DOKEZO Sijalipwa malipo yangu ya Vita ya Kagera, kila nikifuatilia naambiwa hakuna anayedai

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Aisee pole sana babu nimejikuta nabubujikwa na machozi . Nchi yangu Tanzania
 
Mkuu,

Kwanza kabisa shukurani kwa kazi kubwa ya kuilinda Tanzania.

Kuhusu malipo, kwani kabla ya vota makubaliano yalikuwaje? Kulikuwa na makubaliano ya malipo maalum yaliyozidi malipo ya kawaida mnayosema mmelipwa?
 
CCM ni janga.ambao hawakupata haki zao ni wale wadogo wadogo tu lakini wale wakubwa wote wakipewa.Ajabu sana Huyu Samia.Na Kwa Sasa amependekeza wake wa Marais,mawaziri,wakurugenzi wa mashirika walipe 80% ya mshahara na marupurupu ya rais lakini sisi wazee tuliopigana vita kujikomboa Nchi yetu tuna telekezwa.
 
Una uhakika gani General Mabeyo na utawala wa kijeshi wangefanya vizuri kuliko utawala wa sasa?

Acheni ku fetishize utawala wa kijeshi nyie.
Haijalishi kinachotakiwa hawa mashetani macomonist watoke tuanze upya kureform nchia
 
Mkuu,

Kwanza kabisa shukurani kwa kazi kubwa ya kuilinda Tanzania.

Kuhusu malipo, kwani kabla ya vota makubaliano yalikuwaje? Kulikuwa na makubaliano ya malipo maalum yaliyozidi malipo ya kawaida mnayosema mmelipwa?
Afu kuwa na adabu....ujue unazungumza na mtu alie enda front,yaani aliechezea kifa
 
Afu kuwa na adabu....ujue unazungumza na mtu alie enda front,yaani aliechezea kifa
Sasa nimeanza kwa kumshukuru kwa kazi kubwa aliyofanya kuilinda Tanzania, adabu nimeiweka mbele kabisa hapo, unaanzaje kuniambia niwe na adabu?
 
Mkuu,

Kwanza kabisa shukurani kwa kazi kubwa ya kuilinda Tanzania.

Kuhusu malipo, kwani kabla ya vota makubaliano yalikuwaje? Kulikuwa na makubaliano ya malipo maalum yaliyozidi malipo ya kawaida mnayosema mmelipwa?
Ahsante.

Ipo hivi mkuu, kanuni zote za malipo, zimefafanuliwa katika vitabu vya sheria za majeshi ya ulinzi juzuu ya 3.

Kuna mshahara na posho mbalimbali anazostahili askari kulipwa awapo kikosini na maeneo ya operesheni mbali mbali.

Kwa mfano: ukiwa kikosini, utapata mshahara na posho za chakula pamoja na posho zingine zilizokasmiwa.

Ukitoka nje ya kikosi chako, ukapelekwa mipakani huko, wao wanaita 'detouch' automatic unastahili kulipwa allowance ya operesheni pamoja na ration allowance.

Kwa hiyo hela hiyo ya operesheni pamoja na ration allowence hatukulipwa kwa muda wote tuliokaa huko, mi'nilikaa miaka 2.6.

Ila tulipokwenda Msumbiji mwaka 1986, kwa kuwa hapakuwa na udharula kama ilivyokuwa kwa vita vya Kagera , kabla ya kuondoka, malipo na stahiki zingine yalifafanuliwa kuwa kila mwezi tutalipwa dollar ngapi inclusive ration allowance kwa kila mwezi kama ilivyo stahili.

Pesa hiyo kila mwezi tulilipwa, ndiyo maana hausikii mtu aliyeenda Msumbiji analalamikia kudhulumiwa haki zake.

Mkuu inapozuka vita, huwa hakuna mjadala wa malipo, huwa ni kusukumwa tu vitani, isipokuwa haki zote za malipo zipo wazi kwenye vitabu vya sheria za malipo.
 
Wengine babu na mama zetu walikuwa front huko
Alafu sahv anasimama lijamaa tumbo kubwa anakuambia mm mzalendo wa kweli 😄
Mzalendo wa kweli umefanya nini au kwa kulopokalopoka

Ova
 
Salute kamanda

Ova
 
Tatizo waziri anapewa tu taarifa,ukute hela zilishatolewa,zilishaliwa na wakubwa.
 
Sasa nimeanza kwa kumshukuru kwa kazi kubwa aliyofanya kuilinda Tanzania, adabu nimeiweka mbele kabisa hapo, unaanzaje kuniambia niwe na adabu?
Huyo ni babu yako anza na salamu ya heshima....anyway ni utani tu mkuu,ila jf kuna mababu zetu humu aisee
 
Huyo ni babu yako anza na salamu ya heshima....anyway ni utani tu mkuu,ila jf kuna mababu zetu humu aisee
Mimi sina utani na wewe lakini. Usijipe haki ya kufanya utani na watu usio na utani nao kihivyo.
 
Mimi sina utani na wewe lakini. Usijipe haki ya kufanya utani na watu usio na utani nao kihivyo.
Sasa mkuu....una haki gani ya kumuita huyo mzee mkuu au hujui neno mkuu linamaana gani.?

Mpe heshima yake bhna....mpigie ata saluti ndo umuulize hayo maswali ya kinafiki
 
Sasa mkuu....una haki gani ya kumuita huyo mzee mkuu au hujui neno mkuu linamaana gani.?

Mpe heshima yake bhna....mpigie ata saluti ndo umuulize hayo maswali ya kinafiki
Hapa napo bado unaendeleza utani au uko serious?

Sikuelewi.
 
Pole Sana mkuu naomba serikali ya SSH ifikirie hili jambo maana hapo chini pameniumiza Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…