Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Nakumbuka milikataa kwenda jeshini mzee akamind sana.

Siku zaa hivi karibuni akasema ungeenda walau na wewe ungekuwa na Noah.
 
Analyse katika ubora wake wa masimulizi.

Very interesting story lkn mambo hayapaswi kuyaacha pending.....

1. Tukio la hallucination ya Mzee mvuka barabara limeishia pending- possible was just imaginations?. Ungetupatia conclusion yake

2. Msala wa mama mwenye nyumba na kina Mzee KY ulilimalizaje jumla jumla?

3. Mzee ambaye ndiyo dhumuni la Uzi aliwahi kufanikiwa kukupatia connection- hii ni halali yetu sisi kujua maana ndiyo dhumuni la huu Uzi....
 
1. Kwa upande wangu, siwezi sema ni hallucination or imagination, kwasababu everything was real at that time. Na hata kuacha kwake, yaliacha after kurudi tena kule kwa mtaalam, maana ilifikia hatua sikua poa kabisa. Hata Yale mazungumzo niliyofanya na Mshua kwenye portion ya 22 ilikuwa ni after kurudi nomo, japo sikumuelezea ukweli nini kilitokea at that time.

2. Kuhusu Mzee KY na Mstaafu, after kubadili namba za simu, nilihama pia ule ukanda niliokuwa nakaa. After hapo nilitoka nje ya Dar kwa muda mrefu sana. Sikuwahi tafutwa au kuuliziwa anything na anyone kuhusu zile issue. Na hata nilivyorudi town, sikuwahi kabisa kutaka kujua anything, so sifahamu kabisa walichukua hatua gani.

3. Laiti angefanikiwa kunipa connection, nisingekuwa na majuto kabisa, maana huwa nashkuru kwa kila kitu. Yani pale ndio ilikuwa imetoka. Alijaribu kuniconnect sehem kadhaa, lakini Nazo hazikwenda kama tulivyotaka, maana unakaa miezi kadhaa, then panatokea changes, unapigwa chini.

Sijui nimejibu maswali yako mkuu? Kama hapana, unaweza kuuliza tena.
 
Satsfied kabisa , nashukuru.

Hapo namba moja mtaalamu alikuambia sababu ilikuwa ni nini na nani kuona vitu siyo normal?
 
Satsfied kabisa , nashukuru.

Hapo namba moja mtaalamu alikuambia sababu ilikuwa ni nini na nani kuona vitu siyo normal?
Nilimcrash kabla hajatwambia, maana shida iliyokuwepo Mshua sikumwambia ukweli on what happened wakati nipo town. Na kama yule mtaalam angeisema sababu, sidhani kama ningetoka salama pale.

Uzuri wa wale jamaa, hawawezi kusema kitu kama wewe mgonjwa/mwenye tatizo hujaruhusu. Japo Mshua alihisi kuna kitu hakipo sawa, lakini alikosa means ya kumfanya akijue. Maana sio Mimi wala yule mtaalam aliyekuwa tayari kumwambia.
 
Shukrani
 
Hii ni mara ya pili unaenda kwa mganga baada ya lile tukio la kisauti?

Pia kuna sehemu ulisema kwenye hii dunia ili uishi vizuri ni lazima uwe vizuri kwa Mungu au nguvu za giza...so where are as of now

Unaweza kutupa experience kidogo
 
Mkuu baada ya kuacha mishe na kina mzee dingi ila mzee KY ulisema kuwa uliendelea kuwasiliana nae kwa muda fulani

Mbona sijaona umetolea maelezo sababu ya kuendelea kuwasiliana na mzee KY
 
Na mim nishawah peleka mzazi fake shule niliambulia viboko tu [emoji23][emoji23][emoji23] utundu huu jamani
Umenikumbusha
Niliwahi kupeleka mzazi feki pia kumbe huyo mzazi feki alishawahi kucheza dili na yule discpline Master na wakadhurumiana. Aisee sitosahau niliishi maisha magumu sana kipindi kile
 

natia nukta.
 

ww jamaa uko na kipaji kikubwa sana cha uandishi mzur
 
Hii ni mara ya pili unaenda kwa mganga baada ya lile tukio la kisauti?

Pia kuna sehemu ulisema kwenye hii dunia ili uishi vizuri ni lazima uwe vizuri kwa Mungu au nguvu za giza...so where are as of now

Unaweza kutupa experience kidogo
Yeah hii ilikuwa ni mara ya pili, ukiachana na zile seke seke za Kisauti. Nilivyorudiga nyumbani, ile hali ya kutokewa na vitu au watu iliendelea, ndio ikabidi twende tena kwa mganga.

Yeah ili uishi vizuri, lazima uchague upande either kwa Mungu au kwa waganga, hutakiwi kuwa neutral, na hii nilikuwa nakwambia wewe kama msomaji. Bahati mbaya, wewe unataka kujua kuhusu Mimi πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…. Anyway, nilishaachana na maswala ya waganga, na hata hizi simulizi ninazowapa ni past experiences, ila bahati mbaya kadiri nilivyokuwa nasimulia, ndio wadau walivyokuwa wanakuja pm kutaka connection na waganga, na bahati mbaya wengine sio waelewa.

Lengo langu ilikuwa ni kushare nanyi my past experiences, na sio kurudi tena kwenye Yale maisha. Na ndio maana hizi sehem ambazo nilienda tena kwa waganga, nilizitoa, sikutaka kuzisimulia.

Sijajua kama nimejibu vizuri maswali yako, kama sijajibu unaweza kuuliza vizuri tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…