Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaomba msaada sio!
Hata limbwata ni nyama pia inahusika.Ushuzi wa bata huu
Wahi hospitalini ukatibiweNi upumbavu Kwa wapoteao, ila ni msaada mkubwa Kwa wanaoonewa na kufungwa na shetani.
Nilikuwa nasoma kwa utuli na umakini mkubwa lakini nilipofika kwenye macho ya roho basi nikaanza kusoma kwa kudharauSalaam, shalom!!
Nitaeleza Kwa ufupi.
Siku Moja mpendwa wetu mmoja alifiwa na ndugu yake Kijiji fulani, tukalazimika kusafiri Toka Kijiji kimoja kwenda Kijiji kingine Kwa ajili ya maziko.
Tulipofika, kilikaa kikao na kuazimia mbuzi wawili wachinjwe Ili ipatikane nyama ya kulika msibani Kwa siku hiyo.
Mbuzi walichinjwa na kuandaliwa vyema muda ya asubuhi, ilipofika mchana, kililetwa chakula na watu wakala mchana na mbuzi alikuwa safi kabisa.
Sasa baada ya kuzika, nyama iliyobaki ilitunzwa Ili iliwe jioni siku hiyo,
Utata ukaja ilipofika jioni saa 12 wakati wa chakula,
Nilipokwenda kwenye pitapita ZANGU kama mmoja wa viongozi wa msafara, nilipata hamaki kubwa kuona yafuatayo,
Nyama Ile ya mbuzi sufuriani ilionekana kubadilika RANGI na kuonekana Kwa RANGI ya Bluu, na ilionekana kuota ukungu na kuwa kama nyama iliyooza na kukaa siku nyingi ni kama mzoga vile.
Nilipoona Yale, niliwaita ndugu nilioongozana nao msibani na kuwaonya kuwa, yule Si mbuzi tuliyekula mchana, niliwambia nyama imebadilishwa, na Si njema Kwa matumizi ya chakula.
Sasa Kwa kuwa wengi wao hawakuwa na macho ya Roho, walirudi kuiangalia nyama na kuiona Iko sawa na wakapuuza ujumbe na maonyo Yale na walikula chakula na nyama Ile jioni Ile.
Kilichofuata baada ya robo sana hivi, umati Ule uligeuka tafrani, tumbo la kuhara liliwashika wote waliokula nyama Ile, watu waliharisha mfululizo na Kwakuwa mazingira ya vijijini hakuna vyoo vya kutosha, uharibifu wa mazingira ulifanyika vichakani,
Watu wale pale kijijini waliokula nyama Ile waliendesha Kwa usiku kucha, na kesho yake, Kila Mmoja alijutia uamuzi mbovu wa kutosikia maonyo ya mtumishi wa Mungu. Baadae ilikuja fahamika kuwa kundi la wachawi mahasimu waliamua kuchukua nyama Ile nzuri wakaila wao na kuleta mzoga Ili kuwakomoa wafiwa Kwa faida zao kichawi.
FUNZO.
1. Makinika na ulaji wa nyama kwenye misiba, wengi hutafutwa kuangamizwa kichawi katika Makusanyiko ya aina Ile.
2. Ombea maji na chakula chochote kabla ya kula Kwa Imani, na ukisita kula usilazimishe.
3. Pata macho ya rohoni Ili uone sawasawa, uepuke hatari mbeleni.
Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako, fuatisha Sala hii,
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN.
Source: Mtumishi wa Mungu ( Jina linahifadhiwa).
Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, usije ukafanana naye.Wahi hospitalini ukatibiwe
Sio msibani tu hata ugeniniNajua unapenda nyama,
Nyama za msibani achana nazo🙏
Sasa unashangaa nini kuhusu macho ya Roho ilhali Kila ikifika usiku unaota ndoto Ukiwa umefumba macho,Nilikuwa nasoma kwa utuli na umakini mkubwa lakini nilipofika kwenye macho ya roho basi nikaanza kusoma kwa kudharau
Wasiokuelewa waache usijibuzane naoUsimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, usije ukafanana naye.
Ukimya nao ni jibu.
Kwaheri.
Mkuu hao wasiokuelewa waache usijibuzane nao tupo tuliokumbwa na hio mikasa tumekuelewa vizuriSasa unashangaa nini kuhusu macho ya Roho ilhali Kila ikifika usiku unaota ndoto Ukiwa umefumba macho,
Hujiulizi ni macho Gani hutumika ndotoni ilhali macho ya MWILI umefumba USINGIZIni?
Sasa kwa kuwa ugenini huwezi kataa chakula,Sio msibani tu hata ugenini
Mkuu una safari ndefu ya kusaka pesa nyingi uachane na hizo blablaa.Sasa hutakiwi kuleta mambo ya kisaikolojia ilhali mtumishi ameona na kuthibitishiwa kuwa ni chakula kichafu.
Labda tatizo lako Unadhani watumishi wa Mungu hawawezi kubaini Siri na michezo ya wachawi.
Weka kisa kimoja Kwa uelewa wa wengine, Si lazima kutaka eneo au Majina ya watu.Mkuu hao wasiokuelewa waache usijibuzane nao tupo tuliokumbwa na hio mikasa tumekuelewa vizuri
Ugenini Mimi nikiona chakula sikielewi Sili wale wenyewe nimefanya mara kibao sana nafsi yangu ikiniambia usile Sili nikila tu linanikuta jambo nikisema Sili siliSasa kwa kuwa ugenini huwezi kataa chakula,
Kitakase Kwa Jina la YESU Kisha kula bila shida, hutopata madhara yoyote, kitini macho hakitafanyika ukiomba.
Sasa wapi umeona Kuna Mahali nimemuomba mtu pesa?Mkuu una safari ndefu ya kusaka pesa nyingi uachane na hizo blablaa.
Siwezi kuweka hapa hii ni public ID wananijua kibao humu personally sio fake IDWeka kisa kimoja Kwa uelewa wa wengine, Si lazima kutaka eneo au Majina ya watu.
Karibu.🙏
WANADAMU ni viumbe wenye Hila sana.Ugenini Mimi nikiona chakula sikielewi Sili wale wenyewe nimefanya mara kibao sana nafsi yangu ikiniambia usile Sili nikila tu linanikuta jambo nikisema Sili sili
Ok ndugu.🙏Siwezi kuweka hapa hii ni public ID wananijua kibao humu personally sio fake ID
Sijasema umeomba au pm mkuu huwa hakuna usiku kwanguSasa wapi umeona Kuna Mahali nimemuomba mtu pesa?
Na lini uliona hata PM yangu wazi?
Usilolijua ni usiku wa Giza Totoro.