Siku ambayo askari MP alipojitayarisha kumpiga risasi askari Sajenti kwa amri ya Mkuu wa Kambi ya Mgambo JKT

We uache ubishi we sema tu kwamba kimazoea luteni wa kwanza mnamuita "luteni" bas tutakuelewa ila ki rasmi anaitwa luteni wa kwanza na kiukweli jeshini hakuna cheo kinachoitwa luteni bila kufuatiwa na neno lingine.

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
Unaongea academically badala ya conventionally. Sasa kama ukitaka tuongee academically, huo ni uwanja mwingine. Kumbishia mtu kwa sababu unataka awe academically correct ni kujitoa kwenye ulimwengu wa uhalisia. Kuna siku utabishana na Mluguru ambaye anakuambia nimekuambia kanikatie tiketi ya basi wewe unaniletea tiketi ya Dar Eksipresi. Ticket ya basi ni Abudu Basi!

Nenda kambi yeyote ya JWTZ usikie kama kuna Luten anaitwa luteni wa kwanza!
 
Na kama niko kambini niende wapi[emoji16][emoji16]

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Ni jambo ambalo sintalisahau maishani mwangu, japo lilitokea zaidi ya miaka 20 iliyopita. Leo nimeamua kulisimulia kwa kuwa nadhani kwa sasa limefikia hatua ya kuwa "declassified" hata kama lilikuwa ni siri, ila sintataja majina ya wahusika.

Ilikua usiku mmoja katika kambi ya JKT Mgambo, katika sehemu moja ya starehe watu walikuwa wakinywa na kuburudika kwa vinywaji mbalimbali pamoja na bia, wakihudumiwa na wasichana warembo service girls. Katika sehemu hii, alikuwapo pia Mkuu wa Kambi, ama CO kama tulivyowaita mara nyingi.

Sasa tunajua kwamba pombe sio chai, na baada ya bia mbili au tatu watu hubadilika katika kufikiri kwao na hata kutenda. Katika harakati za kuhudumia watu, service girl moja alipokuwa akipita katikati ya meza za wateja wake, aliangusha chupa ya bia ya askari Luteni ikapasuka na bia kumwagika. Luteni (nimekumbushwa kwamba alikuwa Luteni mmoja bongebonge sio Sajenti na mtu aliekuwapo Mgambo) huyu alikuja juu kama vile amepoteza maji yake ya uzima! Alianza kumfokea yule service girl kwa uzembe kwa sauti ya juu.

Sasa Mkuu wa Kikosi alipoona hivyo alitoa amri kwa Luteni, "kamanda acha kelele! Service girl, mpe bia nyingine kamanda kufidia iliyovunjika"

Basi yule service girl alienda kumletea Luteni bia nyingine. Sasa jambo la ajabu ni kwamba yule Luteni alipoletewa bia kufidia iliyovunjia, bado akaendelea kumbwatukia yule service girl. Kitendo hiki kikamuudhi sana Mkuu wa Kikosi, akasema kwa hasira, "Kamanda, umerudishiwa bia yako na bado unapiga kelele, haya inuka nenda mahabusu sasa hivi"

Kwa ujasiri wa ajabu yule Luteni hakuinuka. Mkuu wa Kikosi akarudia tena, "Kamanda nakuamuru jipeleke mwenyewe mahabusu". Yule Luteni aliendelea kukaa pale kwenye kiti huku akigumia kwamba huo ulikuwa uonevu, kwa sababu bia yake ilivunjwa kwa uzembe.

Sasa Mkuu wa kikosi alikuwa na dereva wake MP nje ambaye alikuwa na SMG. Aliitwa ndani na Mkuu wa Kikosi akaambiwa "askari, koki silaha, mlenge sajenti". SMG ilitoa mlio wa vyuma kugongana wakati ikikokiwa, sauti ambayo wale wanaozijua bunduki watakuwa wanaifahamu vizuri. Ni mlio wa pekee sana.

