Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

22nd Portion (Portion Finale)


.... Tuliongea mengi sana usiku ule. Ngoja nikusimulie machache ya alichonisimulia. Alisema hivi;

"Mpaka wewe unakuja kuzaliwa, kiuchumi walau nilikuwa vizuri kwa kiasi fulani. Yale maisha ya kwenda sehemu za mbali kukaa muda mrefu sababu ya utafutaji nilikuwa nishaachana nazo. Mimi kama mzazi, sikutaka kabisa kuwa kama alivyokuwa Babu yenu, sikutaka kuwa mkoloni na kulazimisha mfanye vitu ambavyo havikuwa kwenye maono yenu.

Nilikuwa naamini kama nitawasupport kwenye vitu mnavyotaka, basi kuna uwezekano mkubwa sana wa kupiga hatua nzuri kwenye maisha. Nilikuwa naamini nimepitia njia ngumu za utafutaji sababu ya kumsikiliza Babu yenu. Laiti ningefatisha njia zangu tokea awali basi nisingepitia msoto kama niliopitia.

Ulipoamua kukimbilia Dar es salaam, pale ndio alarm ililia kichwani kwa mara ya kwanza, ila nikaamua kuipuuzia, kwa kuangalia hata Mimi kuna kipindi kwenye maisha nilishapitia hali ile.

Kwa namna zangu ninazozijua Mimi, niliamua kukusupport katika njia uliyochagua. Kukupa Uhuru ndio jambo ninalojutia mpaka sasa. Niliamini utakuwa unajua kitu unachohitaji, na ndio maana niliamua kukusupport.

Nilikuja kushtuka ikiwa too late, kwamba upo kwenye harakati ambazo hata wewe mwenyewe hujui nini hasa unahitaji. Kibaya zaidi, ukajiingiza kwenye mapenzi. Mapenzi na utafutaji ni vitu ambavyo kamwe haviwezi kwenda pamoja, hata ungejaribu vipi. Ndio maana hata baada ya miaka michache ya kupambana kwako, bado ulirudi nyumbani mikono mitupu, kama ulivyoondoka.

Ile hela niliyokupaga kama mtaji, ilisababishwa na majuto niliyokuwa nayo. Sikujua nini nifanye kwa wakati ule, ndio maana nikakupa ile hela walau ukaendeleze ulichokuwa umeanza. Mimi kama Baba nilitakiwa kuwa mwongozo wako katika kila kitu, kitendo cha kukuachia mtoto uongoze, kimetuingiza wote shimoni.

Niliishi muda mrefu nikiwa na hasira na chuki kwa Babu yako, niliamini yeye ndio alivuruga maisha yangu na kuyafanya yawe magumu. Ila ujio wako, ulionesha ni Kwa kiasi gani sikuwa sahihi. Na pia ikawa wazi Babu yako alikuwa sahihi kwenye mengi.

Hakuwa perfect, ila kwa kiasi chake palikuwa na jema katika kila alilokuwa ananifanyia. Mfano mdogo angalia maisha yangu sasa hivi, vitu vingi nilivyofanya na kuhangaikia, sipo navyo. Hata nyie watoto, wote mmetawanyika, kila mmoja yuko anapojua yeye. Hata hizi mali pengine mpo mnazipigia hesabu, na pia sitokuwa na namna zaidi ya kuwarithisha. Nimebaki na kitu kimoja tu, ambacho hakuna anayefikiria kukichukua toka kwangu, nacho ni Mama yenu. Nimebaki na Mama yenu tu hapa. Cha kustaajabisha ni kwamba, Mama yenu nilichaguliwa na Babu yenu, ambae siku zote niliishi nikimlaumu. Sijui kama unanielewa?.

Nikatikisa kichwa tu kukubali.

Akaendelea:

"Siku niliyokutana na wewe ukiwa kama kibarua kule kwenye tangawizi, ndio siku niliyotambua ni Kwa kiasi gani nilimkosea Babu yenu. Maumivu niliyoyahisi moyoni mwangu,siwezi kuyaelezea. Na ndio yalinipa picha, ni kiasi gani nilimuumiza Babu yenu. Hakuna maumivu makubwa, kama pale unapochukiwa na mtu ambae upo tayari kufanya lolote kwa ajili yake.

