Elections 2015 Siku tano za kampeni: Chokochoko za CCM, serikali yake na vyombo vya ulinzi

Elections 2015 Siku tano za kampeni: Chokochoko za CCM, serikali yake na vyombo vya ulinzi

Ninacho jua hakuna binadamu duniani anaependa kuibiwa kwa hiyo ccm wakiiba kura tu tunakinukisha
 
Mamlaka ya hali ya hewa inaweza kuja na kituko kingine.

Kutokana na kuwepo na joto kubwa katika bahari ya Mediteranian ambayo itasababisha mvua za El Nino wagombea uRais watatakiwa kuomba kibali Mamlaka ya hali ya hewa kabla ya kufanya mikutano yao ili kuondoa uwezekano wa kutokea madhara yatakayosababishwa na mvua za El Nino.


Hapa umeua... haaaaa...daaah...!!!

Ukawa, wakiomba mkutano wataambiwa MVUA KUBWA sana ya MAWE MAKUBWA KAMA TOFALI YA AJABU KUNYESHA NA WATU WAJIFICHE majumbani...
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Wamaweza Mwishowe Wakasema Lowassa Ana Ebola.
 
Gadafi aliwaita walibya mende yaani kokirochi...ila hao mende hadi leo wapo ila yeye hayupo
 
Mamlaka ya hali ya hewa inaweza kuja na kituko kingine.

Kutokana na kuwepo na joto kubwa katika bahari ya Mediteranian ambayo itasababisha mvua za El Nino wagombea uRais watatakiwa kuomba kibali Mamlaka ya hali ya hewa kabla ya kufanya mikutano yao ili kuondoa uwezekano wa kutokea madhara yatakayosababishwa na mvua za El Nino.

haa haa ni kweli mkuu. safar hii ukawa watapambana na matawi yote ya ccm toka polis,tbc,tanesco, TCRA na hata TCCA..
 
huku uraiani habari ni ccm kumwogopa lowasa mpaka kuanza kutumia taasisi za serikali kama Mamlaka ya usafiri wa anga.
 
Pema usijapopema, ukipema si pema tena ujue......Wenyewe watakuwa kwenye makasri yao South Africa, Dubai na London wakati huo waatu wanachinjana hovyo Bongo. Tusisahau kwamba wanajeshi nao ni watoto wetu, kaka zetu, vijana wetu, dada zetu, wajomba zetu, nao wana mapenzi na wagombea tofauti na mapenzi kwa vyama tofauti. Utiifu wao nao una kikomo cha kibinadamu. Moto ni mzuri ukiutumia kwa busara lakini unaua usipokuwa mwangalifu nao. Gari lako linaweza kukuua kirahisi tu. Neea ya Mn iwe pamoja nai sasa na hata milee na miele, men.
 
"When you go to fight for truth and freedom don't wear your best trousers"
 
Hapa umeua... haaaaa...daaah...!!!

Ukawa, wakiomba mkutano wataambiwa MVUA KUBWA sana ya MAWE MAKUBWA KAMA TOFALI YA AJABU KUNYESHA NA WATU WAJIFICHE majumbani...

Na hatoruhusiwa mtu kutoka ile ukitoka tu unachezea virungu kwa kisingizio utasababishia serikali hasara kwa kuhudumia wagonjwa na vifo visio na lazima maana tayari taarifa ya janga imeshatolewa.
 
Those are ccm symptoms, soon will die and none should make its history!

CCM inaangushwa na wanaccm wenyewe wala si UKAWA!
 
serikali ipi hii ya raisi wake anahongwa suti pair tano kwa kubadilishana na loliondo hii ya kumaliza asilimia sitini tembo kwi kwi itaipata safari hii na nguvu ya umma

Acha kutukumbusha machungu ya suti! Wapo watu sasa hivi bado wanaumia kwa maamuzi yale wakati suti alizo hongwa jamaa zimeshacha kaa
 
SIKU TANO ZA KAMPENI: YAFUATAYO YANAONESHA DHAHIRI KUWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZINASHIRIKIANA NA CCM KUJARIBU KUHARIBU UCHAGUZI HUU;


1. Kumzuia mgombea urais wa CHADEMA/UKAWA kuhudhuria msibani eti kwa sababu amesindikizwa na watu, kana kwamba watu walewale kwa idadi ileile wangekwenda wenyewe wangeleta madhara yoyote. Najiuliza tu, ingekuwaje mgombea na watu wale wangelazimisha kwenda msibani; JIBU: Mapambano na Polisi, mgombea kukamatwa na kufunguliwa kesi, wafuasi kujeruhiwa kwa risasi, kuuawa ama kukamatwa.

