12th Portions:
... Maongezi yakaendelea
Mzee: "Unajua kwanini Baba yako alikuwa anataka uonane na Mimi?
Analyse: "Aliniambia unaweza kunisaidia kwenye maswala ya kazi"
Mzee: "Na mbona hukunitafuta?"
Analyse: (Kimya)
Mzee: "Alichokwambia ni kweli, ila umekuja kwa mtu sahihi, wakati usio sahihi"
Analyse: "Kivipi? "
Mzee: "Tayari nipo nje ya mfumo, wakati ule ingekuwa rahisi sana tofauti na sasa"
"Unajishughurisha na nini sasa hivi?"
Analyse: "Nipo tu Mzee, Sina shughuli maalum"
Mzee: "Una muda gani tokea uanze kutokuwa na shughuli maalum?"
Analyse: "Tokea nimemaliza chuo mambo ndio hivi hivi"
Mzee: "Kama ni hivyo, mbona kipindi chote hicho tumeshindwa kuonana, nilidhani uko busy?"
Analyse: "Kimya...."
Mzee: "Nakumbuka kama nishawahi kukupigia simu sana, ila hukupokea. Mtu ambae huna shughuli maalum, unashindwaje kupokea simu?"
Analyse: (kimya)
Mzee: "Kama kuna kitu kigumu kukielewa, basi ni jinsi vijana wa sasa mnavyofikiria. Mpo busy sana, lakini hakuna cha maana mnachofanya"
Akaendelea "Mifumo yetu hapa nchini jinsi ilivyo, ukitoka tu nje ya mfumo, ni rahisi sana kusahaulika. Wanakuona kama mzigo, hawakupi tena attention sana maana huna msaada kama mwanzo. Hata huu ufugaji na biashara tunazofanya, inakuwa ni kupunguza stress na kujiweka fit financially, maana njia za mkato zote zinapotea". "Ukistaafu, watu uliokuwa nao, wataendelea kuwa karibu na wewe kwa muda, ila kadiri muda unavyosogea ukiwa nje ya mfumo, na wao wanazidi kujiweka mbali na wewe, hatimae ushawishi uliokuwa nao unapotea wote, unabaki kuwa mtu wakawaida mbele yao"
"Baba yako alikuwa anatamani sana usome, na kama ungesoma wakati ule, ilikuwa rahisi kupata sehemu ya kukuweka, ila ukachagua njia tofauti. Haya hebu niambie, ukiachana na makovu kibao uliyokuwa nayo, kipi cha maana unachojivunia katika hizo hustling zako?
Nikabaki kimya. Nae akabaki ananiangalia tu.
Analyse: "Ila Baba hakuwahi niambia yote haya, na sikuwahi kuyajua"
Mzee: "Kwahiyo mpaka ujue faida ya unachoenda kufanya, ndio ukifanye? Haya faida za hiyo njia uliyochagua ni zipi mpaka ukaichagua?"
Nikawa kimya tena. Mzee kila akifungua mdomo, anatoa punch za kwenye mshono.
"Leo hii pakitokea dharura, inahitajika milioni 5 Kwa ajili ya matibabu ya wazazi wenu, familia nzima mkihitajika kuchangia,wewe unaweza kutoa kiasi gani in such short notice?
Nikainama tu, ningesemaje sasa?
"Zamani wazazi walikuwa wanafurahia Sana wakipata watoto wakiume. Ila siku hizi hujui kama ufurahie au la, maana hamtabiriki kabisa. Mapenzi yanawaondolea sana akili, mmekuwa kama mbwa, anayeweza kwenda umbali mrefu sana kufata jike, ila siku akija mwizi nyumbani, atamfukuza mpaka hatua chache kutoka nyumbani, kisha atamuacha. Vya maana hamvipi uzito, ila visivyo na msingi mnavifanya kwa umakini"
Akaendelea:
"Hivi unajua Mimi na Baba yako tumefahamiana vipi?"
Analyse: "Hapana"
Mzee (akasikitika): "Bure kabisa"
Baada ya hapo akatema punch zingine ambazo nilishindwa kuzihimili.
