Sijivunii wazazi wangu

Umefika fomu foo bado unataka wakubebe wawe wanatembea na wewe huko mjini.

Pambaneni huko na msisahau kuleta pesa kwa wazazi.
Wala hawastahili kuletewa hata senti moja au hata sumniii!!!![emoji23][emoji23]

Inatakiwa wavune walicho panda.let them reap what they sow....[emoji1]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 

MTU akifanya upumbavu unataka aitwe Mwenye hekima?
Hizi dini zimefundisha Watu unafiki WA kiwango kikubwa Sana.

Yaani Mimi Kwa vile ni Baba nikifanya upumbavu unataka Watoto wangu wanione ninahekima?
Watoto wangu sitawafundisha unafiki.
Baba Yao nikizingua wajue nimezingua, na wewe na uwezo wa kuniambia Mzee hapo umepuyanga. Nami niombe Radhi ikiwa kweli nimekosea.

Sio hizo hadithi za kijinga jinga, zakinafiki, zakizamani, zakitumwa, zakufanya Watu miungu Watu.
 
Wenye wazazi wenye connection na hawajasaidiwa unawaambia nini..?
Haikuwa lazima wao kusaidiwa na wazazi wao...

Hapa mada imejikita kwenye malezi ya mtoto angali bado haja anza kujitegemea from 0-18 years hapa lazima mzazi awajibike ipasavyo ila sio akwepe majukumu yake kwenye hichi kipindi..

Baada ya 18 years sasa hapo mtoto hana cha kuwalaumu wazazi..ila kama hawakuwajibika kumlea hadi anafika 18 years mtoto anastahili kuwasema wazazi wake....

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Kwani usipowapa pesa zako watakufa?

Ujue na wanao watakuja kukufanya hivyo hivyo.
Na wao wala sihitaji baraka zao ili nifanikiwe maana walikuwa wazembe kwenye kulea na kutimiza majukumu yao kama wazazi...

Point ni kwamba wazazi wazembe wasitumie kigezo cha "uzazi" kama defence mechanism ya kujilinda na kuficha Uzembe wao....

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 

Pole kwa magumu unayopitia. Ila inatakiwa ujue kuwa wazazi ni binadamu tu waliotangulia kuishi kabla yako, na wakakuzaa.

Hawana kingine cha ziada zaidi ya hicho.

Sasa na wewe umeshaishi-ishi duniani kwa hiyo umeshajionea kuwa kuishi kwingi sio lazima kuambatane na kufanikiwa kwingi. Umeshajionea wazee wengi maskini. Umeshajionea wala bata wa kutosha. N.k.

Wazazi ni binadamu wa kawaida tu ambao nao wanapambana na maisha. Kitendo cha wao kukuzaa wewe usidhani kwamba wao ni watu special sana tofauti na binadamu wengine. Mapambano yao inaelekea hayakufanikiwa sana ndo maana wapo kama walivyo.

Kuzaa ni kitu rahisi sana.

Mtu yeyote yule anaweza akatia mimba, na kubeba mimba. Mimba ni zao la starehe. Mimba haihitaji akili yoyote au jitihada yoyote. Inakuja tu kama magugu baada ya mvua. Kama ni kazi, basi kuzuia mimba ni kazi ngumu kuliko kubeba mimba. Angalau kuzuia mimba kunahitaji matumizi ya akili. Kunahitaji ukumbuke siku za hatari na kuchukua hatua mahsusi za kuepuka kukutana kimwili katika siku hizo.

Masuala ya Kuchezewa (Kurogwa) Achana Nayo Kabisa!

Angalia maisha ya watu wengi. Maskini ni wengi kuliko matajiri. Umaskini ni jambo la kawaida. Utajiri ndo jambo la kitofauti. Kwa hiyo kuanza kufikiria kuwa umerogwa ni akili ndogo hiyo. Inawezekana labda na wazazi wako waliishi kwa imani hizo za ushirikina ndo maana wameishia hapo walipoishia.

Ukiruhusu tu kuhusianisha changamoto zako za kimaisha na masuala ya kurogwa basi utayumba sana, na utatapeliwa sana na wajasiriamali wa imani kama vile akina Mwamposa na waganga wa kienyeji.

