Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

12th Portions:

... Maongezi yakaendelea

Mzee: "Unajua kwanini Baba yako alikuwa anataka uonane na Mimi?
Analyse: "Aliniambia unaweza kunisaidia kwenye maswala ya kazi"
Mzee: "Na mbona hukunitafuta?"
Analyse: (Kimya)
Mzee: "Alichokwambia ni kweli, ila umekuja kwa mtu sahihi, wakati usio sahihi"
Analyse: "Kivipi? "
Mzee: "Tayari nipo nje ya mfumo, wakati ule ingekuwa rahisi sana tofauti na sasa"

"Unajishughurisha na nini sasa hivi?"
Analyse: "Nipo tu Mzee, Sina shughuli maalum"
Mzee: "Una muda gani tokea uanze kutokuwa na shughuli maalum?"
Analyse: "Tokea nimemaliza chuo mambo ndio hivi hivi"
Mzee: "Kama ni hivyo, mbona kipindi chote hicho tumeshindwa kuonana, nilidhani uko busy?"
Analyse: "Kimya...."
Mzee: "Nakumbuka kama nishawahi kukupigia simu sana, ila hukupokea. Mtu ambae huna shughuli maalum, unashindwaje kupokea simu?"
Analyse: (kimya)
Mzee: "Kama kuna kitu kigumu kukielewa, basi ni jinsi vijana wa sasa mnavyofikiria. Mpo busy sana, lakini hakuna cha maana mnachofanya"

Akaendelea "Mifumo yetu hapa nchini jinsi ilivyo, ukitoka tu nje ya mfumo, ni rahisi sana kusahaulika. Wanakuona kama mzigo, hawakupi tena attention sana maana huna msaada kama mwanzo. Hata huu ufugaji na biashara tunazofanya, inakuwa ni kupunguza stress na kujiweka fit financially, maana njia za mkato zote zinapotea". "Ukistaafu, watu uliokuwa nao, wataendelea kuwa karibu na wewe kwa muda, ila kadiri muda unavyosogea ukiwa nje ya mfumo, na wao wanazidi kujiweka mbali na wewe, hatimae ushawishi uliokuwa nao unapotea wote, unabaki kuwa mtu wakawaida mbele yao"

"Baba yako alikuwa anatamani sana usome, na kama ungesoma wakati ule, ilikuwa rahisi kupata sehemu ya kukuweka, ila ukachagua njia tofauti. Haya hebu niambie, ukiachana na makovu kibao uliyokuwa nayo, kipi cha maana unachojivunia katika hizo hustling zako?

Nikabaki kimya. Nae akabaki ananiangalia tu.

Analyse: "Ila Baba hakuwahi niambia yote haya, na sikuwahi kuyajua"
Mzee: "Kwahiyo mpaka ujue faida ya unachoenda kufanya, ndio ukifanye? Haya faida za hiyo njia uliyochagua ni zipi mpaka ukaichagua?"

Nikawa kimya tena. Mzee kila akifungua mdomo, anatoa punch za kwenye mshono.

"Leo hii pakitokea dharura, inahitajika milioni 5 Kwa ajili ya matibabu ya wazazi wenu, familia nzima mkihitajika kuchangia,wewe unaweza kutoa kiasi gani in such short notice?

Nikainama tu, ningesemaje sasa?

"Zamani wazazi walikuwa wanafurahia Sana wakipata watoto wakiume. Ila siku hizi hujui kama ufurahie au la, maana hamtabiriki kabisa. Mapenzi yanawaondolea sana akili, mmekuwa kama mbwa, anayeweza kwenda umbali mrefu sana kufata jike, ila siku akija mwizi nyumbani, atamfukuza mpaka hatua chache kutoka nyumbani, kisha atamuacha. Vya maana hamvipi uzito, ila visivyo na msingi mnavifanya kwa umakini"

Akaendelea:

"Hivi unajua Mimi na Baba yako tumefahamiana vipi?"

Analyse: "Hapana"
Mzee (akasikitika): "Bure kabisa"

Baada ya hapo akatema punch zingine ambazo nilishindwa kuzihimili.

"Kama ilivyokuwa kwa Baba yako, Mimi pia nilikuwa mwanajeshi. Hatukuwa na mazoea wakati tupo kambini. Ukaribu wetu ulianza tulivyochaguliwa kwenda Urusi kwa ajili ya mafunzo maalum yakiweko ya Urubani ambako Baba yako ndio alikuwepo"

"Alikuwa room mate wangu, baada ya kufika kule. Na hata tulipohitimu mafunzo na kurudi nchini, urafiki wetu tayari ulikuwa umekomaa". Akaniuliza "Unajua kwanini yeye alitoka jeshini? "

Japo aliniuliza Mimi lile swali, ila ni kama alikuwa anaongea peke yake, maana kabla sijamjibu, akaendelea "Kipindi cha vita ya Kagera, wakati wa maandalizi ya mwisho, Mzee wako alipata tatizo la kiafya ambalo lilifanya aonekane unfit kwa wakati ule (Mzee wangu mpaka sasa anachechemea mguu mmoja)".

