Sijawahi kuambiwa maneno yakaniuma kama aliyoniambia aliyekuwa mpenzi wangu, sitayasahau kamwe



Mwanamke ameongelewa sehemu nyingi sana, sio hapo tu, nafikiri hakuna mahali biblia imesema kijana wa Standard 7 aoe asioe mwanamke mwenye PhD, will you do that sababu haijaandikwa? Biblia ni kamili, ila usichukue package moja tu.
 
Duh ni hatari
 
Nahisi nimeachwa ila naombea niwe sijaachwa[emoji16].

Siwalaumu kwa kutaka sura t rangi sababu washajikatia tamaa kupata huyo wa mithali mkuu so acha wafaidi uumbaji
Pole mkuu,
Itabidi nawe utafute mume wa kwenye Bible, sijui anatoka kitabu gani manake sio Suleiman wala Daudi walikula K moja tu. Labda Job manake sikusikia kashfa yake.
 
Hapana.
Hajaniita mchawi wa kiswahili ila ni kama ameniita mchawi wa kizungu,a witch.Mzungu akisema my wife is a witch hamaanishi anapaa na ungo wala kuvaa tungure.
Ukieleza kilichotokea utanistua maana nafsi imegawanyika Kuna upande unataka useme na mwingine hautaki na unaishia kuzunguka tu bila kuweka jambo bayana
 
Pole mkuu,
Itabidi nawe utafute mume wa kwenye Bible, sijui anatoka kitabu gani manake sio Suleiman wala Daudi walikula K moja tu. Labda Job manake sikusikia kashfa yake.
Maombi yangu sio kupata mwingine maana hata yeye ni bora kwangu.
Hayo ya K atajua na Mungu wake sijawahi kujua kama ana K nyingine zaidi yangu
 

Mwanamke wa Mithali 31 siyo mwanamke mmoja. Hilo linaeleweka kwa wanazuoni wengi wa Theolojia maana katika uhalisia wake hakuna mwanamke ambaye anaweza kuwa na sifa zote zile labda awe roboti la Elon Musk.

Walimu wengi wanaofundisha mambo ya ndoa huitumia Mithali 31 kama picha tu ya sifa za jumla ambazo mke mwema anapaswa kuwa nazo. Kila muoaji ana vigezo vyake au sifa anazozitafuta na akizipata kwa kiwango cha asilimia angalau 60+ basi inatosha.

Tukumbuke tu kuwa hakuna aliye mkamilifu. Hata Mama E wangu siyo mkamilifu na ana mapungufu mengi sana lakini kwa vile ana sifa chache za msingi nilizokuwa nazitafuta kwa mwanamke basi inatosha. Mengine tunavumiliana, kurekebishana na kuchukuliana kama wanadamu; maana hata mimi siyo mkamilifu kwake.

Na pole kwa maneno ya kuumiza uliyoambiwa na huyo boya aliyekuumiza lakini usijipe steresi kwa kujaribu kuwa kama mwanamke wa Mithali 31. Hutaweza!

 
walokole na umalaya hamjambo.sikia dada bwanawako amepata taarifa kuwa kanisani Kuna kiongozi ana kufukuzia Sasa sijui ni mpiga kinanda au muhasibu au baba mchungaji mwenyewe?wewe ndio utakuwa na jibu sahihi.

hata Mimi mkewangu siwezi kukubali ajifanye mtu wadini sana kumbe nichakula Cha viongozi kwenye ibada zao

hatakama hujaliwa ila kutompa taarifa kuwa ibadani Kunamtu anakutongoza hilo nikosa mana mtongozaji akiongeza siraha za mashambulizi utaliwa na itakuwa ndio tabiayako.

mwamba Yuko sahihi kukuacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…