Siku Nilipoiona Simu Kwa Mara ya Kwanza Odeon Cinema 1955 au 1956 au Nyuma ya Hapo Kidogo Sijavuka Miaka 4

Umuhimu wa hii khabari upo hapo
Kolola,
Kleist Sykes...

Kleist Sykes ni mmoja katika wazalendo ambae historia yake imo ndani ya Dictionary of African Biography (DAB).

Yeye ni muasisi wa African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.

DAB ni volumes 6 na ulikuwa mradi wa Oxford University Press, New York na Harvard.



 
Afrika ya Kusini au Tanganyika?
 
Njabu...
Mimi nitaeleza niyajuayo na kuyakumbuka wako wengi wananiamini.

Lakini ikiwa wewe utaniona mimi muongo hiyo ni bahati mbaya.
Mtoto wa miaka 3 hadi 4 hawezi kukumbuka kupelekwa clinic halafu akaona kitu ambacho SIYO visually appealing au special kimaumbo au kivyovyote kama simu ya mezani, halafu aliweke tukio hili kwenye long term memory yake.
 
Mtoto wa miaka 3 hadi 4 hawezi kukumbuka kupelekwa clinic halafu akaona kitu ambacho SIYO visually appealing au special kimaumbo au kivyovyote kama simu ya mezani, halafu aliweke tukio hili kwenye long term memory yake.
Ngabu...
Nilikuwa napitia na mhariri mswada wa kitabu nilichoandika na kuna mahali nimeeleza kisa nilichokiona nikiwa mtoto wa miaka 4.

Yule mhariri akawa haamini kama ulivyokuwa huamini wewe.

Nikamhadithia mambo mengine niliyoshuhudia.

Akazidi kushangaa.

Princes Magret alipokuja Tanganyika 1956 nimeuona msafara wake ukipita Kitchwele Street.

Nakumbuka mpaka leo na wapi tulisimama.

Tulisimama Mtaa wa Sikukuu na Kitchwele nje ya duka la Toti.

Natafuta picha nitaiweka hapa In Shaa Allah.

Nilikuwa na miaka minne.
 
Itabido jamii forum ijivunie sana wewe kuwa member active kabisa tena na umri huo..
Hongera sana.
 
Ulikatazwa kwenu kuwa na ukaribu na watu wasiyo wa imani yako katika makuzi, au hukumbuki kuwahi kuwa na urafiki na mtu yoyote asiye wa imani yako? Inakuwaje kwa mtu ambaye umesoma shule za kanisa siyo chini ya mbili? Hiyo ya msafara wa Dada ws Malkia mtoto anaweza kuweka kwenye long term memory sababu ni tukio la kipekee kwa maana ya umati kukusanyika pembezoni mwa barabara, magari mengi na Mhusika Mkuu kuwa Mzungu wa kike. Naamini hata ingekuwa Ulaya enzi hizo watoto wa umri huo wengi wana kumbukimbu ya kumtupia macho kwa mara yao watu wenye ngozi nyeusi.
 
Sure hata mm kuna matukio nakumbuka nikiwa na miaka 3 au 4.
Tena ni matukio ambayo sisahau kabisa.
 
Ngabu...
Nashindwa kukujibu kwa kuwa sijajua nini kinakughadhibisha.
Kuwa ungependa kusoma kitu gani kutoka kwangu ili ufurahi.
 
Waanzilishi wa Saigon walikuwa Waarabu au waingereza?
 
Waanzilishi wa Saigon walikuwa Waarabu au waingereza?
Proved,
Saigon ilikuwa ikiitwa Everton 1966.
Nina umri wa miaka 14 club ya mpira ya watoto wadogo wa Kariakoo.

Hakuna usajili wa club.

Ni club ya watoto shule ya msingi tukisoma Mnazi Mmoja, Mchikichini na Al Jamiatul Islamiyya Muslim School na shule nyingine za Dar es Salaam.

Tulikuwa watoto wa Kiafrika ndiyo tulikuwa wengi na watotonwachache wa Kiarabu kama Salum " Gordon Banks" Khalil, Rashid Vava, Ali, na Rafiq na Bulji hawa wawili walikuwa Wahindi.

Chico na Vava hawa unaouna Uarabu kwa mbali.
Gordon Banks yeye Uarabu ulikuwa peupe kabisa.

1967 ikageuka kuwa Saigon hadi leo mimi nina miaka 70.

Rafiq baba yake alikuwa na hoteli maarufu Royal Hotel wakijulikana kwa upishi wa biriani.
 
Alipokuwa na miaka 4 kakumbuka hadi alipokatiza mtaa wa Kleist Sykes SIKU MOJA?!! Mitaa yote ya Kariakoo hadi kufika Odeon Cinema ya wakati huo kaicha.
Njabu...
NImezaliwa Mtaa wa KIpata (Sasa Kleist Sykes).

Nikitoka nyumbani kwetu kuelekea Mnazi Mmoja nakata Mtaa wa Swahili kushotom kuna nyumba ya Hassan Machakaomo.

Hassan Machakaomo baba yake Machakaomo alikuwa Mzulu aliyekuja German Ostafrika na Sykes Mbuwane na akina Plantan.

Machakaomo alikuwa mmoja wa viongozi wa Young Africans mwaka wa 1948.

Nakuwekea picha ya viongozi wa Young Africans wakiwa na Abeid Amani Karume na Mtoro Rehani mwaka wa 1948.

Hassan Machakaomo ni huyo wa kwanza aliyekaa chini.
Mtafute Karume.

Nakatiza Mtaa wa Sikukuu kulia kwenye kona na Kipata kuna nyumba ya Clement Mohamed Mtamila aluyekuwa Secretary wa TAA President akiwa Mwalimu Thomas Plantan.

Uongozi huu ndiyo uliopinduliwana Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kwa msaada wa Schneider Abdillah Plantan wakaingia madarakani Dr. Vedasto Kyaruzi kama President na Abdul Sykes Secretary 1950.

Baada ya hapo navuka Mtaa wa Livingstone kulia ndipo ilipokuwa studio ya Mohamed Sheba aliyepiga picha nyingi sana za siku za mwanzo za TANU na kumpiga picha Julius Nyerere.

Baadhi ya picha hizi zipo katika Maktaba yangu kwa hisani ya mwanae Mbaraka Shebe.

Sasa nafika mwisho wa Kipata kushoto kuna nyumba ya Sheikh Abdallah Simba Liwali wa Songea na rafiki ya babu yangu, Salum Abdallah.

Babu yangu kaishi nyumba hii hadi 1947 alipohamia Tabora.
Mkabala wa nyumba hii ni nyumba ya Kleist Sykes.

Naingia New Street (Sasa Lumumba Avenue).
Naijua Gerezani na wakazi wake.

Hii ndiyo ilikuwa dunia yangu.


 
kumbe mzee wangu mtu wa bara wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…