Akaendelea

"Pamoja na yote, Mzee wako hakutaka kutoka jeshini, akiamini atapona na kurudi nomo, ila kwa shinikizo na Babu yako, ikabidi Baba yako atoke jeshini kwa lazima. Maana walifikia hatua hadi ya kutoelewana kati yao"

"Hata nilivyorudi kutoka vitani, Mzee wako bado alikuwa na hasira na Babu yako. Tulipoteza marubani wengi wazuri, nilijaribu kumwambia pengine hata yeye angeweza kufa kama wengine, ila mpaka leo anaamini yeye angerudi mzima au ni heri kufia kule kuliko kulala kitandani"

Mzee aliongea vitu vingi sana kuhusu Mshua, vingine ndio ilikuwa mara ya kwanza navisikia.

Kiufupi yote aliyokuwa anaongea, ni kama vile alikuwa ananisema. Maana yalifanya nikajisikia vibaya sana. Wakati tunaendelea na maongezi, nikamuuliza

"Kwanini hakuwahi kunigusia chochote juu ya haya mengi? Au kwanini hakuwahi kunisisitizia umuhimu wa hii njia aliyonichagulia yeye?"

Akatoa tabasam fulani hafifu, alaf akaniambia

"Ingekuwa vipi kama angekufosi upite njia aliyoitaka yeye alafu mbeleni mambo yakafeli?"

"Babu yako wakati anamshawishi Baba yako atoke jeshini, aliahidi kumpa kiwanda chake cha upasuaji mbao ili kiwe chanzo chake cha kipato. Ila baada ya Baba yako kuacha kazi jeshini, sehemu ya kile kiwanda ilishika moto, na kwenye harakati ya uokoaji, baadhi ya vitu viliibiwa, vingi viliungua na vingine kupotea, hiyo story nadhani unaijua"

"Kilichofata, Baba yako kazi hana, na kiwanda hakipo. Baada ya hapo Baba yako na Babu yako ukaribu ulipungua sana, maana palitokea ugomvi kati yao.. Baba yako alikuwa akimlaumu sana Babu kwa mambo yake kwenda mlama, maana anaamini yeye kumtoa jeshini, ndio chanzo cha yote. Huu ukaribu kati yao unaouona umekuja hivi karibuni tu."

"Baba yako anakupenda sana, ila hawezi kukupush kwenye njia aliyochagua yeye, anakusupport unapochagua wewe, ili asijekuwa sehemu ya lawama zako, kama ambavyo yeye alishindwa kuacha kumlaumu Baba yake, bila kuangalia nia njema aliyokuwa nayo (Baba yake) kwake"

"Kati ya wanae wote, wewe ndiye anayekukubali sana. Inapotokea umemdisappoint, huwa anaumia sana, ila hawezi kukwambia. Mara nyingi huwa anasema, hivi ulivyo ni copy and paste ya kipindi chake cha ukuaji, ndio maana huwa anashindwa kukulaumu. Hata leo hii Mama yako akimwambia nyie wote sio watoto wake, wale wengine anaweza kukubali ila sio wewe".

Maongezi na Mzee yakawa kama mwiba kwangu. Kila anachoongea kinaniuma. Mzee wangu mara kadhaa amekuwa akimuuliza Bi Mkubwa kama kweli Mimi ni mwanae, au kusema nimerithi tabia ujombani, lakini kumbe uhalisia uko tofauti? Nikiwa nae tunapiga story tunacheka, najua yaliyopita yamepita na kila kitu kipo sawa, ila kumbe anaumia ndani kwa ndani?.

Pale ndio akili ikanifunguka, kumbe sio kila tabasam ni la furaha. Kumbe kicheko nacho kinaweza kikawa njia ya kuficha hudhuni?. Kuna mtu alishawahi kuniambia kuwa tabasamu ni deni, ila sikuwahi kumuelewa alimaanisha nini. Hii siku ndio nikaipata tafsiri ya alichomaanisha. Maana tabasamu ambalo amekuwa akinionesha Mshua wangu, limegeuka kuwa deni kubwa, Deni ambalo nimechelewa sana kulijua. Deni ambalo sijajua ntalilipa vipi. Hakika tabasamu la wakupendao ni deni, maana lina siri nyingi.

