Story ninaipata vizuri sana. Ila aliyeleta story ameikosea sana.
Kwanza Sargent hawezi kukaa sehemu moja ya vinywaji na Mkuu wa Kikosi, therefore ile ilikuwa officer's mess.
Unayemtaja kukokiwa bunduki alikuwa na Cheo cha Lieutenant. Msukuma mmoja bongebonge.
Yule CO alikuwa bonge la Kamanda. Alipenda sana seriousness katika kila kazi hasa training mnapokuwa "uwanja wa damu". (R.I.P)
Lakini kwenye burudani alipenda sana jokes (of course pale baada ya kuona jamaa amelewa na hataki kutii amri, alimnong'oneza mtu fulani na kikafanyika kilichofanyika. Ilitumika SRA na si SMG (haikuwa na risasi), maana SRA inalia sana ikikokiwa, na good enough it worked, maana jamaa alisimama juu bila shuruti " paaap".) Ilikuwa burudani tosha!!
Operation nidhamu!!