Sikio la Kufa halisikii dawa - Wakataa ndoa wote

Sikio la Kufa halisikii dawa - Wakataa ndoa wote

majoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
2,595
Reaction score
4,775
Wakati unashawishika na watu waliovuta bangi zao, waliojikatia tamaa ya kuishi, wasiotaka ndoa kwa kuwa wao si wanaume wala si wanawake... hawajielewi, waliotingishika akili baada ya kutendwa kwenye mapenzi; waliolelewa nje ya famili na wakachukia familia; kaa chini utafakari. Hapa si quote mstari wowote wa vitabu vitakatifu, hapa nakupa makali live.

Jaribu kufikiria, ulilelewa na familia na sasa unajitegemea. Kwa nini uishi peke yako? Wakati ukiwa na familia yako ndio waliokuwa wakipa huduma zote ulizohitaji wakati wa furaha na wakati wa magumu sasa iweje leo uwe mwenyewe? Huo ubinafsi wa kuishi peke yako unautoa wapi? kwa nini usioe? kwa nini nawe usisimame kama baba ukiienjoy na mke na watoto wako?

Hivi kesho ukihitaji huduma za kuhospitali nani atakuogesha? nani atakufariji? Najua una ndugu zako, nao watakuwa bize na familia zao; utashirikiana nao katika mambo ya nje na si ya ndani. Hivi usiku unajikumbatia peke yako kama mchawi na hata wachawi wanaoa! Hata kama utanunua wanawake... utachoka... hutapata amani na faraja ambayo ungeipata kwa mke. Kwani nini uishi kiunyongee?

Jaribu kuangalia walioishi peke yao..... hakuna aliyekuwa na furaha ya dhati, waliishia kuwa walevi na wanunua papuchi mwisho walifia ndani na kukutwa wamepasuka. Ndoa ni muhimu kwa binadamu. Changamoto za ndoa zinaweza kuwa solved lakini ukiwa na upweke si vya kukimbilia. Najua kuna wanaojifariji eti nitazalisha huko nje na kuchukuwa watoto wangu.

AMKA jipange kutafuta familia uitunze ikutunze. Hao wanaokudanganya humu hutakuwa nao na utakufa kibudu.

Ndo nshasema.. wakataa ndoa wote hawajielewi... wakajicheki afya ya akili na kama ukitaka kuwaiga usithubutu.

Mapovu ruksa.... ndoa zidumu na zitadumu milele na milele.
 
Yaani unasema mapovu. While povu unalitoa ww linapenya hadi katikati ya meno.
Kwanza kumbe hujaelewa kataa ndoa ni nini, the big slogan humu. Hujui amendments zake hufahamu how it works. Kaa kimya sio lazma kila kitu uandike chunguza what is kataa ndoa.
#kataandoa
#Ndoaniutapeli
 
Kataa ndoa haina mahusiano na kuzaa.

Adam na Eva walituzaa nje ya Ndoa, hawakutaka Stress..

Ronaldo CR7 Ana Familia ila hana ndoa.

Ogopa sana mkataba wa kutenganishwa na KIFO...
Inawezekana hujui ndoa ni nini? Adamu na Eva walikuwa ndani ya ndoa. Kumbe kinachokuogopesha ni Mkataba wa kutenganishwa na kifo? 😀
 
Yaani unasema mapovu. While povu unalitoa ww linapenya hadi katikati ya meno.
Kwanza kumbe hujaelewa kataa ndoa ni nini, the big slogan humu. Hujui amendments zake hufahamu how it works. Kaa kimya sio lazma kila kitu uandike chunguza what is kataa ndoa.
#kataandoa
#Ndoaniutapeli
Nilijua mtakuja kwa kasi ya SGR..... Ndoa zitadumu na zitaishi milele
 
KATAA NDOA MKATABA WA KITAPELI
KATAA NDOA LINDA MAISHA YAKO
KATAA NDOA LINDA UCHUMI WAKO
KATAA NDOA LINDA UHURU WAKO
Mkataba wa kuishi pamoja kwa uaminifu
Maisha yako yanakuwa salama zaidi
Uchumi wako utakua na kuongezeka
Uhuru wako utakuwa nao ni kiasi cha kuwekeana mipaka tu.
 