Akili yangu ilivurugika, mawazo yakaenda mbali sana, nikawa nakumbuka matukio ambayo nishawahi kumpitisha Mshua. Nikiwaga nyumbani kuna muda tunacheka na kufurahia sana, mbona hajawahi kunionesha kama kuna kitu kinamuumiza ndani ya nafsi yake?. Inawezekana mtu akawa na maumivu ambayo ni ngumu kuyaelezea kwa anayeyasababisha?. Je, na Mimi nitatakiwa kuja kuipitia hii hali dhidi ya wanangu? Kwamba inawezekana nisiweze kuwaelezea kila kitu ? Nitatakiwa kucheka na kufurahi mbele yao, hata kama moyoni nina majeraha?. Heri ya Mimi nimepata mtu wa kunielezea haya mambo, itakuwaje kama wanangu wasipoweza kuyajua maumivu yangu?.

Ni kwamba Mshua alitaka nije kuonana na huyu Mzee, ni Kwa ajili ya kupata connection tu au alihisi ningeweza kuyajua haya mambo?. Inabidi niongee na Mshua, ila nitaanzia wapi? Au natakiwa nikamuombe msamaha kwanza?. Atanielewa? Na mambo yaliyotokea kati yetu ni mengi sana, huo msamaha namuombaje?.

Ilifikia hatua mpaka nikawa sisikii kabisa vitu alivyoendelea kuniambia yule Mzee. Ni kama sikuwa eneo lile kabisa, usikivu ulipotea hadi yule Mzee akaniambia nirudi nyumbani kwanza nikapumzike.

Akanisisitizia kuwa kila wiki end anakuwa pale japo sipo anapoishi, kwahiyo nikiwa na muda niwe naenda kumuona ili tuzidi kuongea.

Tukaagana. Kijana wake akanisogeza tena mpaka Kongowe mwisho.


* *** ***** ******** *****

Njia nzima najilaumu, hadi kichwa kimepata sana moto, kiasi kwamba ukinishtua naweza hata kuzimia. Nikaifikiria ile siku ambayo Mzee ananipigia simu, alaf Mimi nimeiweka silent kisa yule mpenzi wangu wa kipindi kile alikuwa anataka tukiwa pamoja tusitumie simu. Kilichoniuma zaidi sio kwamba yule manzi tumeshaachana, bali ni sababu iliyofanya tuachane. Mimi nilikuwa naamini hapendi tutumie simu tukiwa pamoja, ili akili na mawazo yetu yasiende mbali, kumbe mwenzangu alikuwa na mahusiano na jamaa mwingine, hivyo alikuwa anatengeneza mazingira ya kutokupokea simu.

Nakumbuka kuna siku, wakati ameenda kuoga, nilishika simu yake na kukuta msg toka kwa mtu aliyemsave "Suka". Msg ilimwambia aende tena kulala kwa huyo jamaa, maana ameshamiss alichompa siku iliyopita. Yaani kwangu anakuja mchana mpaka jioni, kwa Suka anaenda kuilaza. Alafu old chatting zikaonesha ni wapenzi wa muda mrefu, japo huyo jamaa amenikuta. Wakati mimi manzi namla kistaarab, Suka yeye anamgeuza atakavyo.

Wakati bado nimeishika, Suka akapiga tena, demu nae anaingia ndani, nikapokea kisha nikaweka loud. Demu hakuongea akaikata. Sikutaka hata tuzozane, nikamwambia avae aende kwa Suka. Imagine mwanamke ninayemvalue high, kumbe akienda kwa Suka, anampa jamaa honi, anaipuliza mpaka inazima.

Maumivu niliyokuwa nayafeel baada ya kutoka kwa Mzee, yaliongezeka maradufu nilipomkumbuka yule manzi, maana nilimuonaga kama wife material. Eti wife material? [emoji28][emoji28][emoji28]wife material my ass**.

Yule manzi alinifanya nikakosa connection ambayo pengine ingeweza kubadili maisha yangu.

Tunasemaga makaburi yamezika ndoto za watu wengi. Ila kwa upande mwingine mapenzi nayo yanaziua sana ndoto, huku yakituacha waotaji tuendelee kuishi kwa msoto.

Kiufupi sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, kama hii siku niliyoongea na huyu Mzee. Vitu alivyoniambia viliniondolea utulivu kabisa.

***** ******* ****** ******** ****** *****

Nilivyokuwa ndani ya daladala, ndio nikashika simu, maana muda wote ilikuwa silent, mfukoni kuepusha usumbufu kwa yule Mzee.

Nakuta missed calls saba, 6 za mpenzi wangu wa wakati huo, moja ya shangazi fulani ambae nilikuwa nae kipindi hicho anaitwa Shani. Sikuwa na mood ya kupiga simu, nikawapotezea.