2. Kupiga Marufuku maandamano na mbwembwe za kuwasindikiza wagombea kurejesha fomu. Hili lilifanywa mara baada ya Magufuli na Lowassa kwenda kwa maandamano lakini yale ya Lowassa yakionekana kuwa na maelfu mengi ya watu zaidi kuliko ya magufuli. Lakini pamoja na marufuku hiyo majuzi nimejionea wafuasi wa CCM wakiandamana kutoka Manzese hadi Jangwani wakiwa na MASABURI, bila polisi kuwazuia.

3. Kuzuia mgombea wa UKAWA/CHADEMA kufanya ziara maalum za kushtukiza kuwatembelea wananchi wa kawaida. Hizi zinapigwa marufuku kwa mgombea huyu wakati wale wa CCM wakifanya watakavyo. Mfano ni Bi. Samia Suluhu alivyoonekana Moshi akiacha ratiba ya ziara na kutembelea raia mtaani bila kukatazwa na Polisi.

4. Kuzuia UKAWA kufanya mkutano wake wa uzinduzi Uwanja wa Taifa na hata UKAWA ilipoamua kufanyia mkutano huo katika viwanja wa JANGWANI umezuiwa na Manispaa ya Ilala nadhani kwa shinikizo la CCM chini ya sababu dhaifu sana kwamba kuna watu wameshaukodi, Ni halmshauri ipi hivi sasa ambayo ina-PRIORITIZE shughuli zingine kwenye viwanja vikubwa wakati vyama vya siasa viko kwenye uchaguzi mkuu jambo ambalo ni kipaumbele cha taifa kwa sasa?

5. CCM kufanya mkutano wake wa uzinduzi hadi saa 12.38 jioni tena mbele ya Mkuu wa nchi na viongozi wote wa serikali wakati wanajua fika kuwa sheria inawataka kufunga mkutano saa 12.00 jioni. Kwamba CCM na inavionesha vyama vingine kuwa iko juu ya sheria na kwamba wengine wakiiga watajiju. Na baada ya kupitisha muda huo CCM inamshinikiza Mkurugenzi wa manispaa ya ILALA aandike barua NEC kuijulisha kuwa ni yeye ndiye alielekeza mkutano uendelee hadi muda huo (very illogical reason).

6. Rais mstaafu wa awamu ya 3 Benjamin William Mkapa kusimama hadharani na kuwatukana wapinzani kuwa ni "MALOFA na WAPUMBAFU". Mpumbavu ni neno kali na lina maana ya "juha", "zuzu", "mtu asiyejielewa", "-----", "----", n.k. Wakati Mkapa akitukana hivyo hadharani na kuachwa juu ya Sheria, Lawrence Masha ambaye ni mwana UKAWA (hivi sasa) lakini zamani akiwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania, yeye amekamatwa na kuwekwa rumande na kunyimwa dhamana (inacheleweshwa kimakusudi) kwa "kosa" la kumtukana askari polisi (wengi kama sikosei) kwamba ni "washenzi", "wasio na shukrani na wasio na dini". Kwamba kwa tafsiri ya CCM na serikali yake pamoja na vyombo vinavyosimamia sheria (POLISI), neno "Upumbavu na Ulofa" siyo tusi lakini neno "Ushenzi na Kutokuwa na shukrani" ni tusi baya sana.
Hayo mambo sita niliyoyataja na mengine kadhaa ni dalili tosha kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaweza kuishia mahali pabaya. Hadi sasa sijaona CHOKOCHOKO kutoka upande wa UKAWA, hii ina maana kwamba hizi za CCM, VYOMBO VYA DOLA NA MAMLAKA ZA SERIKALI zikiendelea na zikawa zinahujumu kwa dhahiri maslahi ya UPINZANI na UKAWA, lolote lile linaweza kutokea.
 
Ni kweli kuwa imetokea vita kali sana kati ya M4C na 4U Movement baada ya Lowassa kuelekeza rasilimaliwatu ya M4C iwekeze zaidi kwenye kujenga Red Brigade na kuacha mikakati ya kampeni kufanywa na wazoefu 4U Movement?
 
vita vya kupigania haki poa sana.....
 
Dalili za chama cha Mapinduzi kusababisha vurugu katika uchaguzi mkuu zimeanza kuonekana mapema kutokana Na vikwazo vinavyowekwa Na watendaji Wa serikali.Vikwazo hivyo in pamoja Na kuvizuia vyama vya Upinzani kufanya mikutano yao katika viwanja vya Umma.Tunaishauri CCM kwa namna moja au nyingine iache kutumia mbinu hizi chafu kwa wananchi wakikosa uvumilivu watataka kuzizuia kwa nguvu Na kusabisha uvunjifu Wa amani.Ni vema kampeni zikaendelea bila hujuma zozote.
 
Back
Top Bottom