Kisha Mkuu wa Kikosi akasema, "Kamanda, nakuamuru kwa mara ya mwisho inuka jipeleke mwenyewe mahabusu"

Watu wote pale ukumbini wakawa kimya, ungeweza hata kusikia kishindo cha sisimizi wakitembea!

Yule Luteni aligeuka akaona SMG imeelekezwa kwake, na akajiinua taratibu na kuanza kuondoka kwenda mahabusu huku akisema kwa chini chini hii sio sawa.

Baada ya Luteni kuondoka, kulikuwa bado na kimya cha kama sekunde 30 hivi, na Mkuu wa Kikosi akasema "tuendelee kuburudika na kufurahi"

Lilikuwa na gumzo lililotawala kikosini kwa muda mrefu, watu wakijiuliza hivi Luteni angekataa kuinuka Mkuu wa Kikosi angemwambia dereva mpige risasi? Dereva angetii? Mimi niliamini kwa dhati kwamba Mkuu wa Kikosi angetoa amri Luteni apigwe risasi na dereva angetii, kwa sababu tu ya Mkuu wa Kikosi kulinda heshima yake.

Lakini jambo moja lilikuwa wazi kwangu, kwamba wote Luteni na Mkuu wa kikosi walifikia hatua ile kutokana na kwamba walikuwa wamekunywa bia. Na kwa mara nyingine niliona wazi kwamba kweli pombe sio chai!
Yule Luteni aikuwa cock up!
Kukataa amri ya CO ni utovu mkubwa wa adabu.
Angepigwa risasi angejilaumu mwenyewe.
 
Hivi akili yako ina nini?

Nimekuambia Lieutenant jeshini ni cheo cha nyota mbili, lakinini pia neno lieutenant linatumika kama prefix kwa kanali na jenerali.

Umewahi kuona mtu amevaa cheo chenye alama ya nyota mbili na ngao? Unamwitaje?

Na mtu mwenye nyota mbili, unamwitaje?

Usijifanye kujua wakati hujui
Huyu jamaa kuna vitu vingi havijui na ninahisi atakuwa alipita jeshini kama mujibu wa sheria( wale wanaomalizaga form six na kusombwa). Kwahiyo kuna baadhi ya mambo alimeza ndo analeta hapa. KAMA BADO ANAJUA SAMEJA NI SEHEMU YA RANKS ZA KIJESHI KWELI KAZI IPO.
 
Ni jambo ambalo sintalisahau maishani mwangu, japo lilitokea zaidi ya miaka 20 iliyopita. Leo nimeamua kulisimulia kwa kuwa nadhani kwa sasa limefikia hatua ya kuwa "declassified" hata kama lilikuwa ni siri, ila sintataja majina ya wahusika.

Ilikua usiku mmoja katika kambi ya JKT Mgambo, katika sehemu moja ya starehe watu walikuwa wakinywa na kuburudika kwa vinywaji mbalimbali pamoja na bia, wakihudumiwa na wasichana warembo service girls. Katika sehemu hii, alikuwapo pia Mkuu wa Kambi, ama CO kama tulivyowaita mara nyingi.

Sasa tunajua kwamba pombe sio chai, na baada ya bia mbili au tatu watu hubadilika katika kufikiri kwao na hata kutenda. Katika harakati za kuhudumia watu, service girl moja alipokuwa akipita katikati ya meza za wateja wake, aliangusha chupa ya bia ya askari Luteni ikapasuka na bia kumwagika. Luteni (nimekumbushwa kwamba alikuwa Luteni mmoja bongebonge sio Sajenti na mtu aliekuwapo Mgambo) huyu alikuja juu kama vile amepoteza maji yake ya uzima! Alianza kumfokea yule service girl kwa uzembe kwa sauti ya juu.