Kwenda upande wa msg, nakuta msg 4, moja ya shangazi. Tatu za mpenzi wangu. Msg ya mpenzi moja iliuliza niko wapi, nyingine ilitumwa baada ya robo saa ikisema nisipomtafuta ndani ya nusu saa ijayo nisimtafute tena, tunaachana. Ya tatu aliituma hata kabla ya nusu saa aliyonipa kufika, akasema Mimi na yeye basi, nisijisumbue nae. Nikajiuliza huyu alikuwa anataka nini? Nikajaribu kumpigia, nakuta kaniblock. Nikaachana nae. Kusoma ile msg ya shangazi, ananiambia "Pitia nyumbani kwangu, nina zawadi yako", nikajisemea huku ndio pa kwenda.

Nafika kule, nikakuta msosi, nikala, ila akili yangu bado inawaza maneno ya yule Mzee tu. Ikabidi nimchane Shani kuwa mood ya shoo haikuwepo. Akanijibu "Achana na habari za shoo wewe, yani ukishiba tu akili yako inawaza kuparamiana. Hata hivyo bao la kwanza alihitajigi mood, hata uwe hutaki litakuja tu, hebu njoo huku uone."

Kumsogelea nakuta kaniletea zawadi ya PS4 na pad moja. Akaniambia "Leo nataka kukupa vitu unavyopenda tu, leo inabidi ufurahi"

Mood yangu taratibu ikaanza kurudi. Nikamuuliza "Mbona unasema hivyo, kuna zawadi nyingine kwani? Akasema sio zawadi, ni taarifa. Nikamuuliza taarifa gani? Akasema "Nipo tayari sasa, nataka tuzae".

Nilikuwa bado nimeishika ile PS4 mkononi, ikabidi niiweke mezani, kisha nikae ili nimuone vizuri.

Analyse: "Uzae na nani? Kwani nimekwambia nataka mtoto Mimi?"
Shani: "Mbona umeshtuka hivyo, kwani kuna tatizo tukipata mtoto?"
Analyse: : "Nyumbani familia hawawezi kukubali ili jambo"
Shani: "Kwani nazaa na familia au nazaa na wewe, hebu nipishe mie"
Analyse: "Hicho kitu hakipo"
Shani: "Tena usinitibue, hii siku kwangu ni nzuri, mwanaume mzima unaogopa kuwa na mtoto. Na ntawapigia familia yako wote niwachambe, maana wanataka kukuendesha. Wewe mtu mzima, jisimamie"

Nikawahi kuchukua simu yangu ili asije kuiba namba zao mule, maana Kwa akili yake hashindwi kuwapigia kweli.

Akaishia kucheka tu. Alafu akasema;

Shani: "Namba za wakwe ninazo siku nyingi sana, nitaanza na wifi, yeye ndio ataambia na wengine"

Hata hamu na ile zawadi ya PS4 ilikata...
Imebidi nirudie tena kuisoma mara ya pili. Hasa sahemu ya maneno ya mzee. Hakika yamekuwa mwiba,japo ni madini ya uhakika. Yanaacha ujumbe mzito sana kwenye dunia ya vijana. Kweli utu uzima dawa. Mzee ana mawe mazito yenye madini.

Mpaka nikajisemea kumbe kuna kheri fulani kwa sisi tuliozika baba zetu hata bila kupata mapenzi yao. Yaani nikiwa mtoto wa miaka minne tu. Angalau najihisi hakuwahi kupitia maumivu yangu,ingawa sio wazazi wote wanaweza kupitia hayo. Ila angekuwa hai nina uhakika kwangu pia angepita kwenye maumivu,japo yanaweza kuwa ya tofauti,lakini Naamini maumivu ya mzazi kwa mwanae ni yale yale tu.

Kitu kimetulia mwamba. Hasa hii episode imetufunza jambo. Hasa kuhusiana na safari yetu ya maisha. Hasa kuhusiana na mapenzi. Hasa kuhusiana na wazazi wetu
 
Heri Mimi narusha moja kila siku. Ila kule kwingine ni kipande kimoja kila baada ya siku 3 au 4 😅😅😅😅.

Nilikuwa narusha vipande viwili sababu nilikuwa napata muda wa kutosha. Ila kuanzia jana mpaka inaisha, tutarudi mwendo wa portion moja per day kama tulivyoanza 😅😅
Sawa bosi,vyote sawa tuuu
 
Imebidi nirudie tena kuisoma mara ya pili. Hasa sahemu ya maneno ya mzee. Hakika yamekuwa mwiba,japo ni madini ya uhakika. Yanaacha ujumbe mzito sana kwenye dunia ya vijana. Kweli utu uzima dawa. Mzee ana mawe mazito yenye madini.

