United ya Ferguson
JF-Expert Member
- Oct 29, 2021
- 3,132
- 6,353
wew kwenu umejenga kitu Gani acha umasikin wa akili yani mtu ashindwe tumia pesa yake kisa wew umejenga Nyumba kijijini kwenu Tumia pesa ikuzoee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuwa na kwake
Vizuri sana kwa kuclear mambo, lakini kukumbushana ndio ubinadamu. Hata Enzi hizo ambazo hakukuwa na pesa nyingi, wakina (Mogella golden boy) walijenga na kufungua miradi kibao, wakati wenzao (hamna haja ya kuwataja) pesa zao ziliishia bar na machangudoa kila kona.Saidi Ntibazonkiza amecheza ligi ya Uholanzi (Eredivisie) kwa misimu minne yaani 2006 -2009 akiwa na Nijmegen Eendracht Combinatie (NEC), Pia amewahi kucheza ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) na timu ya Caen msimu mmoja 2015/16 kabla ya hapo alikuwa ligi kuu ya Uturuki (Super Lig) msimu wa 2014/15 na Akhisarspor Kulübü.
Jaribu kuangalia vizuri hii career yake utalinganisha na mchezaji aliyekuwa analipwa Tshs. 30M as a signing fee miaka hiyo? Mishahara mikubwa mikubwa kidogo ililetwa na Yusuf Manji tena miaka chini ya 2012 Simba na Yanga Tshs. 5M ulikuwa mshahara mkubwa sana. Hapo unampa mchezaji na kagari ka Tshs. 20M plus signing fee Tshs. 25M. Mshahara kwa mwezi Tshs. 3M.
Makaveli kiwanja unarusha jiwe litakapodondokea ndo kiwanja chako kutoka uliposimama"pesa yake matumizi, hakuna elfu 10 iliyoandikwa ni ya mfuko wa cement wala tofali"😂
"Hakujenga baba kipindi cement mfuko sh 2, kiwanja unajikatia, nijenge mie cement 18000" 😂😂
"Tumia pesa ikuzoee" 😂
"Dunia tunaoita, sijengi, nitajengewa nyumba yangu ya milele nandugu jamaa na marafiki "
🤣😂😂
Marehemu asemwi vibaya ila huyu mwamba alinifurahisha sana.
Mmoja kati ya viungo bora kabisa wa enzi zake,siku moja kabla ya kifo chake,Isnsil Aden Rage akimpatia milioni zaidi ya kumi kama sehemu ya ada ya usajili wake.
Mafisango akaita marafiki zake wakaitumbua aswaa,ilikuwa ni kuhama bar tu mara mikocheni mara masaki mara kinondoni,mara paaa ajaki hii hapa
Tukaenda msibani aisee ni uswazi kama Tandale hakuna hata pa kufunga hema.
Naandika haya nikiwa bujumbura baada ya kuonyeshwa mjengo wa yule mzee wetu Saidoo,ni mjengo hata huko Tanzania hakuna mchezaji au celebrity anaweza kuumiliki.
Ajabu hawa hawa wanaosema marehemu hasemwi vibaya ndio hao hao wanaomsema vibaya Yuda Iskarioti.Kama marehemu alikuwa mjinga mjinga lazima asemwe ili liwe fundisho kwa wengine
Na Mungu sio bibi yao.Na hawataki kukuona ukila na kunywa vizuri ,wanataka kukuona unalialia na kuhuzunika muda wote
Sawa sawa..Kwa hiyo milioni kumi ndio angejenga hekalu kama la Saido? Wala sishangai hayo ndio maisha ya Wakongo wengi,hata ukienda Kinshasa au mji wowote mkubwa wa Kongo ukikutana na Mkongo njiani au sehemu ya starehe jinsi alivyovaa na starehe afanyayo halafu ukienda kuona anapoishi ni mbingu na ardhi.
Kuna nchi za west africa pia misiba yao inashangazaMafisango alizikwa kwao Goma ..misiba ya wakongo unaeza sema wanakufuru kumbe ndio msiba huo...jeneza la mafisango lilikua kuna muda linawekwa chini watu wanacheza sebene kisha linabebwa tena yaani mpk kufika makuburi ni vurugu tu ...
Msiba ulikuwa wakushangaza kwa watanzania wachache waliokua msibani
Ni kweli west Africa nao wako hivyo...ila drc km ni mgeni unaeza sema hawa wanakufuru au walikuwa na ugomvi na marehemu..masebene mwanzo mwishoKuna nchi za west africa pia misiba yao inashangaza
NAKAZIAAjabu hawa hawa wanaosema marehemu hasemwi vibaya ndio hao hao wanaomsema vibaya Yuda Iskarioti.
Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana.
Au unamzungumzia yule mwamba aliyekuwa akiishi magomeni kimamba????Vizuri sana kwa kuclear mambo, lakini kukumbushana ndio ubinadamu. Hata Enzi hizo ambazo hakukuwa na pesa nyingi, wakina (Mogella golden boy) walijenga na kufungua miradi kibao, wakati wenzao (hamna haja ya kuwataja) pesa zao ziliishia bar na machangudoa kila kona.
Kuna mchezaji ambae alikuwa mtu wa karibu sana, na ambae alifanyikiwa kucheza kwenye timu ya Yanga, huyu bwana alikuwa anaenda kwa wale wahindi wa timu nakulalamika kwamba anajenga huko kwao na anahitaji msaada. Zaidi ya mara tatu nomeshuhudia vifaa vya ujenzi wa nyumba yake vikitiwa ndani ya behewa reli ya kati (msaada kutoka kwa hao matajiri) lakini kabla vifaa havijafika huko kwao, mnunuzi kaishapatikana hapohapo Dar, vikifika kule, anakabidhiwa pesa yake hapo Kinondoni, vifaa vya ujenzi vinakwenda upande mwingine. Hakuna kiwanja wala banda. Anashinda zake Bar mpaka hela zimuishie. Msimu wa ligi ukianza anaanza tena.
Alhamdulillahi, alifanyikiwa kujenga baada ya kupata mwanamke wa kimanyema ambae hakuwa anataka mchezo. Alimshika jamaa masikio kama Sungura mpaka wakafanyikiwa kujenga. Vinginevyo, sijui angekuwa wapi sasa hivi.
Unaweza kujenga na kile kidogo ulichonacho, lakini wakati mwingine mtu anahitaji msaada wa ziada ili kubadilisha muelekeo na vipaumbele.
Ya pilau 🤣🤣🤣Majungu tuu