Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Uchumi wa Zambia ni mdogo sana kulinganisha NA Tanzania ila wazambia wengi wao ni waaminifu sana.
Ya Zambia mtu anaweza kununua kitu cha kwacha elfu 10 akakupa 5, afu akakwambia 5 atakumalizia week ijayo. Na kweli ukienda week ijayo mnamalizana. Bongo nilikuwa naleta lap top, sim, plasma tv nk, tena katika ofisi zinazoaminika kuwa ni za watu wenye pesa. Lkn akikupa hela nusu na kukwambia uje week ijayo, basi week ijayo ukifika humkuti au huwakuti unaowadai wote. Bora mtu ajifiche chooni masaa matatu, lkn ahakikishe nimeondoka bila kunilipa 😂😂😂
 
Mpumbavu ushaanza upumbavu!

Badilika

#Usipobadilikatutakubadilisha
Shukran mkuu, bora umenisaidia kumuelimisha jamaa. Watu wa aina hii huwa wanafurahi pale mtu anapoleta uzi unaozungumzia kina Zali, Wema Sepetu, Diamond, Kiba nk. Ila hizi thread zenye uhalisia wa maisha hawazipendi kwa sababu hazina mipasho ile waliyoizoea kule kwa kina Diamond na Kiba.
 
Umeongea ukweli mtupu mkuu,sisi wazee wa road trips ndani ya barabara za Zambia 🇿🇲 unaweka kambi popote na kama unawasiwasi zaidi unalala kwenye check points za police au jeshi!
 
Usalama unaanzia udogoni kwani watoto wanashuhudia wazazi na jamaa wanavyofanya biashara na kuaminiana nao wanakua na kuiga

Sisi ni tofauti kabisa mtoto anakuwa kwa kushuhudia utapeli au nyumbani mtu anagonga kuja kudai utasikia mtoto anaambiwa mwambie baba hayupo

Wizi ni janga la Taifa letu na hakuna wa kumuamini na utakaesema huyu kalia sana Acha nimkope ndio kabisa hiyo imekula kwako

Lingine ni kuwa kuna wengi wanatetea wizi yaani mfanyakazi au kiongozi serikalini au sekta binafsi anaiba na akibainika utasikia- Safi sana wacha waibe hata mimi nisingeacha

Hapo tegemea hakuna mwenye unafuu na wizi hautaisha hata serikalini


Hili la kuweka hela za kubadilisha hadharani zipo sehemu kadhaa hata kuna mji Somaliland panaitwa Hargeisa ipo kwenye YouTube
Yaani kina mama wanauza Dhahabu hadharani huku vijana wakibadilisha hela zikiwa juu ya meza kibao na hakuna wa kuiba
Tena anaenda kusali anafunika na shuka [emoji3064]
Utashangaa ya Zambia ila kuna wengine waaminifu pia
 
Uko sahihi Somalia ndio kiboko

Mtu anaenda msikitini kaacha maburungutu ya hela wazi njiani anapobadilishia na haibi mtu

Nchi Haina amani vurugu tupu lakini uaminifu wa pesa uko juu mno kuliko Sisi watanzania tuliojaa amani
 
Ni kweli kabsa yan uko sheria zao kali na wanazifatilia sana ndio maana wananchi wao wanatii sheria bila shuruti!! Lakin waho wazambia braza wako na roho mbaya sana kuna visa wanatufanyia sana sisi wapita njia mi nimeishi hapo MPIKA
 
Uko sahihi Somalia ndio kiboko

Mtu anaenda msikitini kaacha maburungutu ya hela wazi njiani anapobadilishia na haibi mtu

Nchi Haina amani vurugu tupu lakini uaminifu wa pesa uko juu mno kuliko Sisi watanzania tuliojaa amani

Yaani unaweza kuacha mzigo kwa msomali hata baada ya mwaka ukaukuta
Wizi hakuna utakula shaba hadharani
 
Uko sahihi Somalia ndio kiboko

Mtu anaenda msikitini kaacha maburungutu ya hela wazi njiani anapobadilishia na haibi mtu

Nchi Haina amani vurugu tupu lakini uaminifu wa pesa uko juu mno kuliko Sisi watanzania tuliojaa amani
Nimekumbuka kitu kutokana na mchango huu!!

Ndugu zetu Waislam asilimia kubwa hujitahidi kuyaishi wanayofundishwa tofauti ki % na upande mwingine.(naomba nisishambuliwe ni mtazamo wangu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…