Aramun
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 461
- 2,213
Hii trend sasa ni rasmi katika miji yote. 99% ya migahawa au cafe au vyovyote vile utakavyoiita, kwa nje lazima waweke na banda la chipsi.
Na 90% ya wateja utawakuta wanakula chipsi. Na wakila chipsi lazima wanunue na kinywaji kama soda cha kusukumia hizo chipsi, kama ujuavyo chipsi ni viazi na vina tendecy ya kukwama kooni.
Mimi sina neno na ulaji wenu, ila ndani ya miaka 10 ijayo tujiandae kuteseka na magonjwa yasiyoambukiza ambayo ni mabaya kushinda yanayoambukiza.
Sababu kuu ni kwamba mijini wengi wetu hatufanyi manual works, tunafanya tu light duties ambazo hazifanyi kuyatumia hayo mafuta tunayoyala kwa wingi. Mwisho wa siku yanakundikana mwilini na kuziba mishipa ya damu, hii inapelekea moyo kupata shida ya kusukuma damu na kuishia kwenye magonjwa kama Presha ya Kupanda na Kisukari.
Kwa sasa ukienda hospitali ya taifa Muhimbili, kwa siku hukosi wagonjwa wapya wa Kiharusi (Stroke) kuanzia 5 na kuendelea. Jiji la Dar miaka 10 kila nyumba itakuwa na atleast mwanafamilia mwenye magonjwa yasiyoambukiza hasa Pressure na Kisukari.
Chukua hatua, uamuzi ni wako kusuka au kunyoa.