Wakuu,
Tujikumbushe kidogo wakati Rais Samia akiwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ufunguzi wa Kampeni kitaifa uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Kawe, alizungumzia Sera zake na mambo atakayotimiza kwa wananchi ndani ya siku 100.
Soma GE2025 - Ahadi za Mgombea Urais CCM, Samia Suluhu Hassan kwa siku 100 za kwanza za uongozi wake miaka mitano ijayo (2026 -2030)
Mojawapo ya mambo hayo ni " Uanzishwaji wa mifumo rafiki ya Uwajibikaji ambapo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Watendaji wengine wa Serikali watatoa taarifa na kujibu maswali kutoka kwa Wananchi kwa njia ya Kidigitali na SMS za bure. Hiki ndicho kitakuwa kipimo cha Mawaziri - Ameulizwa ngapi, amejibu ngapi na kuchukulia hatua ngapi"
Hapa aliongelea uwajibikaji wa Viongozi kutataua changamoto na kusikiliza hoja za wananchi kwa njia ya kidigitali ambapo tangu kuzimwa kwa Mtandao Oktoba 29 na kurejeshwa Novemba wananchi wamekuwa wakitoa malalamiko kwa Serikali kwa njia ya Mitandao na ni hakika viongozi wanaona kama wana spy pia wameshapewa taarifa na bado wamekaa kimya na kuendelea kutoa vitisho kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anavyofanya
Je, mauaji, utekaji, ukamataji na kesi za uhaini kwa vijana vilisahaulika au viliuepo kwenye Orodha ya yale amabyo ungefanya ndani ya siku 100? tunaomba jibu hapa Rais Samia maana ni muda sasa tangu umuapishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali binafsi sijakuona kwenye runinga wala kukusikia ukijibu madai ya asasi na taasisi za kimataifa juu ya mauaji yaliyofanyika wakati wa uchaguzi uliokupa ushindi wa 97.66%