Mpaka nikajisemea kumbe kuna kheri fulani kwa sisi tuliozika baba zetu hata bila kupata mapenzi yao. Yaani nikiwa mtoto wa miaka minne tu. Angalau najihisi hakuwahi kupitia maumivu yangu,ingawa sio wazazi wote wanaweza kupitia hayo. Ila angekuwa hai nina uhakika kwangu pia angepita kwenye maumivu,japo yanaweza kuwa ya tofauti,lakini Naamini maumivu ya mzazi kwa mwanae ni yale yale tu.

Kitu kimetulia mwamba. Hasa hii episode imetufunza jambo. Hasa kuhusiana na safari yetu ya maisha. Hasa kuhusiana na mapenzi. Hasa kuhusiana na wazazi wetu
Kweli mkuu,kwenye mapenzi usipokuwa makini unaharibu Mambo na mipango mingi ya maana.
Ukijashtukia unaanza kujilaumu,hasahasa km hayo mapenzi yatapukutika baada ya muda
Heri Mimi narusha moja kila siku. Ila kule kwingine ni kipande kimoja kila baada ya siku 3 au 4 😅😅😅😅.

Nilikuwa narusha vipande viwili sababu nilikuwa napata muda wa kutosha. Ila kuanzia jana mpaka inaisha, tutarudi mwendo wa portion moja per day kama tulivyoanza 😅😅
Kuna story yako moja ulisema una mtoto ulizaa na shangazi mmoja hivi,dogo hajambo ??
 
Kweli mkuu,kwenye mapenzi usipokuwa makini unaharibu Mambo na mipango mingi ya maana.
Ukijashtukia unaanza kujilaumu,hasahasa km hayo mapenzi yatapukutika baada ya muda

Kuna story yako moja ulisema una mtoto ulizaa na shangazi mmoja hivi,dogo hajambo ??
Dogo Yuko poa kabisa mkuu
 
Moja ya nondo nzito kuibeba.......hakika vijana tunamiss wazee kama hawa maishani mwetu
IMG_20230402_150113.jpg
 
Ambacho haujui mkuu, ukiandika, unahitaji urefresh kidogo akili irudi sawa. Sio rahisi kuandika continuously alaf vitu vikaeleweka mpaka wewe msomaji ukaridhika.

Makubaliano ni kwamba nitakuwa napost kila siku baada ya iftar, mpaka story iishe. Nisipo post, ruksa kunilaumu. Huu Muda mwingine nje ya hapo, niachie na Mimi nirefresh JF[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
daaah humu ukijitusu ulete story sasa mtunzi unakuwa kama mtumwa, huna kazi nyingine wewe ni kulete story tu.

Wapeni nafsi watunzi nao wana majukumu yao, wanhitaji kurefresh hata kuinatarct na watu wao humu.

Ukionekana online na hujapost mzigo basi unaonekana kero au unadharau wapenda hadith.

Analyse hajawahi acha hadithi njiani.
 
13th Portion:



... Sikuwa na kitu nilichoweza kufanya kwa wakati ule. Hata kama ningesema nimbembeleze, still isingefanya kazi, maana sijui dhamira yake halisi ni ipi.

Sikutaka hata kulala pale. Nikaamua kurudi gheto kwangu, PS4 yake nikamuacha nayo.

Njia nzima kichwa kimezongwa na mawazo hasa juu ya yale mazungumzo na yule Mzee. Kuna muda unaweza ukawa umezungukwa na watu wengi, alaf wasiwe na faida, na wale wachache wenye faida pia usiweze kuwatambua. Kutwa nalalamika maisha magumu, michongo hakuna, alaf watu wenye uwezo wa kunipa michongo ndio nawapotezea, Kisha nakumbatia wasio na umuhimu.

Usingizi ulinipaa kabisa. Niliwaza mengi sana, kiasi kwamba nikajikuta namtumia msg yule Mzee kuomba kuonana nae tena siku inayofuata. Sikutegemea anijibu muda ule ule, maana ilikuwa ni karibia saa nane kasoro. Niliendelea kuwaza mambo tofauti tofauti mpaka nilipopitiwa na usingizi.

***** ****** ****** ******

Asubuhi niliamshwa na mlio wa simu yangu, iliyokuwa ikiita. Kuiangalia nakuta Mshua ndio anapiga. Sijui kwanini, ila nilishtuka sana. Nikajikuta naogopa kuipokea ile simu, maana najiuliza anataka kuniambia nini?. Yule Mzee amemwambia kama tumeonana? Au nikipokea nitaweza kuongea na comfortable?. Ushawahi kufanya jambo fulani la aibu sana, alafu ukutane na mtu au watu wanaolifahamu, huwa unapoteza ule uchangamfu mbele yao. Hata katika story utakazopiga nao, wakicheka utahisi wanakucheka ile aibu yako. Hiyo hali ndio nilikuwa najihisi muda huo wakati Mshua anapiga. Kwa mara ya kwanza nikashindwa kupokea simu ya Mshua. Ikaita hadi ikakata.