Nasikitika jaribio la mfumo wa maisha niliokuwa nautamani, limefeli, kibaya zaidi limefeli katika hatua ambayo hatuwezi kurekebisha. Sasa ndio naamini, unaweza ukampenda sana mtu, ila katika namna ya kumuonesha upendo wako ukajikuta unaharibu. Na ubaya ni kwamba jamii haiangaliagi nia, inaangalia matokeo. Watahukumu kulingana na matokeo ya ulichofanya, hata kama nia yako ilikuwa njema.

Mpaka kufikia ile siku tunakutana kule, japo ukaribu na Babu yako ulikuwa umerudi, ila nilijihisi mkosefu upya. Ukaribu uliokuwa umerudi, ilikuwa ni ile naturally tu kama watu wazima tuliamua kusahau yaliyopita. Ila kwa jinsi nilivyojisikia siku ile nilipokuona, nilitambua kuwa natakiwa kumuomba msamaha Mzee wangu, namshukuru Mungu kwa kunipatia ile nafasi, sijui kama Babu yenu angekuwa ameshafariki ningejisikiaje. Hakuna mzazi anayependa kumuona mtoto wake akiteseka"

Kufikia hapa, Mshua akanyamaza kidogo. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, nilishuhudia Baba yangu akitokwa na machozi. Tulikuwa tumeangaliana, akainama chini, na Mimi nikaangalia pembeni. Hata kwenye misiba ambayo nilishawahi kuhudhuria na yeye akiwepo, sikuwahi kumuona akilia. Ila usiku ule Baba alilia mbele yangu.

Siwezi elezea nilijisikia vipi, ila itoshe kusema I felt so bad. Akaniambia "Kuwa strong haimaanishi hatuumii, ila pia chozi kutoka sio symbol ya udhaifu. Tuna wengi tunaowaangalia, ila ni wachache wanaotuangalia na kuyaelewa yale tunayoyabeba, hata kama hatujawaambia"

Baada ya ukiwa wa dakika kadhaa. Nikauvunja ule ukimya

Analyse: "Nadhani hata Mimi natakiwa kukuomba msamaha Mzee. Maamuzi yangu mengi ndio yametufikisha hapa Mimi na wewe"

Mshua: "Sio Kweli. Maamuzi yangu Mimi mengi ndio yametufikisha hapa. Mimi ndio niliamua uje duniani, Mimi ndio nilitakiwa kuendelea kukusimamia mpaka pale utakapokuwa kuwa tayari kuanzisha maisha yako. Sikutakiwa kukusikiliza, hakuna ubishi juu ya ilo. Niliteleza, na nimegundua nikiwa nimeshachelewa sana, sema wewe bado hujachelewa. Una nafasi kubwa ya kuweka mambo vizuri. Hasa yale yaliyonishinda Mimi."

Akaendelea;

"Unajua unapokuwa mtoto, unakuwa sharp katika vitu vingi sana, kasoro vision tu. Upeo na maono yanakuwa wazi kulingana na umri unavyoongezeka Kadiri unavyokua, ndivyo unavyong'amua makosa uliyokuwa ukiyafanya katika umri uliopita. Usikubali maono ya siku chache mbele, watakayokuwa nayo vijana wako, yaharibu mipango yako juu yao ya miaka mingi mbele. Ndio maana jukumu la mzazi ni kumsimamia na kumuongoza mtoto mpaka akue. Niliweza kukusimamia, ila nikashindwa kukuongoza"

Analyse: "Sawa nimekuelewa Mzee. Naamini kila kitu kitakaa sawa siku moja"

Mshua: "Sawa. Vipi huko mjini, mambo yako yanaendaje?"

