Sijui ni wangapi nimewaambukiza mpaka sasa. Wengi ni waume za watu

Sijui ni wangapi nimewaambukiza mpaka sasa. Wengi ni waume za watu

Ujumbe mzuri bila kujali uhalisia wa hadithi hii.

Ugonjwa huu upo sana mtaani na hivi siku hizi watu wanavyotumia madawa ya kufubaza virusi basi ni tabu tupu kumjua mwenye umeme hasa kwa wale wazee wa kupima kwa macho.
 
Haya mambo yanatokea sana na mimi ni shuhuda kwa kisa kimoja kama Hilo.

Ila yule hakubakwa, bali aliambukizwa na mpenzi wake.
Alipokuja kujua kaathirika akaanza revenge kwa kila mwanaume aliemtongoza.

Kwa hiki kisa kwa kweli wanawake wote linapokuja suala la Mme huwa wanatetea kwa nguvu zote waume zao.

Hata kama kutakuwa na ugomvi kati yao wanandoa lakini bado mke atakuwa upande wa Mme tu.

Ila wanawake sijui kwanini hawaamini watoto wakiwashitakia kuwa waume zao wamewatongoza au hata kuwabaka?

Hii sio chai kwani mambo haya yapo sana

Mleta mada anaweza kuwa kaipata mahali na kuja ku share na sisi, ila yanatokea sana
 
Mimi ni mwanafunzi wa chuo, binti mwenye sura ya kawaida lakini anayejua kuitumia. Natabasamu na kuongea kwa upole, lakini ndani yangu nimebeba maumivu makali sana. Na leo, nimeamua kusema ukweli wangu, kwa sababu nimechoka kubeba mzigo huu peke yangu.

Nilipoingia darasa la sita, familia iliniamini sana. Nilikuwa nakaa kwa dada yangu mkubwa, alinihudumia kama mama. Shemeji yangu, mume wa dada yangu, alikuwa kama baba kwangu. Lakini usiku mmoja uliharibu kila kitu, alinibaka. Nilijichukia sana.

Dada yangu hakutaka kusikia haya mambo, alisema namkosea heshima mume wake. Nilikuwa nalia kila usiku. Hakuna aliyeniona, hakuna aliyeniuliza, "Uko sawa?"

Miaka ikaenda, niliendelea kusoma, lakini nikawa siyo yule yule tena. Nilianza kuwa na hasira na wanaume, nikawa siamini mtu yeyote. Nilijifundisha kuficha chuki yangu ndani ya tabasamu, na nikaanza mpango wangu wa kulipa kisasi. Bila kujua, nilikuwa nimeambukizwa virusi vya UKIMWI na shemeji yangu.

Nilipofika chuoni, nikageuka kuwa mtu mwingine. Nikawa natafuta wanaume, hasa waliooa. Nilikuwa nawafanya wanione kama mwanamke wa ndoto zao. Nikawaambia maneno wanayotaka kusikia, nikawapa mapenzi ya kuwakoleza, na baada ya hapo, nilihakikisha wanakuwa sehemu ya kisasi changu.

Sijui ni wangapi nimewaambukiza mpaka sasa. Wengi wao ni waume za watu, viongozi wa makanisa, walimu, wafanyabiashara, na sijawahi kuwaambia ukweli. Niliamini kama mimi niliumizwa bila huruma, basi nitafanya dunia yote ilie pamoja nami.

Lakini leo… leo nimechoka kuvaa tabasamu la kishetani huku nikiungua kwa ndani. Najua ninachokifanya si sahihi, lakini je, ni nani aliyenisaidia kipindi nilipokuwa nalia na unyanyasaji niliofanyiwa?

Siombi huruma yenu, maana ni mfu mtarajiwa. Naomba ushauri tu. Je, naweza kubadilika? Nawezaje kuiponya nafsi yangu yenye uchungu? Nawezaje kurudisha utu wangu uliopotelea kwenye visasi?

■ Kama una jambo linakutatiza, usikae nalo. Linaweza kuharibu hatima ya maisha yako. Tushirikishe, tusaidiane na tushauriane. Nitumie ujumbe WhatsApp: 0716 101690
View attachment 3426643
Huyu demu yuko wapi tufanye partnership nae...mie pia na ukimwi na sijui wangapi nimewaambukiza.
Huyu atafaa tuwe bonny and clyde
 
Back
Top Bottom