Siku moja kabla ya kifo chake Mafisango aliteketeza milioni 10 kwa starehe,cha ajabu hakuwa amejenga kwao

Vizuri sana kwa kuclear mambo, lakini kukumbushana ndio ubinadamu. Hata Enzi hizo ambazo hakukuwa na pesa nyingi, wakina (Mogella golden boy) walijenga na kufungua miradi kibao, wakati wenzao (hamna haja ya kuwataja) pesa zao ziliishia bar na machangudoa kila kona.

Kuna mchezaji ambae alikuwa mtu wa karibu sana, na ambae alifanyikiwa kucheza kwenye timu ya Yanga, huyu bwana alikuwa anaenda kwa wale wahindi wa timu nakulalamika kwamba anajenga huko kwao na anahitaji msaada. Zaidi ya mara tatu nomeshuhudia vifaa vya ujenzi wa nyumba yake vikitiwa ndani ya behewa reli ya kati (msaada kutoka kwa hao matajiri) lakini kabla vifaa havijafika huko kwao, mnunuzi kaishapatikana hapohapo Dar, vikifika kule, anakabidhiwa pesa yake hapo Kinondoni, vifaa vya ujenzi vinakwenda upande mwingine. Hakuna kiwanja wala banda. Anashinda zake Bar mpaka hela zimuishie. Msimu wa ligi ukianza anaanza tena.

Alhamdulillahi, alifanyikiwa kujenga baada ya kupata mwanamke wa kimanyema ambae hakuwa anataka mchezo. Alimshika jamaa masikio kama Sungura mpaka wakafanyikiwa kujenga. Vinginevyo, sijui angekuwa wapi sasa hivi.

Unaweza kujenga na kile kidogo ulichonacho, lakini wakati mwingine mtu anahitaji msaada wa ziada ili kubadilisha muelekeo na vipaumbele.
 
Makaveli kiwanja unarusha jiwe litakapodondokea ndo kiwanja chako kutoka uliposimama
 

Mafisango hakuagwa uswahilini

Wewe ni MUONGO!

Japo ni kweli wachezaji wa zamani na hata wa sasa wanakufa snaa masikini after career path yao

Christopher Alex Massawe moja ya beki safi sana ndani ya SSC aliyewatoa zamalek long time kitambo. Jamaa alikufa hata pesa ya jeneza ilipatikana kwa shida sana

Hakuna kiongozi wa SSC aliyehuhudhuria maziko yake

Mpira wa Tanzania ni umasikin tu
 
Sawa sawa..
 
Mafisango alizikwa kwao Goma ..misiba ya wakongo unaeza sema wanakufuru kumbe ndio msiba huo...jeneza la mafisango lilikua kuna muda linawekwa chini watu wanacheza sebene kisha linabebwa tena yaani mpk kufika makuburi ni vurugu tu ...

Msiba ulikuwa wakushangaza kwa watanzania wachache waliokua msibani
 
Kuna nchi za west africa pia misiba yao inashangaza
 
Au unamzungumzia yule mwamba aliyekuwa akiishi magomeni kimamba????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…