Von Bismarck
JF-Expert Member
- Jul 11, 2018
- 3,890
- 8,647
Bado sijaona sababu ya msingi kabisa ya kuwaondoa wamachinga barabarani.
Kama wanaziba njia na wanakaa kwenye mifereji ilo linazungumzika na inawezekana kuwasogeza sio kuwafukuza kama mbwa. Hii nchi ni ya kila mmoja.
Kuna watu nimeona wanasema nchi za weupe hakuna wamachinga....nawaambia watembee waone kuna nchi wamachinga mpaka kwenye reli.
Kuna watu wanajiona wameyaweza maisha..
Ana cheo, ana gari ana nyumba familia inakula vizuri n.k unategemea afanye nini juu ya wamachinga?
Atakwambia wamachinga wanaziba barabara, wanaharibu taswira ya mji n.k
hakuna nchi ambayo haina wamachinga duniani hapa...
Ila hapa kwetu kunaviongozi wapumbavu hivi kwao machinga ni kero!