ya Nyerere iliingia mkataba wa kiulinzi na mafunzo kwa Serikali ya Uganda ya Binaisa kwa miaka miwili, uliokuja kumalizika mwezi June mwaka 1981.
Ilipofika mwaka 1980, mwezi March, jeshi liliamua kuanza kuwarejesha kidigo kidogo nyumbani baadhi ya askari wake kwa uchache.
Na mwaka 1981 mwezi March shughuli za kuwarejesha nyumbani askari wote 40,000 waliokuwa nchini Uganda kwa mkataba niliouelezea zilianza.
Pale Mwanza Kizumbi palijengwa Centre kubwa kwa ajili ya mapokezi na malipo.
Askari tuliokuwa maeneo ya mbali nchini Uganda, mfano mimi nilikuwa Kasese(Rwenzori mtn) kwa wakati huo, sote tulisogezwa mjini Jinja kwa ajili ya maandalizi ya kurejeshwa nchini.
Ilipofika mwezi May, sikumbuki tarehe, kazi rasmi ya kuwasafirisha askari kwa kutumia meli ya Mv Viktoria ikaanza.
Mimi main first yangu ilisomwa na kusafiri na kufika Mwanza mwezi June 1981 na kukuta mapokezi makubwa Mjini Mwanza na kukuta utaratibu wa malipo ulishaandaliwa kwa mchanganuo ufuatao:
Wale waliokuwa mobilized (Polisi, Magereza na Mgambo) walipigiwa mahesabu ya mishahara kwa vyeo vyao kwa muda waliokaa Uganda, wakalipwa na kurejeshwa makwao ama kwenye vituo vyao vya kazi vya awali.
Kwa sisi wanajeshi waajiriwa wa Jwtz hatukulipwa chochote pale Mwanza, bali tuliandaliwa tu usafiri na kurejeshwa kwenye vikosi vyetu vya awali tulivyoondokea kwenda vitani kwa maelezo kwamba stahiki zetu tutalipwa vikosini mwetu.
Tulipofika vikosini, tuliandaliwa Aquitance rolls za malipo ya malimbikizo ya mishahara yetu kwa idadi ya miezi tuliyokuwa vitani, kama vile mobilized walivyofanyiwa kule Mwanza.
Baada ya hapo hakuna malipo yoyote ya vita kwa askari wa muda ama askari wa kudumu yaliyotolewa mpaka leo.
Sana babu
Miaka ya karibuni kwenye utawala wa Kikwete ndiyo tukasikia Mheshimiwa Rais Museveni wa Uganda alitoa ruzuku ya fedha ama shukurani kwa askari wote walioshiriki vita vya Kagera vya kumng'oa Amin, lakini mpaka leo habari hizo zimebakia kuwa ni tetesi tu.
Kwa hiyo majibu ya mheshimiwa Waziri kuwa askari wote wa vita walikwisha kulipwa yalitushangaza sana, kwani malimbikizo ya mishahara yetu ya nyuma hayakuwa ni malipo ya vita.
Na wengi wetu tulioshiriki vita hivyo takribani miaka 50 sasa, tayari walikwishapoteza maisha kutokana na jambo lenyewe hilo kuwa ni la miaka mingi sana.
Pia utaratibu alioutangaza kwa wale wote walioshiriki vita hivyo, lakini wakakosa sifa za penshini, wote wataunganishwa kwenye pensheni, sijaona hatua yoyote kuchukuliwa nadhani ni kubuy time ili nature itende jambo hilo liishe kimya kimya.