Analyse: "Mambo ni magumu sana Mzee, kila siku napiga hatua moja mbele, mbili nyuma"

Mshua: "Na hivyo ndivyo maisha yalivyo siku zote, ugumu wa maisha upo ili kutukumbusha namna ya kuishi na watu au kuwa na shukrani pale tunapofanikiwa. Yakiwa mepesi sana tungejisahau"

Analyse: "Ni kweli, lakini, hao watu tunaotakiwa kuishi nao vizuri, mbona hawanijali kabisa?"

Mshua: "Hawakujali kivipi?"

Analyse: "Hata yule unayeona anaweza kukusaidia, nae hakupi kabisa ushiriakiano"

Mshua: "Bwana mdogo, siku zote nakwambia hakuna aliyezaliwa kwa ajili ya matatizo yako. Mtangulize Mungu siku zote. Hata yule unayeona anatakiwa akusaidie, na yeye kuna sehemu anahitaji kusaidiwa. Usipolielewa ilo, utamchukia kila mtu"

Akaendelea, "Hivi huwa unasali?".

Kwa macho makavu kabisa, nikamjibu "Ndio"

Akacheka, "Tabia ya mwanadamu huwa haijifichi, tokea umekuja hapa, hakuna siku ambayo hukukumbushwa na Mama yako kwenda kanisani. Unajiweka mbali sana na Mungu, hivi hizi Baraka anazokuombea Mama yako kila siku zitakufikia vipi?".

Nikabaki kimya. Akaendelea na punch zake;

"Jitihada bila Nuru, utazidi kupotea. Jiweke karibu na Mungu, kisha fanya mambo yako, ongea na watu, wapigie simu, omba kuonana nao hata kama hawataki, maana kwenye haya maisha tunawahitaji hata wale ambao hawatuhitaji"

Analyse: "Nimefanya hivyo sana Mzee, lakini hata wale waliokuwa rafiki zangu, hawapo tena karibu na Mimi kama zamani. Maisha yao yanaenda ila yangu yapo vile vile"

Mshua: "Ukisema hivyo unakosea sana, alafu utaonekana kama ni mbinafsi. Vipaumbele vinabadilika kadiri umri unavyosogea. Kama kuna watu ulikuwa unashinda nao siku nzima mkiongea na kufurahi, usitarajie wakishaoa/kuolewa au kuwa na watoto/familia, wataendelea kukupa uzito kama ilivyokuwa zamani."

"Hao unaowasema, jaribu siku kuwapigia simu alafu uone kama kuna atakayekukatia, mtaongea vizuri tu, na hata wasipopokea, waelewe. Hawajakutenga, ila kawaida umri unaambatana na majukumu. Ukilielewa ilo, hutoumia juu ya ukimya wao"

"Maisha yetu hayana tofauti na safari, mliopo kwenye safari moja ndio mtakutana ndani ya bus. Kuna bus la elimu, bus la kazi, bus la semina nk. Na kwenye hayo mabus, kila mmoja atashukia sehemu yake. Ikitokea mtu ameshuka, mtakie kila la kheri huko aendako maana safari yenu ya pamoja inaishia hapo. Ila ukitaka aendelee kuwepo, utajikuta unashukia njiani au unamlazimisha apitilize vituo. Huko mbeleni lazima hamtoelewana, kuna mmoja kati yenu hiyo safari ya kulazimishana itamchosha, maana utajaribu kumuonesha uzuri wa mandhari nje ya dirisha, ataangalia lakini mawazo yake yatakuwa kwingine, mwishowe atashuka. Sasa kwanini usingeacha ashuke wakati ule?"

"Mliyenae safari moja, hawezi kushukia njiani. Na atakayeshukia njiani huyo hampo safari moja."

"Unakumbuka kipindi mnakua jinsi wewe na ndugu zako mlivyokuwa na furaha hapa nyumbani?"

Analyse: "Ndio?"

Mshua: "Mbona siku ya harusi ya dada yako ulikuwa unacheza mziki kwa furaha sana, ingali ukijua sherehe ikiisha hatokuwa hapa tena?"

Analyse: (Kimya).