"Kama ilivyokuwa kwa Baba yako, Mimi pia nilikuwa mwanajeshi. Hatukuwa na mazoea wakati tupo kambini. Ukaribu wetu ulianza tulivyochaguliwa kwenda Urusi kwa ajili ya mafunzo maalum yakiweko ya Urubani ambako Baba yako ndio alikuwepo"
"Alikuwa room mate wangu, baada ya kufika kule. Na hata tulipohitimu mafunzo na kurudi nchini, urafiki wetu tayari ulikuwa umekomaa". Akaniuliza "Unajua kwanini yeye alitoka jeshini? "
Japo aliniuliza Mimi lile swali, ila ni kama alikuwa anaongea peke yake, maana kabla sijamjibu, akaendelea "Kipindi cha vita ya Kagera, wakati wa maandalizi ya mwisho, Mzee wako alipata tatizo la kiafya ambalo lilifanya aonekane unfit kwa wakati ule (Mzee wangu mpaka sasa anachechemea mguu mmoja)".
Akaendelea
"Pamoja na yote, Mzee wako hakutaka kutoka jeshini, akiamini atapona na kurudi nomo, ila kwa shinikizo na Babu yako, ikabidi Baba yako atoke jeshini kwa lazima. Maana walifikia hatua hadi ya kutoelewana kati yao"
"Hata nilivyorudi kutoka vitani, Mzee wako bado alikuwa na hasira na Babu yako. Tulipoteza marubani wengi wazuri, nilijaribu kumwambia pengine hata yeye angeweza kufa kama wengine, ila mpaka leo anaamini yeye angerudi mzima au ni heri kufia kule kuliko kulala kitandani"
Mzee aliongea vitu vingi sana kuhusu Mshua, vingine ndio ilikuwa mara ya kwanza navisikia.
Kiufupi yote aliyokuwa anaongea, ni kama vile alikuwa ananisema. Maana yalifanya nikajisikia vibaya sana. Wakati tunaendelea na maongezi, nikamuuliza
"Kwanini hakuwahi kunigusia chochote juu ya haya mengi? Au kwanini hakuwahi kunisisitizia umuhimu wa hii njia aliyonichagulia yeye?"
Akatoa tabasam fulani hafifu, alaf akaniambia
"Ingekuwa vipi kama angekufosi upite njia aliyoitaka yeye alafu mbeleni mambo yakafeli?"
"Babu yako wakati anamshawishi Baba yako atoke jeshini, aliahidi kumpa kiwanda chake cha upasuaji mbao ili kiwe chanzo chake cha kipato. Ila baada ya Baba yako kuacha kazi jeshini, sehemu ya kile kiwanda ilishika moto, na kwenye harakati ya uokoaji, baadhi ya vitu viliibiwa, vingi viliungua na vingine kupotea, hiyo story nadhani unaijua"
"Kilichofata, Baba yako kazi hana, na kiwanda hakipo. Baada ya hapo Baba yako na Babu yako ukaribu ulipungua sana, maana palitokea ugomvi kati yao.. Baba yako alikuwa akimlaumu sana Babu kwa mambo yake kwenda mlama, maana anaamini yeye kumtoa jeshini, ndio chanzo cha yote. Huu ukaribu kati yao unaouona umekuja hivi karibuni tu."
"Baba yako anakupenda sana, ila hawezi kukupush kwenye njia aliyochagua yeye, anakusupport unapochagua wewe, ili asijekuwa sehemu ya lawama zako, kama ambavyo yeye alishindwa kuacha kumlaumu Baba yake, bila kuangalia nia njema aliyokuwa nayo (Baba yake) kwake"
"Kati ya wanae wote, wewe ndiye anayekukubali sana. Inapotokea umemdisappoint, huwa anaumia sana, ila hawezi kukwambia. Mara nyingi huwa anasema, hivi ulivyo ni copy and paste ya kipindi chake cha ukuaji, ndio maana huwa anashindwa kukulaumu. Hata leo hii Mama yako akimwambia nyie wote sio watoto wake, wale wengine anaweza kukubali ila sio wewe".
Maongezi na Mzee yakawa kama mwiba kwangu. Kila anachoongea kinaniuma. Mzee wangu mara kadhaa amekuwa akimuuliza Bi Mkubwa kama kweli Mimi ni mwanae, au kusema nimerithi tabia ujombani, lakini kumbe uhalisia uko tofauti? Nikiwa nae tunapiga story tunacheka, najua yaliyopita yamepita na kila kitu kipo sawa, ila kumbe anaumia ndani kwa ndani?.