Wakati unashawishika na watu waliovuta bangi zao, waliojikatia tamaa ya kuishi, wasiotaka ndoa kwa kuwa wao si wanaume wala si wanawake... hawajielewi, waliotingishika akili baada ya kutendwa kwenye mapenzi; waliolelewa nje ya famili na wakachukia familia; kaa chini utafakari. Hapa si quote mstari wowote wa vitabu vitakatifu, hapa nakupa makali live.

Jaribu kufikiria, ulilelewa na familia na sasa unajitegemea. Kwa nini uishi peke yako? Wakati ukiwa na familia yako ndio waliokuwa wakipa huduma zote ulizohitaji wakati wa furaha na wakati wa magumu sasa iweje leo uwe mwenyewe? Huo ubinafsi wa kuishi peke yako unautoa wapi? kwa nini usioe? kwa nini nawe usisimame kama baba ukiienjoy na mke na watoto wako? Hivi kesho ukihitaji huduma za kuhospitali nani atakuogesha? nani atakufariji? Najua una ndugu zako, nao watakuwa bize na familia zao; utashirikiana nao katika mambo ya nje na si ya ndani. Hivi usiku unajikumbatia peke yako kama mchawi na hata wachawi wanaoa! Hata kama utanunua wanawake... utachoka... hutapata amani na faraja ambayo ungeipata kwa mke. Kwani nini uishi kiunyongee?

Jaribu kuangalia walioishi peke yao..... hakuna aliyekuwa na furaha ya dhati, waliishia kuwa walevi na wanunua papuchi mwisho walifia ndani na kukutwa wamepasuka. Ndoa ni muhimu kwa binadamu. Changamoto za ndoa zinaweza kuwa solved lakini ukiwa na upweke si vya kukimbilia. Najua kuna wanaojifariji eti nitazalisha huko nje na kuchukuwa watoto wangu... AMKA jipange kutafuta familia uitunze ikutunze. Hao wanaokudanganya humu hutakuwa nao na utakufa kibudu.
Ndo nshasema.. wakataa ndoa wote hawajielewi... wakajicheki afya ya akili na kama ukitaka kuwaiga usithubutu.
Mapovu ruksa.... ndoa zidumu na zitadumu milele na milele.
YANI MWANAUME UMEPAMBANA UMEJIPATA UNAENDA KUPELEKA MALI TENA KWA MWANAMKE -mtume Paulo anasema ni Bora usioe ishi kama padre joh siwashauri vijana kuoa .........Wenda kijana akiwa masikini namana mke wako akiomba talaka mtagawana vijiko Kijana uliyejitambua usioe
 
FB_IMG_17403106841499776.jpg
Vile mwisho wa wakataa ndoa utakavyokua
 
YANI MWANAUME UMEPAMBANA UMEJIPATA UNAENDA KUPELEKA MALI TENA KWA MWANAMKE -mtume Paulo anasema ni Bora usioe ishi kama padre joh siwashauri vijana kuoa .........Wenda kijana akiwa masikini namana mke wako akiomba talaka mtagawana vijiko Kijana uliyejitambua usioe
Kumbe tatizo ni kutoa mahari? Umemgusa Mtume Paulo unayajua maisha yake? alikuwa anaongelea wale ambao hawajajaaliwa kuweza kufanya mambo na hawana tamaa ya kumtamani mwanamke. Lakini kama wewe ni rijali na unatamaa ni vema uoe.
Unaogopa talaka ya kugawana mali..... pambana hilo lisikutokee
 
Back
Top Bottom