Sijawahi kuona vita nyepesi kama hii kwa wananchi

Ndio maana unaitwa Mr. DUDUMIZI, mbona unaandika bila kufikiri sikatai uwekezaji ila kuna makosa kwenye mkataba, embu fungua sehemu ya sahihi niambie majina ya mashuhuda waliokuwepo wakati wa kusaini huo mkataba. Alafu fungua sehemu ya sahihi ya watu wa Dubai, niambie mtu aliyesaini aliteuliwa na nani.
 
Lakini mbona mwamakula hajasema hivyo, ye amefichua kabisa kilichopo nyuma
 
uzeni za zbar , Ila za watanganyika hapana !!
 
A thorny problem for CCM to solve.
 
Halafu hawazidi hata elf 10,yaani nimechekaaaaaa kwa sautiiiii

Watu wana akili bwashee, wakenya na warundi wajue watz wameamka sasa
 
Wewe hujausoma mkataba wa bandari?
 
Wewe hujausoma mkataba wa bandari?
Wewe ambae umeusoma uweke hapa utuoneshe kasoro zake. Wambie wachumia tumbo wenu wasituchukulie watanzania wa leo poa, kama walivyowachukulia nyinyi poa miaka hiyo kwenye swala la Lowasa.

Ile haitatokea. Never and Never again.
 
Watanzania originally wameinuka sasa, kile kimbaumbau na shemegie na kikundi chao walidhani watu bado wamelala?
Ni zamu yao sasa kuonja mateso waliyowapa watanzani miaka dahari
Wakati wao wakila mboga ya millioni kumi wenzao waliishia makande, sasa ni either wale makande au warudi zao rwanda huko, wanyonyaji kabisa kupitia mgongo wa dini
Mama twende kazi pamoja sanaaaaa
 
Inashangaza watu waliodanganya watanzania milioni 60 kuwa Lowasa ni fisadi bado wana uwezo wa kudanganya tena kuhusu mkataba wa bandari na nyinyi mnakubali kudanganywa kizembe zembe kama hamkuwahi kwenda shule.

Unanambia mimi naandika bila kufikiri, lakini ajabu ni kwamba wewe unaejiona unafikiri umeshindwa kuwambia hao wanaopinga watuwekee mkataba hadharani na kutuonesha makosa yaliopo katika mkataba tuyaone na ku judge kupitia macho yetu wenyewe.

Haiwezekani adui yako au jirani yako aanze kutangaza kuwa mtoto wako ni mwizi, alafu wewe uchukue fimbo na kuanza kumpiga mwanao bila ushahidi wa kile alichoiba.

Mtu mwenye akili unatakiwa ujiulize je kama kweli ameiba mbona haukuoneshwa kile alichoiba, au mahali alipoibia. Je kama adui au jirani yako ameamua kuichafua tu familia yako mtaani kwenu kwa kupitia mtoto wako?

Narudia tena, weka mkataba hapa unioneshe sehemu ambazo hazifai nizione kwa macho, sio ulete porojo kama zile za enzi ya Lowasa.
 
kwahiyo unataka kusema lowasa hakuwa fisadi? unamjua lowasa lakini au unamsikia.
 
kwahiyo unataka kusema lowasa hakuwa fisadi? unamjua lowasa lakini au unamsikia.
Kwahiyo mwaka 2015 wapinzani mkiongozwa na Mbowe, Lisu nk mlitaka watanzania na akili zetu tumchague Lowasa ili nchi yetu iongozwe na raisi fisadi au sio?

Afu bado kuna watu wana amini kuwa wapinzani hao ni wazalendo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…