Pale ndio akili ikanifunguka, kumbe sio kila tabasam ni la furaha. Kumbe kicheko nacho kinaweza kikawa njia ya kuficha hudhuni?. Kuna mtu alishawahi kuniambia kuwa tabasamu ni deni, ila sikuwahi kumuelewa alimaanisha nini. Hii siku ndio nikaipata tafsiri ya alichomaanisha. Maana tabasamu ambalo amekuwa akinionesha Mshua wangu, limegeuka kuwa deni kubwa, Deni ambalo nimechelewa sana kulijua. Deni ambalo sijajua ntalilipa vipi. Hakika tabasamu la wakupendao ni deni, maana lina siri nyingi.
Akili yangu ilivurugika, mawazo yakaenda mbali sana, nikawa nakumbuka matukio ambayo nishawahi kumpitisha Mshua. Nikiwaga nyumbani kuna muda tunacheka na kufurahia sana, mbona hajawahi kunionesha kama kuna kitu kinamuumiza ndani ya nafsi yake?. Inawezekana mtu akawa na maumivu ambayo ni ngumu kuyaelezea kwa anayeyasababisha?. Je, na Mimi nitatakiwa kuja kuipitia hii hali dhidi ya wanangu? Kwamba inawezekana nisiweze kuwaelezea kila kitu ? Nitatakiwa kucheka na kufurahi mbele yao, hata kama moyoni nina majeraha?. Heri ya Mimi nimepata mtu wa kunielezea haya mambo, itakuwaje kama wanangu wasipoweza kuyajua maumivu yangu?.
Ni kwamba Mshua alitaka nije kuonana na huyu Mzee, ni Kwa ajili ya kupata connection tu au alihisi ningeweza kuyajua haya mambo?. Inabidi niongee na Mshua, ila nitaanzia wapi? Au natakiwa nikamuombe msamaha kwanza?. Atanielewa? Na mambo yaliyotokea kati yetu ni mengi sana, huo msamaha namuombaje?.
Ilifikia hatua mpaka nikawa sisikii kabisa vitu alivyoendelea kuniambia yule Mzee. Ni kama sikuwa eneo lile kabisa, usikivu ulipotea hadi yule Mzee akaniambia nirudi nyumbani kwanza nikapumzike.
Akanisisitizia kuwa kila wiki end anakuwa pale japo sipo anapoishi, kwahiyo nikiwa na muda niwe naenda kumuona ili tuzidi kuongea.
Tukaagana. Kijana wake akanisogeza tena mpaka Kongowe mwisho.
* ** ******** *****
Njia nzima najilaumu, hadi kichwa kimepata sana moto, kiasi kwamba ukinishtua naweza hata kuzimia. Nikaifikiria ile siku ambayo Mzee ananipigia simu, alaf Mimi nimeiweka silent kisa yule mpenzi wangu wa kipindi kile alikuwa anataka tukiwa pamoja tusitumie simu. Kilichoniuma zaidi sio kwamba yule manzi tumeshaachana, bali ni sababu iliyofanya tuachane. Mimi nilikuwa naamini hapendi tutumie simu tukiwa pamoja, ili akili na mawazo yetu yasiende mbali, kumbe mwenzangu alikuwa na mahusiano na jamaa mwingine, hivyo alikuwa anatengeneza mazingira ya kutokupokea simu.
Nakumbuka kuna siku, wakati ameenda kuoga, nilishika simu yake na kukuta msg toka kwa mtu aliyemsave "Suka". Msg ilimwambia aende tena kulala kwa huyo jamaa, maana ameshamiss alichompa siku iliyopita. Yaani kwangu anakuja mchana mpaka jioni, kwa Suka anaenda kuilaza. Alafu old chatting zikaonesha ni wapenzi wa muda mrefu, japo huyo jamaa amenikuta. Wakati mimi manzi namla kistaarab, Suka yeye anamgeuza atakavyo.
Wakati bado nimeishika, Suka akapiga tena, demu nae anaingia ndani, nikapokea kisha nikaweka loud. Demu hakuongea akaikata. Sikutaka hata tuzozane, nikamwambia avae aende kwa Suka. Imagine mwanamke ninayemvalue high, kumbe akienda kwa Suka, anampa jamaa honi, anaipuliza mpaka inazima.
