Sijawahi kuambiwa maneno yakaniuma kama aliyoniambia aliyekuwa mpenzi wangu, sitayasahau kamwe

Sijawahi kuambiwa maneno yakaniuma kama aliyoniambia aliyekuwa mpenzi wangu, sitayasahau kamwe

Mithali what??? Hahahaaah!
Tuache kudanganyana hapa. Just imagine; (kutoka katika komenti zake)
~age: 36
~watoto: hana
~bikra: hana
~maex: wawili (wanaojulikana mpaka kwa ndugu akiwemo mchungaji)
~hitmen (madanga): unknown
~kutongozwa: yes as a lady
~nk
Kiufupi, our mithali lady yupo desperate sana kutokana na maisha aliyoyapitia na umri alionao

Yawezekana kweli anajiona ni mithali lady lakini uhalisia unamkataa... Church man aliyenaye sasa kagundua kuwa kava la kitabu halisadifu yaliyomo ndio maana kaamua kumove on muda ambao mithali lady alitaka kutulia na kujenga maisha baada ya mahangaiko mengi ya duniani.
Jamaa kagundua ripoti ya CAG ina dosari akaamua kusepa mazima....kwamba kava la kitabu na yaliyomo ndani havina uhusiano hata wa asilimia 15% tu! 😁😁😁

Screenshot_20230717_140602_Instagram Lite.jpg
 
Sasa ndo nini..... kwaiyo alikwambia wewe ni mwanamke wa mithali31
 
kwa akili hizi zake za kuandika. anastahili kuambiwa alicho ambiwa mpaka kikamfikisha huku JF na Nukuu za mithali
Huyo mtu mbona nishamsahau wakuu?Mnaonaje tufunge uzi atajing'ata bure huko saa hizi ashindwe kumkiss mpenzi wake mpya jinsi mnavyomtajataja😁.
He is a closed chapter
 
Sasa ndo nini..... kwaiyo alikwambia wewe ni mwanamke wa mithali31
Uzi usha expire huu mkuu.
Huyo mtu keshakua historia na hayuko tena kwenye maisha yangu na sioni umuhimu wa kuendelea kumjadili hapa.
 
Asepe tu atatokea wakunikubali na madhaifu yangu
Usidinywe tena na watu wa kanisani na hasa Baba Mchungaji. Baadhi yao wanatumia nguvu za giza na ukiingizwa kwenye maagano yao ya kishetani huko hutakaa uwe na amani maishani mwako. I hope utakuwa umejifunza kitu....

Ndiyo utapata mwingine na pengine bora zaidi lakini huyu mwamba ulikuwa unamkubali ndo maana ulikuja mpaka kuanzisha uzi huku. Sizitaki mbichi hizi ama?

Humble yourself. Repent. Be genuine. Focus on yourself and you will attract your Mr. Right!

I am rooting for you sis 🙏🏿
 
Ni kweli niliikua namkubali mwamba na sio sizitak mbichi hizi bali siwez kushinda namuwaza nikilia wkt huko aliko keshanisahau anacheka na kufurahi na mpenz wake mpya.

Nimekua humble kiasi cha kusema hapa kuwa alikua na haki yakunione alivyo niona sasa unataka niwe humble vipi zaidi ya kukiri na kukubali kuwa kweli nilimkosea?

Yeye aende tu nishakubali kuwa Iam single now na namtakia heri huko aendako.
 
Yeye aende tu nishakubali kuwa Iam single now na namtakia heri huko aendako
 
Ni kweli niliikua namkubali mwamba na sio sizitak mbichi hizi bali siwez kushinda namuwaza nikilia wkt huko aliko keshanisahau anacheka na kufurahi na mpenz wake mpya.

Nimekua humble kiasi cha kusema hapa kuwa alikua na haki yakunione alivyo niona sasa unataka niwe humble vipi zaidi ya kukiri na kukubali kuwa kweli nilimkosea?

Yeye aende tu nishakubali kuwa Iam single now na namtakia heri huko aendako.
Mkuu,
Ni kweli ulidinywa na watu wa kanisani kwako?
 