Nikiwa bado nipo pale pale kitandani, simu ikaanza kuita tena. Nilishtuka kana kwamba nimepigwa shoti ya umeme. Nilishusha pumzi za amani baada ya kuona jina la mpigaji. Ni yule Mzee ndio alikuwa ananipigia. Niliipokea, tukaongea mambo kadhaa, ila akaniambia Kwa hiyo siku hatokuwa na nafasi, lakini pia hata siku zinazofata, bado angekuwa busy. Hivyo akashauri kama alivyoniambia jana, kuwa wik end ndio ratiba yake inakuwa wazi. Tukakubaliana niende tena kule kule shambani kwake, siku ya jumamosi.

Baada ya kukata simu, mawazo yakanirudia tena. Picha ikanijia, ni Kwa namna gani masaa 24 yanaweza kubadili kila kitu. Maana ni ndani ya masaa 24, kutoka kuwa mtu anayeongea na Baba yake kwa vicheko na bashasha, hadi kuanza kumuogopa.

Baada ya masaa kadhaa ya kujivuta vuta pale kitandani, nikaanza kutafakari siku yangu niipeleke vipi. Unajua tatizo la kuwa jobless, ni kwamba unakuwa na muda mwingi sana, ila vitu vya maana vya kufanya ndio hakuna.

Baada ya kuwaza sana, nikaona ngoja niende kule maeneo ya katikati ya jiji, nikamtafute Mzee Dingi. Jamaa alitembea na karibia million 15, huku pakiwa na karibia million 6 ya kina Kisauti, ambayo hakuitolea jasho kabisa. Mawazo yakaniambia nimtafute walau nipate mgao wangu, maana tayari nishatumikia adhabu.

Nikasogea hadi maeneo ya Samora, ila hakuwepo. Nikatembelea vijiwe vyake vyote ila nikaambulia patupu, sielewi nampatia wapi. Kwenye simu bado kaniblock. Nikafikiria kwenda kwa Shani, ila nikaona tutaenda kulumbana, alaf ugomvi uzidi kuwa mkubwa. Nikajaribu kumpigia yule mpenzi wangu, nikakuta bado kaniblock. Nikaamua kurudi zangu home.

** * ***

Zilipita kama siku mbili hivi, Mzee Dingi akanipigia simu.

Mzee Dingi: "Uko wapi Apostle?"
Analyse: "Nipo gheto, vipi?"
Mzee Dingi: "Najua bado una hasira, ila wanaume hatuwekagi vinyongo, njoo tufanye kazi"
Analyse: "Nyie fanyeni tu mtajirike, Mimi Sina mpango na hizo kazi zenu"
Mzee Dingi: "Dogo mambo hayaendi hivyo, hakuna tuzo kwa ajili ya watu wanaopata hela kwa shida. Kazi zipo nyingi, utapata hela, na utasahau habari ya ilo deni unalonidai"
Analyse: "Siwezi fanya kazi alaf nimfaidishe mtu mwingine, nyie fanyeni tu ambao mnawezana"
Mzee Dingi: "Ile ilitokea tu, kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Safari hii tutakuwa mguu kwa mguu apostle"

Nikajifikiria kwa muda kidogo, nafsi ikawa mguu nje mguu ndani, Sina mchongo town, bills nitazilipa vipi?
Nikamuuliza, "Kuna dili gani sasa hivi?"
Mzee Dingi: "Hayo sio mambo yakuongelea kwenye simu, kesho njoo ofisini tujadiliane kwa kina"
Analyse: "Sina nauli, kama hatuwezi kuongea kwenye simu, Mimi siji"

Hakunijibu kitu, akakata simu. Alafu baada ya kama dakika tatu, ikaingia elfu sabini kwenye tigopesa toka kwa Mzee Dingi, Kisha akaniandikia msg.

"Kesho fanya juu chini uje Apostle. Usiende makao makuu, njoo tawi la kinondoni"

Nikamjibu "Poa"

Unajua kupambana kunaumiza, ila kukata tamaa kunaumiza zaidi. Maana aliyekata tamaa hana dira, anaweza kujikuta anafanya mambo ambayo hakuwahi kutarajia. Story na yule Mzee zilinifanya nikajiona hopeless sana. Nikajikuta nimeridhia kwa moyo mmoja kujiunga na kina Mzee Dingi.