Sasa Mkuu wa Kikosi alipoona hivyo alitoa amri kwa Luteni, "kamanda acha kelele! Service girl, mpe bia nyingine kamanda kufidia iliyovunjika"

Basi yule service girl alienda kumletea Luteni bia nyingine. Sasa jambo la ajabu ni kwamba yule Luteni alipoletewa bia kufidia iliyovunjia, bado akaendelea kumbwatukia yule service girl. Kitendo hiki kikamuudhi sana Mkuu wa Kikosi, akasema kwa hasira, "Kamanda, umerudishiwa bia yako na bado unapiga kelele, haya inuka nenda mahabusu sasa hivi"

Kwa ujasiri wa ajabu yule Luteni hakuinuka. Mkuu wa Kikosi akarudia tena, "Kamanda nakuamuru jipeleke mwenyewe mahabusu". Yule Luteni aliendelea kukaa pale kwenye kiti huku akigumia kwamba huo ulikuwa uonevu, kwa sababu bia yake ilivunjwa kwa uzembe.

Sasa Mkuu wa kikosi alikuwa na dereva wake MP nje ambaye alikuwa na SMG. Aliitwa ndani na Mkuu wa Kikosi akaambiwa "askari, koki silaha, mlenge sajenti". SMG ilitoa mlio wa vyuma kugongana wakati ikikokiwa, sauti ambayo wale wanaozijua bunduki watakuwa wanaifahamu vizuri. Ni mlio wa pekee sana.

Kisha Mkuu wa Kikosi akasema, "Kamanda, nakuamuru kwa mara ya mwisho inuka jipeleke mwenyewe mahabusu"

Watu wote pale ukumbini wakawa kimya, ungeweza hata kusikia kishindo cha sisimizi wakitembea!

Yule Luteni aligeuka akaona SMG imeelekezwa kwake, na akajiinua taratibu na kuanza kuondoka kwenda mahabusu huku akisema kwa chini chini hii sio sawa.

Baada ya Luteni kuondoka, kulikuwa bado na kimya cha kama sekunde 30 hivi, na Mkuu wa Kikosi akasema "tuendelee kuburudika na kufurahi"

Lilikuwa na gumzo lililotawala kikosini kwa muda mrefu, watu wakijiuliza hivi Luteni angekataa kuinuka Mkuu wa Kikosi angemwambia dereva mpige risasi? Dereva angetii? Mimi niliamini kwa dhati kwamba Mkuu wa Kikosi angetoa amri Luteni apigwe risasi na dereva angetii, kwa sababu tu ya Mkuu wa Kikosi kulinda heshima yake.

Lakini jambo moja lilikuwa wazi kwangu, kwamba wote Luteni na Mkuu wa kikosi walifikia hatua ile kutokana na kwamba walikuwa wamekunywa bia. Na kwa mara nyingine niliona wazi kwamba kweli pombe sio chai!
Kikosini kwetu Bulombora JKT iliwahi kutokea hivi:
Alikuwepo Ofisa mmoja very smart, very strong halafu alikuwa mrefu kupita maofisa wote waliokuwepo kikosini pale. Akiwa antembea, utafikiri anapiga kwata. Alikuwa anaitwa Kepteni Golita.
Golita alitoka siku moja kwenda kunywa pombe mtaani, kijiji kimoja mbali kidogo kinaitwa Kaseke. Bahati mbaya ya kwenye pombe ni mengi, sijui kilitokea nini, ugomvi ukawa umetokea . Golita akapigwa ngeu kichwani almanusura ubongo utoke nje. Alirudije kikosini na hatimaye kupata matibabu hizo details nilshazisahau.
Baada ya Golita kuwa amepigwa ngeu akiwa kwenye pombe Kaseke, kukaratibiwa mpango pale Kikosini. Wanajeshi wakatoroka kikosini na Lorry la kikosi tulikuwa tunaliita NISSAN (Nissan UD), CO Mwankenja akiwa hana taarifa. Lorry hilo likaenda likafanya operesheni Kaseke kijiji kizima kikapigwa, mkong'oto ulitembea hadi kwa watoto wadogo. Baada ya mkong'oto huo, kesho yake tena wanajeshi hao hao wakarudi Kaseke kwenda kunywa pombe huko! Mambo ya jeshi haya!
 
