Tetesi: Siku 7 Zijazo Mbunge Mwingine wa Babati kutimkia CCM

Tetesi: Siku 7 Zijazo Mbunge Mwingine wa Babati kutimkia CCM

Status
Not open for further replies.
Chadema itabidi wamwite tena Upendo Peneza kukemea hii tabia ya machadema kujiuza kwa reja reja. Dah.
 
Hii kweli ni fedheha kwa upinzani. Tatizo unaweza kuta hawa wote waliokuwa CCM na sasa wanarudi walikotoka. Yawapasa kufa na wanachama wenu asili, sio hawa wanaokuja kutafuta madaraka. Utakuta mtu alikuwa upande ule akakosa uteuzi kugombea ubunge anakubaliwa kurukia upinzani pasipo kufanyia veting anakubaliwa. Ndio hawa wanatufadhaisha wapiga kura wao. Tunakoenda watu wengi watagoma kushiriki uchaguzi kwa sababu ya kadhia hii. Vya ma vya upinzani vijitafakari kwa kweli, ukichukulia ushindi ulipatikana kwa kumwaga dau.
 
Na hakika hao ndio wangekuwa Mawaziri wa Nchi hii. Kabla ya kununuliwa wangekuwa wameishauza raia wote wa nchi hii, wangekuwa wameuza mbuga zetu, wangekuwa wameishauza Maliasili zote za nchi.
Zawadi yako ya Noeli: kima.
 
Sipati picha kama hiki chama kingepewa nchi,halafu kati ya wabunge wanaodai kununuliwa mmoja angekuwa waziri wa ulinzi,mwingnne waziri wa mambo ya ndani,sijui Tanzania ingekuwa wapi kwa mfano.
inavyoonekana kuna vyama haviandai wanachama wao kuwa viongozi,na wanapopata uongozi bado hawbndaliwa kuwa viongozi.

Mimi sipati picha pale chama kikongwe, kikuu, kinapowanunua wabunge wa upinzani ili kuufifisha upinzani kama sio kuua. Hizo hela za marudio ya uchaguzi tungelifanya nazo kitu kwenye huo huo mkoa na huku tukijua kuwa tuna coverage ya Press tukajionesha tunapofanya hayo mema, unataka kutuambia kuwa tusingeli pendwa?? Nadhani tatizo sio kununuliwaa bali kufikia hatua ya kuwanunua.
Je, tutawaanunua waliowachagua?? Ningeshauri, njia hii ife tutafute njia mbadala.Mpaka sasa hawafurukuti, tumeshawashikisha adabu kiuchumi, kuwanunua sio njia nzuri.
 
Kwa nini muandike na mate kumbe wino upo? Hivi yule wa JPM na madiwani wake 7 au 8 bado wako njiani au ndo huyo?
 
Huyo akitoka wapo wengine ambao wanaisubiri hiyo nafasi kwa hamu wanatamani hata afe...Chadema ni kama basi anashuka mtu wanapanda watu.
Lisu alishasema kuna tofauti ya mtu aliyeenda bungeni kwa ajili ya kuibana na kuikosoa serikali itekeleze jambo fulani na walioenda bungeni kwa kutanguliza matumbo mbele
Nafasi wataichukuaje wakati wamesusia uchaguzi?
 
Kuna Taarifa tunaendelea kuzifatilia zinasema Mbunge mwingine wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Ameshafikia Bei La fungu na Mandalizi ya Mwisho yanaendelea na Ndani ya siku Saba kwanzia Leo atatimkia CCM

Tunaendelea kufatilia Tutawajuza nini Kinaendelea
mleta mada ebu ongeza nyama(madini) kidogo maana habari inaonekana ya kimbea sana
 
Du,kuanzia leo siiamin chadema kamwe,,hawa viongoz wake nirahis sana kuuza nchi wakipewa madaraka ukiona chama kina kiongoz ngaz ya ubunge ananunulika kipumbavu namna hii pamoja nakua ameshapewa shangingi namakorombwezo yakutosha,sasa huyo siku akiwa wazir wamadin sindoatatuuza mpaka ss wanachi,,?hawa watu hawafai kabisa
Kule waendako pia watapewa madaraka makubwa. Je utawaamini au hutawaamini. Na je, sheria ya rushwa ni kwa yule anayepokea tu au ni pamoja na yule atoae.?
Unamwamini aliye nunua lakini humwamini aliye nunuliwa[emoji87]
 
Pia kuna tetes kuwa Nape na Kinana wakachomoka
 
Kuna waandishi na wachangiaji wengine humu wanashangilia hamahama hii ya viongozi wa kuchaguliwa kwa furaha ya ajabu! Wanasahau jambo moja la maana sana kuwa uchaguzi ni gharama na gharama hizo hazibebwi na mwingine bali walipakodi maskini wa nchi hii. Badala ya kukemea tabia hii ya kipuuzi inayowanyima ndugu zetu maji safi, barabara na dawa mahospitalini tunachekelea na kushangilia as if hazina yetu imeongezewa chochote!
Hawa wanaohama walitakiwa kushtakiwa kwa kuitia nchi hasara kwani naamini hakina bajeti yao.
Tuwazodoe ili waache ulimbukeni wao!
Ishitakiwe Katiba inayoruhusu marudio ya chaguzi mara mbunge anapojiuzulu bila kujali sababu ya Kufanya hivyo lkn ishitakiwe kwa kutoa uhuru wa mtanzania kuhama chama.
 
Sipati picha kama hiki chama kingepewa nchi,halafu kati ya wabunge wanaodai kununuliwa mmoja angekuwa waziri wa ulinzi,mwingnne waziri wa mambo ya ndani,sijui Tanzania ingekuwa wapi kwa mfano.
inavyoonekana kuna vyama haviandai wanachama wao kuwa viongozi,na wanapopata uongozi bado hawbndaliwa kuwa viongozi.
ni hatari sana kwa nchi kuwa na watu wanaonunulika huku vyama vyao vikiwaamini.
kama mnataka nchi basi andaeni kizazi kipya cha viongozi.
kuweni na wanachama chipukizi watakaolelewa ktk misingi na itikadi ya kuamini vyama vyao.
SIASA NI KUJIPANGA,UKIKOSEA MCHEZO UMELIWA.
Hao CCM wanaowanunua kwanni hulalamiki ila unalalmikia wanaochukua hongo kutokana na njaa zao

Hao ccm waliouza nchi kupitia mikataba mibovu na sheria mbovu kabisa ndio unawaamini??? Yaani mbunge mmoja wa upinzani ndio akufanye usiamini kambi nzima alafu unaiamini serikali ya ccm ambao kwa miaka 50 wameuza tembo wetu na madini yetu kwa wazungu

Ur not serious
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom