Siku ambayo askari MP alipojitayarisha kumpiga risasi askari Sajenti kwa amri ya Mkuu wa Kambi ya Mgambo JKT

Siku ambayo askari MP alipojitayarisha kumpiga risasi askari Sajenti kwa amri ya Mkuu wa Kambi ya Mgambo JKT

Mkuu mimi wote nimewaelewa na wote wako sahihi.
Kwenye kila mahali kuna lugha ya mkato na iliyozoeleka.
Kwa jinsi ilivyozoeleka hata uraiani ukisema Luteni watu wanaelewa umemaanisha mtu mwenye cheo cha nyota mbili lakini sio formal.
Ni sawasawa ukienda dukani ukamwambia naomba vocha muuzaji atakuelewa na atakupatia mobile credit card ya kuongeza salio kwenye simu yako lakini sio neno sahihi/rasmi.
Yupo sahihi ila ana complicate sana.
Asante.
 
Mimi sio askari lakini ninachofahamu mimi kuruta ni askari ambaye ndio ameanza mafunzo ya awali kutoka kuwa raia na kuwa askari.
Private anakuwa amemaliza mafunzo lakini begani hana kitu,hajapewa V
Kuruta ni recruit. Kiswahili sahihi ni msajiliwa. Ukishajua hilo basi mengine yanatiririka tu.

Unajua jeshini bwana ni babu zetu walikuwa wanatamka maneno ya kizungu kwa Kiswahili.

Hivi unajua kuwa "Ajua" maana yake ni "as you were"

Utakuta afande amekazana nyuma geuka, ajua! Mnanitania, mnageuka kama babuni anataka kuona matako yake kama yamebadilika rangi, kurutaa!! Afandeee!
 
Kuruta ni recruit. Kiswahili sahihi ni msajiliwa. Ukishajua hilo basi mengine yanatiririka tu.

Unajua jeshini bwana ni babu zetu walikuwa wanatamka maneno ya kizungu kwa Kiswahili.

Hivi unajua kuwa "Ajua" maana yake ni "as you were"

Utakuta afande amekazana nyuma geuka, ajua! Mnanitania, mnageuka kama babuni anataka kuona matako yake!
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Basi kuna Mmasai mmoja mrefu sana tulikuwa nae jeshini. Sasas yeye mkiambiwa mbele tembea, alikuwa anajichanganya sana kuanza. Unakuta mara kaanza na mguu wa kushoto mara wa kulia. Sasa akitaka kurekebisha anajikuta anapeleka mkono na mguu wa upande mmoja mbele!

Sasa siku moja afande kamwambia, na wewe ndio kutembea gani huko unatuletea jeshini? Jamaa akasema afande, mie nasaliwa hivihivi siwezi!

Ennhe, greenkwanja wakarukia, afande, huyu anamtukana mama yake huyu, anasema mama yake nae anatembea hivi!!!

Yaani jeshini mara nyingine ilikuwa burudani sana🤣🤣🤣🤣
 
Sio kweli, linakuwa na sheria zinazo eleweka, na viongozi wanao jitambua. Kiongozi anaejua akitoa amri isio halali haitatekelezwa na atawajibishwa kwa kutoa amri hiyo, huwa yuko makini. Hapa kwetu askari anaepokea amri yoyote, hata akivalishwa nguo za kipolisi na kumwambia sense kupiga wafuasi wa Chadema, hana la kuhoji.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
ndio akili ya askari inatakiwa iwe hivyo
 
Ni jambo ambalo sintalisahau maishani mwangu, japo lilitokea zaidi ya miaka 20 iliyopita. Leo nimeamua kulisimulia kwa kuwa nadhani kwa sasa limefikia hatua ya kuwa "declassified" hata kama lilikuwa ni siri, ila sintataja majina ya wahusika.

Ilikua usiku mmoja katika kambi ya JKT Mgambo, katika sehemu moja ya starehe watu walikuwa wakinywa na kuburudika kwa vinywaji mbalimbali pamoja na bia, wakihudumiwa na wasichana warembo service girls. Katika sehemu hii, alikuwapo pia Mkuu wa Kambi, ama CO kama tulivyowaita mara nyingi.

Sasa tunajua kwamba pombe sio chai, na baada ya bia mbili au tatu watu hubadilika katika kufikiri kwao na hata kutenda. Katika harakati za kuhudumia watu, service girl moja alipokuwa akipita katikati ya meza za wateja wake, aliangusha chupa ya bia ya askari Luteni ikapasuka na bia kumwagika. Luteni (nimekumbushwa kwamba alikuwa Luteni mmoja bongebonge sio Sajenti na mtu aliekuwapo Mgambo) huyu alikuja juu kama vile amepoteza maji yake ya uzima! Alianza kumfokea yule service girl kwa uzembe kwa sauti ya juu.

Sasa Mkuu wa Kikosi alipoona hivyo alitoa amri kwa Luteni, "kamanda acha kelele! Service girl, mpe bia nyingine kamanda kufidia iliyovunjika"

Basi yule service girl alienda kumletea Luteni bia nyingine. Sasa jambo la ajabu ni kwamba yule Luteni alipoletewa bia kufidia iliyovunjia, bado akaendelea kumbwatukia yule service girl. Kitendo hiki kikamuudhi sana Mkuu wa Kikosi, akasema kwa hasira, "Kamanda, umerudishiwa bia yako na bado unapiga kelele, haya inuka nenda mahabusu sasa hivi"

Kwa ujasiri wa ajabu yule Luteni hakuinuka. Mkuu wa Kikosi akarudia tena, "Kamanda nakuamuru jipeleke mwenyewe mahabusu". Yule Luteni aliendelea kukaa pale kwenye kiti huku akigumia kwamba huo ulikuwa uonevu, kwa sababu bia yake ilivunjwa kwa uzembe.

Sasa Mkuu wa kikosi alikuwa na dereva wake MP nje ambaye alikuwa na SMG. Aliitwa ndani na Mkuu wa Kikosi akaambiwa "askari, koki silaha, mlenge sajenti". SMG ilitoa mlio wa vyuma kugongana wakati ikikokiwa, sauti ambayo wale wanaozijua bunduki watakuwa wanaifahamu vizuri. Ni mlio wa pekee sana.

Kisha Mkuu wa Kikosi akasema, "Kamanda, nakuamuru kwa mara ya mwisho inuka jipeleke mwenyewe mahabusu"

Watu wote pale ukumbini wakawa kimya, ungeweza hata kusikia kishindo cha sisimizi wakitembea!

Yule Luteni aligeuka akaona SMG imeelekezwa kwake, na akajiinua taratibu na kuanza kuondoka kwenda mahabusu huku akisema kwa chini chini hii sio sawa.

Baada ya Luteni kuondoka, kulikuwa bado na kimya cha kama sekunde 30 hivi, na Mkuu wa Kikosi akasema "tuendelee kuburudika na kufurahi"

Lilikuwa na gumzo lililotawala kikosini kwa muda mrefu, watu wakijiuliza hivi Luteni angekataa kuinuka Mkuu wa Kikosi angemwambia dereva mpige risasi? Dereva angetii? Mimi niliamini kwa dhati kwamba Mkuu wa Kikosi angetoa amri Luteni apigwe risasi na dereva angetii, kwa sababu tu ya Mkuu wa Kikosi kulinda heshima yake.

Lakini jambo moja lilikuwa wazi kwangu, kwamba wote Luteni na Mkuu wa kikosi walifikia hatua ile kutokana na kwamba walikuwa wamekunywa bia. Na kwa mara nyingine niliona wazi kwamba kweli pombe sio chai!
Hapa analengwa luteni na sajenti ambaye ni MP, au MP analenga sajenti na Luteni? Yaani Luteni anaambiwa na CO ondoka, halafu CO tena anamwambia MP amlenge Sajenti - sijaelewa!
 
mkuu jeshini ni amri tu na nidham mbele bila hivyo kusingekalika kule
Na vitendo pia.
Kuna kambi moja nasikia CO alirudi kalewa alipofika lango kuu aliaamrishwa ajitambulishe, akakataa, then akapelekewa moto na kuelekea kuzimu!
 
Hapa analengwa luteni na sajenti ambaye ni MP, au MP analenga sajenti na Luteni? Yaani Luteni anaambiwa na CO ondoka, halafu CO tena anamwambia MP amlenge Sajenti - sijaelewa!
Hujaelewa kwa kuwa hujasoma thread vizuri.

Nimesema kwamba, mara ya kwanza niliandika ni Sajenti aliyetaka kupigwa risasi. Kuna jamaa alikuwapo Mgambo akaweka post kwamba hapana, yule jamaa aliyetaka kupigwa risasi alikuwa Luteni mmoja Msukuma bongebonge hivi, sio sajenti. Kwa hiyo nikarekebisha, ila sasa siwezi kurekebisha kichwa cha thread. Ndio maana kuna huo mkanganyikano
 
Hujaelewa kwa kuwa hujasoma thread vizuri.

Nimesema kwamba, mara ya kwanza niliandika ni Sajenti aliyetaka kupigwa risasi. Kuna jamaa alikuwapo Mgambo akaweka post kwamba hapana, yule jamaa aliyetaka kupigwa risasi alikuwa Luteni mmoja Msukuma bongebonge hivi, sio sajenti. Kwa hiyo nikarekebisha, ila sasa siwezi kurekebisha kichwa cha thread. Ndio maana kuna huo mkanganyikano
Sawa.
 
🤣🤣🤣 Nadhani ndio maana waliamua kuwawekea bia zao za bei chee ili wasije kunywa uraiani
Dah hivi pale kawe msasani bado ipo ile bar ya jeshi.
Tulikua tunalewa huku tunakula mbata na makonzi utatulia mwenyewe ukichoka utaondoka taratibu.demu ukimuona usitongoze wao huyo🤣🤣🤣
Ila sikukoma,kila w end niko mpk wakanizoea pale.
Aah hapo sasa wachumba walikoma na mi nikajifanya mjeshi basi kiulaini.
Ile sehemu ilikua na mandhari nzuri sana beach kule i mean view ya masaki na msasani ile mijumba,pale bar palikua takataka na upepo mzurii
 
Pale Mgambo miaka hiyo mazinguzi ya silaha yalikwepo saanaa , kuna afande mmoja alikwenda kwa nick name Kablasi, alipigwa marafuku kushika silaha baada ya kumtishia kumshuti ofisa mmoja kwa madai yakuonewa, aliamriwa kutogusa bunduki tena na akafanywa dereva wa punda kutoa mboga garden na kuleta kikosini, tembea yenyewe ya kablasi ilikuwa burudani, wazee wa miaka ile mupo na story za afande kiwembe kata madem
 
Story ninaipata vizuri sana. Ila aliyeleta story ameikosea sana.

Kwanza Sargent hawezi kukaa sehemu moja ya vinywaji na Mkuu wa Kikosi, therefore ile ilikuwa officer's mess.
Unayemtaja kukokiwa bunduki alikuwa na Cheo cha Lieutenant. Msukuma mmoja bongebonge.

Yule CO alikuwa bonge la Kamanda. Alipenda sana seriousness katika kila kazi hasa training mnapokuwa "uwanja wa damu". (R.I.P)

Lakini kwenye burudani alipenda sana jokes (of course pale baada ya kuona jamaa amelewa na hataki kutii amri, alimnong'oneza mtu fulani na kikafanyika kilichofanyika. Ilitumika SRA na si SMG (haikuwa na risasi), maana SRA inalia sana ikikokiwa, na good enough it worked, maana jamaa alisimama juu bila shuruti " paaap".) Ilikuwa burudani tosha!!

Operation nidhamu!!
Nilipangiwa kwenda hiyo kambi, wakati tunajiandaa kwenda utaratibu wa kwenda JKT kwa lazima ukafutwa.

Nyongeza nyingine:
Sasa hivi unakula kuku kwa mrija pande zipi kamanda?
 
Back
Top Bottom