Naona Ni maafisa wote ndio wanachangia hoja yao haya nasoma comment ...ila nyinyi maafisa jkt mliwai kuninyanyasa kipindi fln katka ukumbi wa jkt njiro nane ane cntasahau ile siku mlininyanyasa kisa tu Kuna jamaa ambae nilikuja nae pale kunywa bas alivyolewaa akamuita kijana mmoja na kumuambia anikamate kwa kuwa nazingua pale nilipigwa bila kosa yule jmaa alikuwa ameajiriwa uamiaji baada ya kunifanyia huyu ujinga ajakah sna kazin akafukuzwa kwa matumiz ya madaya ya kulevya..aliwaamuru wale vjina wanikamate na kunipiga eti kwa kuwa na yeye Ni askar wa uamiaji Ni mwezao ..
 
Unapoingia jeshini bado una maji magotini hujui hata kupiga mguu upande, wewe ni kuruta. Kwa JKT hupewi hata kombati, unavaa bukta na vesti.

Unapokuwa umamaliza mafunzo yote ya msingi ya jeshi lakini wewe ni askari bila cheo chochote, wewe ni private. Ukiona polisi au mwanajeshi hana kitu chochote begani, huyo ni private
kwenye geshi la polish ni konstebo
 
Ahaa, kwa hiyo Lieutentant sio cheo kwa kuwa kuna first na second?

Sasa huo sio utaratibu wa JWTZ. Sisi nyota mbili tunaita Luteni, kama unatuletea mambo ya USA nenda USA kaongelee puani tuondolee shombo za kina Trump hapa.
Jamaa ni mbishi tu "Sijui ni Muha wa wapi pale kigoma "
Mimi ukisema tu luteni nakua nishakuelewa.
 
Kikosini kwetu Bulombora JKT iliwahi kutokea hivi:
Alikuwepo Ofisa mmoja very smart, very strong halafu alikuwa mrefu kupita maofisa wote waliokuwepo kikosini pale. Akiwa antembea, utafikiri anapiga kwata. Alikuwa anaitwa Kepteni Golita.
Golita alitoka siku moja kwenda kunywa pombe mtaani, kijiji kimoja mbali kidogo kinaitwa Kaseke. Bahati mbaya ya kwenye pombe ni mengi, sijui kilitokea nini, ugomvi ukawa umetokea . Golita akapigwa ngeu kichwani almanusura ubongo utoke nje. Alirudije kikosini na hatimaye kupata matibabu hizo details nilshazisahau.
Baada ya Golita kuwa amepigwa ngeu akiwa kwenye pombe Kaseke, kukaratibiwa mpango pale Kikosini. Wanajeshi wakatoroka kikosini na Lorry la kikosi tulikuwa tunaliita NISSAN (Nissan UD), CO Mwankenja akiwa hana taarifa. Lorry hilo likaenda likafanya operesheni Kaseke kijiji kizima kikapigwa, mkong'oto ulitembea hadi kwa watoto wadogo. Baada ya mkong'oto huo, kesho yake tena wanajeshi hao hao wakarudi Kaseke kwenda kunywa pomebe huko! Mambo ya jeshi haya!
I say pale Mgambo kuna jamaa yetu alienda kijijini kunywa gongo. Sasa kosa alolofanya ni kuja na chupa ya gongo kikosini. Alipelekwa court martial akafungwa uraiani miezi miwili!
 
Naona kosa lilikuwa kubwa kiasi kwamba kifungo cha kikosini kilikuwa hakitoshi tena. Vipi baada ya kutoka jela alirudishwa kazini tena?
 