Jifunze kutumia akili. Mfano akili yako imekutuma kuwa kumiliki kiwanja ni jambo zuri, basi fanyia kazi hilo. Weka lengo la kumiliki kiwanja na uanze kudunduliza kununua hicho kiwanja popote pale kinakopatikana. Katika harakati ndo utafungua fursa zaidi za kufanikiwa. Hauhitaji kwenda mganga wala kununua mafuta ya upako ili kufanikisha malengo yako. Kuwa mkali tu na malengo yako. Kama hela unayoingiza ni ndogo, acha kabisa habari ya kuwatumia wazazi wako mpaka utakapofanikisha lengo lako la kumiliki ardhi. Wazazi wakikupigia kelele waambie unadunduliza kwa ajili ya kufanikisha malengo yako ya kiuchumi.

Usiruhusu kabisa imani za uchawi kichwani mwako, hata kama watu wangapi watakwambia nini. Maana watanzania kwa kuropoka tu hawajambo, lakini mwambie akupe ushahidi sasa.... utasikia tu "We kama huamini shauri yako, ila uchawi upo!"
 
Kuna watu wengi tumeshindwa kuelewa kuwa psychologically kuzungumza ni njia ya kupata relief, Kuna weng wamefanya action mbaya zaidi hata kuua au kujiua kwa kushindwa tu kuyaongelea yale yanayowasibu.
 
Mzazi wako ni mjinga ?
Mtu kuwa mzazi haifanyi ujinga wake kuisha Akilini na wala sio kigezo cha kuficha Uzembe wake

Kama mzazi ni mjinga ni mjinga tu.
haibadilishi uhalisia wa ujinga wake.

Unataka kutumia kigezo cha 'Uzazi" kama defence mechanism ya kutetea uzembe wa wazazi?




Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ushauri makini kabisa huu...Umetema madini yote mkuu....[emoji817][emoji817][emoji817][emoji404]

Sio hawa wengine wanataka kutumia "uzazi" kama defence mechanism ya kuwatetea wazazi wajinga na wazembe...

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Pole sana Kwa kupitia hayo kwa kukosa maarifa ya wajibu wako kama mtoto kwa wazazi, endelea kuwapenda kama unavyowapenda ila Sasa tambua wajibu wako kama mtoto Ili uwe na amani ya moyo, wajibu wa mtoto kwa mzazi ni kumuheshimu na siyo kutunza mzazi wewe ulichokosea nikuanza kutunza wazazi wako ukiwa Bado mdogo, kulingana na jinsi ulivyoeleza baba na mama yako wanaishi tofauti pia bado hukupaswa kubeba majukumu ya kuwatunza maana jukumu la kutunza mke na watoto ni la baba Sasa baba yako alipaswa kujitunza yeye, mke wake na wewe mtoto na mama yako kama alihitaji matunzo basi alitakiwa kumuomba baba yako na siyo wewe.

Kwa vile umeshajitambua anza upya kutengeneza maisha yako na uchumi wako Ili uwe baba bora utakapo anzisha familia yako, Sasa basi watu wanaotakiwa kulelewa niwazee maana nguvu zao zimekwisha hawawezi kufanya kazi ndipo hapo wazee wenye watoto wao hulelewa na watoto ndo maana unaona Kila dini na serikali inasisitiza na kulazamisha baba atunze watoto wake kwa kuwajibika kuwaandalia maisha ya baadaye Ili waje wamsaidie uzeeni, hapo utaona matunzo ya mama yapo kwa mumewe na siyo mtoto ila baba akifariki mama anatakiwa kutunzwa na jamii kama mjane na watoto watatuzwa pia na serikali pamoja na jamii kama wajane ila baba hata akifiwa na mke bado anawajibu wa kufanya kazi Ili atunze familia mpaka uzee utapomfika ndo watoto wanachukua jukumu la kumlea, hivyo basi Fanya jukumu lako la kuwaheshimu wazazi na hayo yakuwapa vipato achana nayo mpaka muda wako wa kuwahudumia ufike.
 
Fact...[emoji817][emoji817][emoji817][emoji404]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
NAWASHUKURU WOTE MNAOTOA MAONI YENU, KUNISHAURI, KUNIPA MOYO NA HATA WALE MNAOKOSOA PIA MAANA NAAMINI PIA HAKUNA MWENYE MAONI YENYE NIA MBAYA KWANGU KWANI YOTE YANA MATOKEO MAZURI KWA KUWA SIJAONA COMMENT YENYE LENGO BAYA HATA MOJA.... NAWASHUKURU SANA KWA MUDA WENU
 
Kaa utambue,
anayemsaidia mtu yeyete katika maisha , ni Mungu, mimi ninaendika hapa bila mzazi wangu alifungwa nikiwa darasa la 4. Alikuwa mfanyakazi na bosi kiaina. maisha yalibadilika kutoka kuchagua chakula hadi kukosa hata chakula kibaya cha kutosha.
lakini leo nachagua chakula tena. ni Mungu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…