. ***** ***** ***** ******

Kesho yake nikatimba pande za Kino, nikakuta timu ya watu watatu, Mzee Dingi akafanya utambulisho. Nikajiunga nao rasmi.

Tulijadili mipango kadhaa, na tokea siku ile tukaanza kupiga dili kulingana na zinavyokuja. Siwezi elezea in details ni kwanma gani tulikuwa tunafanikisha hizo deals, ni watu gani tuliwapiga au hata kuyataja hayo madili, maana sio lengo la story lakini pia huwezi jua nani anasoma, nisijekuamsha hasira zilizolala.

Tulikuwa tunahama vijiwe kadiri tunavyopiga dili, ili kuepuka kukutana na wale tunaowapiga. Wengi tuliokuwa tunawapiga, michongo yote ilikuwa based on coincidences, ndio maana baada ya kuspend time sana na kina Mzee Dingi, I will never ever believe in coincidence, NEVER.

Baada ya kama miezi miwili au mitatu, Mzee Dingi akaniomba tukutane wawili tu, Mimi na yeye. Tulikutana baa maeneo ya buguruni.

Mzee Dingi: "Apostle kuna mtu anataka kukutana na wewe. Kuna dili limejitokeza"
Analyse: "Ni nani huyo? Na kwanini atake kukutana na Mimi?"atake
Mzee Dingi: "Huyu mtu shoo zake sio ndogo ndogo Apostle. Dili zake zote ni mikia ya kondoo"
Analyse: "Mikia ya kondoo kivipi?"
Mzee Dingi: "Huyu kwa mwaka akipiga dili nyingi ni nne, ila mkwanja unaopatikana hapo, unaweza kwenda likizo muda mrefu, tena kwa mtoto kama wewe, unaweza Kaa hata mwaka bila stress ya kipato, ni matumizi tu"
Analyse: "Duh anaitwa nani huyo Mzee?"
Mzee Dingi: "Jina lake la kazi tunamuita Kesho Yetu"
Analyse: "Kwanini sasa anataka kuonana na Mimi?"
Mzee Dingi: "Wewe fanya mpango kesho tuonane nae pale Kinondoni, kuna dili analeta, linahitaji watu kadhaa, na wewe ametaka uwepo"
Analyse: "Ananijua kwani?"
Mzee Dingi: " Ndio anakujua, ameona kazi kadhaa ulizoshiriki, uchangamfu na usharp wako ndio anautaka"

Nikaguna pale, ila mwisho wa siku tukakubaliana, kesho yake tukutane pale Kino...

***** ****** ****** *****

Kesho yake asubuhi na mapema nikatimba Kinondoni Manyanya. Nikamcheki Mzee Dingi, akanielekeza walipokuwa wamekaa. Yupo yeye, mwanasheria feki, na Mzee mwingine ambae ndio ilikuwa mara ya kwanza namuona, kwa jina la kazi alikuwa anafahamika kama Kidevu.

Kitu kingine nilichonote, hawa jamaa wote hakuna aliyekuwa anafahamika kwa jina lake halisi. Na hiyo ndio sababu ilifanya Mimi niwaache waendelee kuniita apostle. Na kingine hakuna aliyekuwa anajulikana anapokaa. Kiufupi, ingetokea mmoja akakamatwa, angeishia kutaja majina ya apostle, Mzee Dingi, Kidevu au Kesho Yetu. Akiambiwa akaoneshe wanapokaa hao watu, wangezunguka Dar nzima.

Baada ya utambulisho. Mchongo mzima ukawekwa mezani. Kulikuwa na mwalim mstaafu ametoka kuchukua mafao yake. Yule mwalim alikuwa anahitaji eneo kubwa kwa ajili ya mradi wake wa green house aliotaka kuuanzisha. Lakini pia, alikuwa anahitaji vifaa kwa ajili ya umwagiliaji, na kuchimbiwa kisima kwenye ilo eneo atakalo nunua. Sasa mpango ilikuwa apigwe kwenye eneo, alafu dili likisha kamilika, apigwe kwenye vifaa na uchimbaji.

Mzee Dingi yeye alitakiwa kucheza kama dalali wa eneo linalouzwa, mwanasheria feki na yule Mzee Kidevu, wao wawe majirani, Mimi nikaambiwa niwe kama afisa mtendaji au mwenyekiti wa kile Kijiji. Mzee Dingi ananiambia:

"Wewe apostle inabidi uwe mtendaji wa kile Kijiji. Unajua watendaji wengi ni vijana na wasomi. Ni rahisi yule Mama kuamini"

Nikabaki na mwangalia tu. Akaendelea

"Yule Mama tukishamaliza kuuziana nae kiwanja, itabidi hapo hapo wewe (Mimi) kama mtendaji umwambie unaweza kumsaidia kutafuta kampuni ya uchimbaji visima, na kuweka set up nzima ya kila kitu kwa ajili ya project yake".