Maumivu niliyokuwa nayafeel baada ya kutoka kwa Mzee, yaliongezeka maradufu nilipomkumbuka yule manzi, maana nilimuonaga kama wife material. Eti wife material? [emoji28][emoji28][emoji28]wife material my ass**.
Yule manzi alinifanya nikakosa connection ambayo pengine ingeweza kubadili maisha yangu.
Tunasemaga makaburi yamezika ndoto za watu wengi. Ila kwa upande mwingine mapenzi nayo yanaziua sana ndoto, huku yakituacha waotaji tuendelee kuishi kwa msoto.
Kiufupi sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, kama hii siku niliyoongea na huyu Mzee. Vitu alivyoniambia viliniondolea utulivu kabisa.
***** ******* ****** ******** ****** *****
Nilivyokuwa ndani ya daladala, ndio nikashika simu, maana muda wote ilikuwa silent, mfukoni kuepusha usumbufu kwa yule Mzee.
Nakuta missed calls saba, 6 za mpenzi wangu wa wakati huo, moja ya shangazi fulani ambae nilikuwa nae kipindi hicho anaitwa Shani. Sikuwa na mood ya kupiga simu, nikawapotezea.
Kwenda upande wa msg, nakuta msg 4, moja ya shangazi. Tatu za mpenzi wangu. Msg ya mpenzi moja iliuliza niko wapi, nyingine ilitumwa baada ya robo saa ikisema nisipomtafuta ndani ya nusu saa ijayo nisimtafute tena, tunaachana. Ya tatu aliituma hata kabla ya nusu saa aliyonipa kufika, akasema Mimi na yeye basi, nisijisumbue nae. Nikajiuliza huyu alikuwa anataka nini? Nikajaribu kumpigia, nakuta kaniblock. Nikaachana nae. Kusoma ile msg ya shangazi, ananiambia "Pitia nyumbani kwangu, nina zawadi yako", nikajisemea huku ndio pa kwenda.
Nafika kule, nikakuta msosi, nikala, ila akili yangu bado inawaza maneno ya yule Mzee tu. Ikabidi nimchane Shani kuwa mood ya shoo haikuwepo. Akanijibu "Achana na habari za shoo wewe, yani ukishiba tu akili yako inawaza kuparamiana. Hata hivyo bao la kwanza alihitajigi mood, hata uwe hutaki litakuja tu, hebu njoo huku uone."
Kumsogelea nakuta kaniletea zawadi ya PS4 na pad moja. Akaniambia "Leo nataka kukupa vitu unavyopenda tu, leo inabidi ufurahi"
Mood yangu taratibu ikaanza kurudi. Nikamuuliza "Mbona unasema hivyo, kuna zawadi nyingine kwani? Akasema sio zawadi, ni taarifa. Nikamuuliza taarifa gani? Akasema "Nipo tayari sasa, nataka tuzae".
Nilikuwa bado nimeishika ile PS4 mkononi, ikabidi niiweke mezani, kisha nikae ili nimuone vizuri.
Analyse: "Uzae na nani? Kwani nimekwambia nataka mtoto Mimi?"
Shani: "Mbona umeshtuka hivyo, kwani kuna tatizo tukipata mtoto?"
Analyse: : "Nyumbani familia hawawezi kukubali ili jambo"
Shani: "Kwani nazaa na familia au nazaa na wewe, hebu nipishe mie"
Analyse: "Hicho kitu hakipo"
Shani: "Tena usinitibue, hii siku kwangu ni nzuri, mwanaume mzima unaogopa kuwa na mtoto. Na ntawapigia familia yako wote niwachambe, maana wanataka kukuendesha. Wewe mtu mzima, jisimamie"
Nikawahi kuchukua simu yangu ili asije kuiba namba zao mule, maana Kwa akili yake hashindwi kuwapigia kweli.
Akaishia kucheka tu. Alafu akasema;
Shani: "Namba za wakwe ninazo siku nyingi sana, nitaanza na wifi, yeye ndio ataambia na wengine"
Hata hamu na ile zawadi ya PS4 ilikata...
Endelea hapa
Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee