Siku aliyozaliwa Yesu bado Kitendawili

Hebu tueleze japo kidogo, kuna dhambi gani kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu?
Pia kusherehekea birthday kuna ubaya gani?
Eleza hayo inawezekana tukakuelewa.
Ndugu, sijasema ni DHAMBI au Si DHAMBI kusherehekea!!

Nilichowauliza wakristo, Kanisa, maelekezo ya kusherehekea Christmas tarehe 25 December wameyatoa wapi?

Je ni maelekezo ya Roho mtakatifu kusherehekea Christmas tarehe 25 December na BIRTHDAYS?

Karibu🙏
 
Una ushahidi wa kimaandiko kuhusu Ruhusa hiyo?

Roho mtakatifu ndani Yako anakushuhudia kuwa unachofanya ni sahihi mwana wa Mungu Donatila ?
Kwako wewe ushahidi ni maandiko tu?

Utakuwa ni mlokole au msabato
 
Unaamini Yesu kupitia Roho MTAKATIFU angetaka tusherehekee Christmas, angeshindwa kutupa exact date ya kusherehekea Kuzaliwa kwake?

KWANINI siku hiyo ametuficha?
 
Ingekuwa ni Jambo baya ndo tungeanza kuhoji ni maelekezo ya nani yameleta 25december iwe siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu. Kama sio dhambi hakuna mantiki ya kujadili jambo hili.
Kwenye birthday naona napo kama unapinga au sijakuelewa vizuri?
 
Ingekuwa ni Jambo baya ndo tungeanza kuhoji ni maelekezo ya nani yameleta 25december iwe siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu. Kama sio dhambi hakuna mantiki ya kujadili jambo hili.
Kwenye birthday naona napo kama unapinga au sijakuelewa vizuri?
Nimewauliza wakristo swali Hilo,


Wakristo wanaoongozwa na Roho mtakatifu, Je ni Yeye ndiye aliyewaelekeza kusherehekea Christmas tarehe 25 December?

Ni Yeye amewaelekeza juu ya umuhimu wa kusherehekea siku ya Kuzaliwa, BIRTHDAYS?
 
Unaamini Yesu kupitia Roho MTAKATIFU angetaka tusherehekee Christmas, angeshindwa kutupa exact date ya kusherehekea Kuzaliwa kwake?

KWANINI siku hiyo ametuficha?
ili upate tarehe hiya anzia kuitafuta kwa yohana mbatizaji mama yake alipata ujauzito kipindi gani, njoo kwa mariamu ndio utajua ni kipindi gani Yesu alizaliwa
 
Nimewauliza wakristo swali Hilo,


Wakristo wanaoongozwa na Roho mtakatifu, Je ni Yeye ndiye aliyewaelekeza kusherehekea Christmas tarehe 25 December?

Ni Yeye amewaelekeza juu ya umuhimu wa kusherehekea siku ya Kuzaliwa, BIRTHDAYS?
We roho mtakatifu amekuelekezaje kwani hadi unauliza wengine?
 
Tatizo mnalazimisha Ukiristo iwe ni Dini, wakati ata Yesu mwwnyewe haijui hiyo dini
 
Yesu huyo hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Ndio maana hata kuzaliwa kwake hakujulikani kwa vile Yesu ni Fictional character invented by religion to scam people.
 
Kwenye hiyo picha ya huyo jamaa aliyenyoosha vidole viwili kuna wahuni walim edit wakamshikisha fegi kati kati ya hivyo vidole
REJEA AMRI 10 ZA MUNGU usijifanyie kitu chochote chochote kilichopo juu mbinguni wala kukitumikia,kukiabudu sasa mapicha ya yesu katika torati ya musa haitakiw au katika taifa la Israel mpaka Leo hakuna hiko kitu
 
Hili swali lako halijibiki kwasababu wafia dini wamelevywa na mvinyo wa dini
 
Kwako wewe ushahidi ni maandiko tu?

Utakuwa ni mlokole au msabato
Bila maandiko unathibitishaje ?
Au wewe ndio wale wafuasi wa Geodav anadai anaongea na Yesu kila siku huenda akina Gwajima, Mwamposya na Manabii wa digital wana majibu ya tarehe kwa kutumia njia ya mkato
 
KWANINI TUNASHEREHEKEA CHRISTMAS MWEZI 12?

Na@Frt.Shirima

Watu wamekuwa wakijiuliza, Ikiwa Bikira Maria alichukiwa Mimba Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu katika Mwezi wa 6, je! Inakuwaje Yesu azaliwe Mwezi wa 12? Kwahiyo alizaliwa akiwa tu na miezi 6? (Rej. Luk. 1:26-45)

Ipo hivi; pamoja na maelezo Mengine sahihi juu ya kipindi ambacho Bikira Maria alichukuwa Mimba ( The Years Before the Common Era), maana Yesu alizaliwa mwaka wa 1, yapo maelezo Mengine ambayo huitwa FUNDISHO JUU YA CHRISTMAS kama tutakavyoona.
Kwanza wakati Bikira Maria anachukuwa Mimba, Ikumbukwe hapakuwa na Utaratibu wa kuhesabu miaka Kwa kwenda Mbele kama ilivyo Sasa (A.D), LAKINI PIA IKUMBUKWE CHRISTMAS HAIKUWEKWA MARA TU BAADA YA YESU KUZALIWA, Bali iliwekwa baadaye.

Tuanze hivi; Mwanzo wa Krismasi umechipukia kutoka tamaduni za kipagani na za kirumi. Warumi walisherekea sikukuu mbili katika mwezi Desemba (12).

Sikukuu ya kwanza iliitwa Saturnalia, ambapo waliisherekea kwa wiki mbili wakimheshimu mungu wao wa kipagani aliyeitwa Saturn (jina la moja kati ya sayari). Huyu kwao alikuwa mungu wa kilimo.

Sikukuu nyingine ni ya kuzaliwa kwa Mithra au mungu Jua (kwa sababu waliliabudu jua) ambayo ilifanyika tarehe 25 Desemba.

Sherehe zote mbili walizisherekea kwa kufuru ya hali ya juu ya kufanya zinaa na kunywa pombe nyingi.
Code:
Na kwa sababu mwezi Desemba ulikuwa na giza nene kuliko miezi mingine waliwasha mishumaa na kusherekea
usiku mzima.

Ukristo ulipokuwa ukienea bara la Ulaya, maklero wamisionari hawakuweza kutokomeza kirahisi tamaduni hizi zilizozoeleka kwa miaka mingi sana ( ilikuwa ni kazi ngumu Mno).

Na kwa sababu hakuna aliyefahamu kwa uhakika wote wa tarehe haswa ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo waliamua kutumia busara ya Roho Mtakatifu kuweka hapo hiyo tarehe ya kipagani ya kufanya ufuska wa kusherekea miungu yao (mungu Jua) na badala yake kusherekea kuzaliwa kwa Yesu tarehe hiyo hiyo ya 25 Desemba (ambapo wapagani walisherekea mungu Jua).

Na tafsiri iliyokuwepo miongoni mwa wapagani, ilibadilika, ikawa kwamba Yesu ndiye Jua la kweli na la haki na takatifu, pambazuko la uumbaji mpya liletalo ukombozi dhidi ya ushetani wa kipagani na kuleta uzima wa utakatifu wa Mungu kwa watu wote wa ulimwengu kama ilivyoelezwa katika Maandiko Matakatifu na ndiyo Chimbuko la kusherehekea Christmas December 25.

Hii ilisaidia pia kuwaongoa wapagani wengi ambao Walikuwa wakiabudu wasichokifahamu, hivyo Maklero waliwafundisha habari za jua wa haki huyo, ambaye ni Kristo Yesu.

Tushirikishane Tone la Upendo.
Na.Frt. Shirima
 
Hatujui Yesu alizaliwa tarehe gani wala mwezi gani, ila tumechagua kusheherekea siku yake ya kuzaliwa Dec.25.
 
it is true but we can do it in glory of our God JESUS ....
ile sikukuu ya kuzaliwa kwa mungu wa Jua Tammuz sisi tunaivunja na kufanya Kuwa Siku ya Kuzaliwa kwa Mkombozi Yesu.....

biblia imesema lolote unalo lifanya basi lifanye kwa ajili ya UTUKUFU wa Mungu.....

the most important thing for any christian is NOT A DAY but Accepting JESUS Christ as a survivor ....ndio maana hata Mungu hajaaona umuhimu wa kukuandikia siku ya Kuzaliwa Yesu katika biblia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…