Mshua: "Kuna muda unatakiwa ufurahi pindi uwapendao wakiwa wanaondoka"

Akakaa kimya kidogo kisha akaniuliza: "Hivi ishawahi kutokea umekutana na mtu katika jambo fulani, mkapoteana, baada ya muda mkaja kukutana tena sehemu nyingine?"

Analyse: "Ndio, ishawahi kutokea Kwa watu niliosoma nao"

Mshua: "Nadhani walau utakuwa umenielewa sasa, mnaweza mkawa ndani ya bus moja, ila safari zenu ni tafauti. Uliyekutana nae shuleni, usilazimishe aendelee kubakia kwenye maisha yako, wakati kusoma mmeshamaliza."

Akaendelea; "Kwahiyo unapokuwa huko mjini, basi jitahidi sana unapokuwa kwenye mihangaiko yako. Japo unahitaji watu, lakini pia uwe selective kwa kiasi fulani. Pia usijiweke mbali sana na Mungu, kuna wakati anatushindia magumu mengi pasipo sisi kujua, jitahidi usifanye mambo yasiyompendeza".

Analyse: "Sawa Mzee, me nimekuelewa, nitajitahidi kubadilisha baadhi ya vitu na mitazamo yangu pia"

Mshua: "Itakuwa ni jambo la kheri, maana usipokuwa makini utashangaa miaka inaenda ila mambo yako yamesimama."

Analyse: "Ila Mzee, umeniambia nina wahitaji hata wale wasionihitaji. Ila hapo hapo unaniambia sitakiwi kulazimisha watu wabaki kwenye maisha yangu"

Akasikitika kidogo kisha akaniambia, "Kuna tofauti kubwa kati ya sehemu ya kujiegesha, na sehemu ya kuegemea. Usichanganye hizo sehemu mbili".

Nikabaki kimya tu namsikiliza huku najaribu kuabsorb maneno yake.

Tukaendelea kuongea mambo kadha wa kadha, lengo ikiwa ni kucatch up with our past. Mwisho wa siku nikamuuliza:

Analyse: "Ulisema nikirudi bila mwanamke, utaniozesha binti yeyote wa hapa kijijini, vipi kuna yeyote uliyenichagulia?"

Mshua (akatabasamu kidogo): "Siwezi kukuchagulia mke"

Analyse: "Kwann? Huoni utakuwa unaenda kinyume na alivyofanya Babu?"

Mshua: "Babu yako alijua naweza kurudi na mzungu, ndio maana akafosi kunitafutia mke. Ila wewe leta yeyote tu, sisi fresh" (Alafu akageuka nyuma kuangalia kama Mama yupo karibu)

Nikajikuta nacheka. Alaf akaniuliza

"Au unawaogopa wanawake huko mjini? Ukihitaji msaada wewe niambie"

Analyse: "Hao wote ambao niliokuwaga nao nimewapata vipi?

Mshua: "Siwezi jua, labda unatanguliza hela je?. Alafu zikiisha wanakuacha, unarudi huku kupumzika, tunajua unastress za maisha kumbe wanawake"

Wote tukaishia kucheka tu.

Mama akawa amekuja mpaka mlangoni, alafu akatuuliza "Mnahitaji chai?". Baba akajibu "Ndio"

Mama: "Analyse, njoo uchukue vikombe na chupa"

Mshua: "Siwezi kuandaliwa chai na huyu, haitokuwa tamu kama ikiandaliwa na wewe mke wangu"

Mama(akacheka) : "Sawa , basi ngoja niwaletee"

Mshua: "Ngoja tuje huko huko ndani, huku mazungumzo yameshaisha"

Mama: "Sawa"

Analyse: "Yani Mama na umri huo unakubali Baba anakuhadaa na vimaneno vyake?"

Mama: "Uongo wa mganga, ndio nafuu ya mgonjwa mwanangu" (Akacheka kisha akaingia ndani)

Nikafikiria kwa muda kidogo alafu nikamuuliza Mshua; "Kwahiyo chai isipoandaliwa na yeye haiwi tamu kwako?"

Mshua: "Mbona ulichofikiria, ni tofauti na ulichoniuliza?"

Nikastaajabu, anaongelea nini huyu Mzee? Amejuaje kama nilichomuuliza sicho nilichofikiria?. Ila kabla sijafungua mdomo wangu akaniwahi:

"Kuna muda binadamu wote ndivyo tulivyo"

Nikabaki namwangalia tu. Akanyanyuka, akanisogelea kidogo. Alivyofika usawa wangu, akaniambia "Unapokuwa mtoto, unatakiwa kumsikiliza mzazi wako. Unapokuwa mtu mzima, mnatakiwa kusikilizana wewe na mzazi wako, maana upeo wako pia unakuwa angavu na umekomaa. Ila kadiri miaka inavyozidi kusogea, wazazi wanatakiwa wakusikilize wewe mtoto wao, maana akili yao inakuwa tayari imechoka. Uwe umejiandaa au hujajiandaa, kuna siku nitatakiwa kukusikiliza mwanangu"

Akanipiga piga kwenye bega, kisha akaingia ndani.

Niliendelea kubaki pale nje kwa dakika kadhaa, nikifanya marejeo ya mazungumzo yetu. Kuna kitu nikagundua alikiongea kwa uwazi, ila nilichelewa kuking'amua. Kilivyokuwa wazi kwangu, nikajikuta nasikitika kwa tabasamu.

Nikanyanyua vitu na kuelekea ndani, tayari kwa kuanza chapter mpya ya maisha yangu.



*******************************************

Wakuu, kama ilivyo ada ya simulizi zangu. Lengo la hii story ilikuwa ni kuelezea mazungumzo yangu na yule Mzee wa Kongowe, niliamua kujumuisha na matukio yangu mengine walau kuweka uzito. Nashkuru kwa uwepo wenu tokea mwanzo mpaka sasa. Panapo majaaliwa, tukutane tena kwenye simulizi zijazo.

Until Next Time,

Wasalaam,

Analyse
Kuwa strong haimaanishi hatuumii, ila pia chozi kutoka sio symbol ya udhaifu
 




Pitieni hizo
Kali zote mkuu
 
Hii mbona story, inataka kufafana na walimu fulani, ila yeye ni wakiume na mkoa wengine!?
 
Analyse mkuu hii stori nlikuwa naipita juu juu tu, ila leo nimeanza kuisoma nmejikuta sijatoka mpaka namaliza.
Umeongea uhalisia wa maisha nimeng'amua how it feels like to grow up with a father on your side, by my side he left me when im in kindergarten.
I can't picture if he was still in my young age would it be troublesome or awesome?
#RIPDAD
 
Analyse mkuu hii stori nlikuwa naipita juu juu tu, ila leo nimeanza kuisoma nmejikuta sijatoka mpaka namaliza.
Umeongea uhalisia wa maisha nimeng'amua how it feels like to grow up with a father on your side, by my side he left me when im in kindergarten.
I can't picture if he was still in my young age would it be troublesome or awesome?
#RIPDAD
Mkuu, wanasema the right time of anything, ni pale kinapokuwa mbele yako. Nadhani huu ndio ulikuwa muda sahihi kwako kuisoma. Pia shukran kwa kusonga nayo mpaka mwisho.

Lastly, pole kwa kumpoteza Mshua ukiwa katika umri mdogo. Kila kitu kina sababu yake.

Stay blessed.
 
Mkuu, wanasema the right time of anything, ni pale kinapokuwa mbele yako. Nadhani huu ndio ulikuwa muda sahihi kwako kuisoma. Pia shukran kwa kusonga nayo mpaka mwisho.

Lastly, pole kwa kumpoteza Mshua ukiwa katika umri mdogo. Kila kitu kina sababu yake.

Stay blessed.
Bless
 
Hizi story za kutunga ambazo huwa mnalazimisha kusema ni kweli ukifikia hatua flani zinakuwa ngumu sana kuendeleza. Hapo mtunzi huanza kukimbia kimbia na kutoa udhuru. Unamwona kabisa yumo humu anasoma tu comments ila anakuambia hivi na vile. Yaani ili mradi tu.
 
Back
Top Bottom