Pole sana dada yangu, kweli ni rahisi mwanaume kumchukulia vibaya mwanamke kutokana uharibifu uliopo Duniani umeharibu kabisa picha ya mwanamke. Mwenyewe nina mchumba wangu ambaye mwanzo nilikuwa na mtazamo hasi juu yake.
Moyo wangu ulikuwa unamkubali ila akili ilikuwa inaniambia hawezi kuwa mke mwema wa Mithali 31 ambaye nimekuwa nikimuomba na kumgoja toka kwa Mungu miaka yote hii.
Mpaka baadae nilipokuja kumfahamu vizuri nikashangaa kumbe ni tofauti kabisa na nilovyokuwa namfikiria.
Hivyo we usivunjike moyo, endelea tu kuwa good girl, atakuelewa tu kama ni mtu sahihi kwako. Asipokuelewa Mungu atakuletea mwingine ambaye ni sahihi kwako na atakuelewa.
 
Hivyo we usivunjike moyo, endelea tu kuwa good girl, atakuelewa tu kama ni mtu sahihi kwako. Asipokuelewa Mungu atakuletea mwingine ambaye ni sahihi kwako na atakuelewa.
Kunielewa hawezi kunielewa ila siwezi kuvunjika moyo na nitaendelea kuboresha mienendo yangu.

Asante kwa maneno mazuri mkuu 🙏
 
Kwa kawaida mida hii huwa nakua kanisani ila kwa jinsi nilivyo depressed hata ningeenda Church nisingetoka na chochote.

Toka juzi nimekuwa naisoma MITHALI 31-10-31 kwa lengo la kujitathimini maana ndoto yangu ni kuwa huyu mwanamke anayeelezewa hapa.

Kila nikiisoma hii Methali najiona nikilandana na huyu mwanamke kwa 97% na tena nasema kwa kujiamini kuwa nimemzidi mwanamke wa Mith. 31-10-31 kwa ubora....(YES).

Mwanamke kuwa mwanamke wa MITH 31 huamki tu siku moja na kujikuta hivyo, wala huzaliwi hivyo na wala sio bahati bali ni kwa kujitengeneza kwa mchakato wa muda mrefu na kwa msaada wa roho wa Mungu.

Hata hivyo Mungu anaweza kukukutanisha na huyu mwanamke ila shetani atahakikisha anakutoa kwake kabla hujajua thamani ya mwanamke uliyenae.

Wanaume wengi mnakutana na hawa wanawake ila kwa vile shetani anapenda kusikia vitu kama KATAA NDOA atahakikisha hata Mungu akikuletea huyu mwanamke HUMUONI. Atahakikisha unaona vile anavyotaka yeye uone na ndio maana Biblia inasema 'MKE MWEMA, JE NI NANI AWEZAE KUMUONA?"

JE NI NANI AWEZAE KUMUONA?
Mwanaume jiulize, UKIMUONA mwanamke ambae kamwe hawezi kukusaliti hata uwe Impotent au atongozwe na Bill Gates au upoteze kazi au uumwe miaka 10 kitandani na hatasema siri hizo kwa yeyote zaidi ya kwa Mungu wake UTAMJUA? Utatumia vigezo gani KUMJUA? Kwanza kuna wanaume na baadhi ya wanawake hawaamini kama hawa watu wana exist ila wapo ila KUWAONA ni mpaka kwa neema.

Wanaume huwa mna vigezo vyenu vya kujua mke mwema ila Mungu akikuletea mwanamke ambae keshajiandaa na kujipa maarifa na uwezo wa kusimama kwa uaminifu bega kwa bega na atakayekuwa mumewe katika kuboresha maisha ya familia yao utatumia vigezo gani KUMUONA?

Je, UTAMUONA kwa zawadi anazokuletea wakati wa uchumba au utamuona kwa sababu haombi nauli au utamuona kwa ajira/biashara yake nzuri au utamuona kwa kuwa hata ukikaa wiki bila kumtafuta halalamiki au utamuona kwa degree yake au utamuona kwa sababu hana kasoro kama binadamu wengine au UTAMUONAJE?

Kwa jinsi ninavyoongoza maisha yangu sikutegemea ipo siku nitaambiwa maneno niliyoambiwa lakini yamenisaidia kujua nifanye nini ili nisije nikaambiwa tena.

NB: Sijaandika kutafuta mwenza ndio mana PM nimefunga. Kuandika ni njia yangu yakujifariji.

Mbarikiwe.

Mithali 31:10-31

Umeambiwa nini?
 
Back
Top Bottom