"Yani inabidi tukimaliza tu kulipana hela za kiwanja, malipo ya hizo process zingine yafatie. Kuna watu tutakuunganisha nao ambao ndio utaendelea nao kwenye hiyo nngwe ya pili"

Wakati tunaendelea kuongea pale. Kuna Mzee mwingine akaja, yuko smart, kabeba begi muundo wa briefcase au zile za kubebea laptop. Yule Mzee sidhani kama kuna mhuri ambao hana. Kibriefcase chake Kiko full, mihuri, Karatasi, Calculator nk. Akatoa mihuri kadhaa akaiweka mezani. Eneo ambalo alitakiwa akauziwe yule mstaafu, lilikuwa vigwaza. Huyu Mzee smart aliyeongezeka, ndio Mzee Dingi akanitambulisha kwake kama 'Kesho Yetu'. Huyu ndio alikuwa mastermind wa huu mchongo wote, na ndiye aliyetakiwa kuact kama muuzaji wa eneo. Na Kwa mujibu wao, tulitarajia kati ya million 50 mpaka 70, kutegemeana na namna tutakavyofatisha maelekezo ya Mzee Kesho Yetu.

Kila kitu kikawekwa sawa, then yule mstaafu akapigiwa simu, na makubaliano yakafikiwa kuwa kesho akalione lile eneo.

Unajua sometime unaweza Sikia story mtu katapeliwa,alafu ukaanza kumcheka na kumuona mjinga, ila huyu Mzee Kesho Yetu alinibadilisha mtazamo wangu. Mtu akitapeliwa, usimlaumu sana, peleka sifa kwa yule aliyemtapeli. Watu wana mahesabu makali sana, jinsi huyu Mzee Kesho Yetu alivyokuwa anapanga mambo, accuracy yake ni almost 100%. Kinachotakiwa ni kufatisha maelekezo yake tu.

Na hata dili nyingi ndogo ndogo tulizokuwa tunafanya na kina Mzee Dingi, zilikuwa zinatoka kwake zikiwa na full deatils ya kuzipush. Yeye alikuwa anapewa percent fulani ya mgao, alikuwa hashiriki. Ukiona kashiriki, basi ilo dili liko very serious, na target sio chini ya million 50. Na hata hii deal nilidhani usharp na usmart wangu ndio ulifanya anielewe na kuniunganisha kama jinsi Mzee Dingi alivyoniambia, lakin kumbe alikuwa na sababu ya tofauti kabisa. Kitu ambacho sikuwahi kukifikiria kabisa, ila yeye kwa upande wake alishakifikiria miezi mingi iliyopita. Na jibu alilipata ni "Apostle". Nilikuwa funguo yake bila hata ya Mimi mwenyewe kujua.

Tulivyoagana, wakati wengine washaanza kuondoka, nikamsimamisha Mzee Dingi.

Analyse: "Mzee hii deal inahusisha sura ngeni nyingi, na pia hela yake ni ndefu, kuna kila dalili ya kudhurumiwa hapa"
Mzee Dingi: "Apostle unaongea nini wewe?. Hakuna wa kukudhurumu hapa"

Nikamsikiliza tu, lakini sikuwa na amani kabisa.

Tukaagana nikaamsha. Mida ya jioni jioni, Mzee Dingi akaniwekea laki mbili kwenye simu. Kisha akanipigia

Mzee Dingi: "Apostle najua utakuwa na uhitaji wa hela, chukua hiyo, piga ua kesho inabidi utokee"
Analyse: "Tunakutania wapi?"
Mzee Dingi: "Wewe na wale wengine mtatangulia asubuhi sana. Mimi nitakuja na yule mlengwa baadae."
Analyse: "Poa poa"
Mzee Dingi: "Maelezo ya ziada utayapata kule kule, hakikisha unakuwa smart sana, usisahau begi lako"
Analyse: "Sawa nimeelewa "

Alivyokata simu tu, Shani akanipigia

Shani: "Uko wapi we Mtu?"
Analyse: "Nipo gheto tu"
Shani: "Naona umenisusa tokea siku ile. Mimi nishakumiss"
Analyse: "Me nipo"
Shani: "Unaweza kuja kwangu muda huu? "
Analyse: "Poa nakuja"
Shani: "Ndio maana nakupenda, huwekagi vitu rohoni. Haya njoo nakusubiri"

Nikaenda kuoga, ili niende.. ..

Endelea hapa Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee
 
Back
Top Bottom