Hakuwa askari, tulikuwa nae kwa mujibu wa sheria baada ya form six. Na muda wa jela uraiani ilibidi aufidie wakati wa kumaliza.
 
Hakuwa askari, tulikuwa nae kwa mujibu wa sheria baada ya form six
Alikuwa ni Askari, sema hakuwa mwajiriwa.
Kumbuka siku unaingia kikosini, uliapishwa na RSM ukiambiwa kuwa "kuanzia leo utaitwa kruta....." This word "kruta" is just a synonymous swahili word for the english word "new recruit"
 
Alikuwa ni Askari, sema hakuwa mwajiriwa.
Kumbuka siku unaingia kikosini, uliapishwa na RSM ukiambiwa kuwa "kuanzia leo utaitwa kruta....." This word "kruta" is a just a synonymous swahili word for the english word "new recruit"
Aaah, hebu fikiria una experience jela kupitia JKT! Majeshi si lelemama tuzidi kuombeana, tuliimba hivyo.

Ila alisema akiwa jela uraiani jamaa askari wa Magereza walikuwa wanamstahi sana, wanamuona askari mwenzao, na mara nyingi wanakuweka jikoni kupika au kazi sushi nyingine. Baada ya JKT jamaa alienda UD

Ila sasa sijui kama inahesabika kuwa criminal record, maana hata mie hukumu za lupango nilizila sana. Nilikuwa sitaki ujinga na green kwanja. Ngumi mkononi!

Katika watu wachache waliopewa extra drill, nilikuwamo. Niliwahi kupigwa Extra dirll 1x3 za dakika 45. Moja kila siku siku tatu.

Nilikuwa nawaambia makopro wa kombania lazima niende Arusha kupata u-kadet, na nikirudi watanikoma. Nitakuwa luteni wao bado NCOs, nitawalima sana guard duty!!!!
 
Naomba elimu kidogo tofauti ya KURUTA na PRIVATE

Tafadhali
Mimi sio askari lakini ninachofahamu mimi kuruta ni askari ambaye ndio ameanza mafunzo ya awali kutoka kuwa raia na kuwa askari.
Private anakuwa amemaliza mafunzo lakini begani hana kitu,hajapewa V
 
Naona Ni maafisa wote ndio wanachangia hoja yao haya nasoma comment ...ila nyinyi maafisa jkt mliwai kuninyanyasa kipindi fln katka ukumbi wa jkt njiro nane ane cntasahau ile siku mlininyanyasa kisa tu Kuna jamaa ambae nilikuja nae pale kunywa bas alivyolewaa akamuita kijana mmoja na kumuambia anikamate kwa kuwa nazingua pale nilipigwa bila kosa yule jmaa alikuwa ameajiriwa uamiaji baada ya kunifanyia huyu ujinga ajakah sna kazin akafukuzwa kwa matumiz ya madaya ya kulevya..aliwaamuru wale vjina wanikamate na kunipiga eti kwa kuwa na yeye Ni askar wa uamiaji Ni mwezao ..
Dah wabongo walimbukeni sana wa vyeo,aisee kama ni mimi nisingekubali ningemfanyia mission mtaani.
Tena huko arusha ukiwapa vijana elfu 50 tu wanafanya unachotaka.
 
Jamaa ni mbishi tu "Sijui ni Muha wa wapi pale kigoma "
Mimi ukisema tu luteni nakua nishakuelewa.
Mkuu mimi wote nimewaelewa na wote wako sahihi.
Kwenye kila mahali kuna lugha ya mkato na iliyozoeleka.
Kwa jinsi ilivyozoeleka hata uraiani ukisema Luteni watu wanaelewa umemaanisha mtu mwenye cheo cha nyota mbili lakini sio formal.
Ni sawasawa ukienda dukani ukamwambia naomba vocha muuzaji atakuelewa na atakupatia mobile credit card ya kuongeza salio kwenye simu yako lakini sio neno sahihi/rasmi.
 
Back
Top Bottom