Until_The_End
JF-Expert Member
- Nov 21, 2020
- 1,456
- 2,202
Jiunge na hawa jamaa unajifunza mwenyewe ila wata ku guide kwa kukupa resources na Task mpaka utakapo maliza.UPDATE:
Jana usiku nilichapa code za calculator. Code ya mwanzo ilikuwa user anachagua kama anataka kuadd, ku substract, kudevide, au ku multiply, so namba atakazoweka baada yapo zinakuwa calculated kutokana na alichochagua mwanzo ila mwisho inamuuliza kama anataka kuendela akijibu yes, inarudi kumuuliza add, sub, mult, div anachagua tena.
Usiku wakati nimelala nikawaza kwanini nisitengeneze code ya calculator ambayo inapokea sign za hesabu pia baadala ya kumuuliza mtumiaji mwanzoni.
So, nimeamka asubuhi nilikuwa tayari nishaifikiria, nikaamka naichapa japo nimepata changamoto mbili tatu ila imerun japo bado inakasoro moja. Ikisharun ikakuuliza kama wataka kuendela, ukajibu yes, unaendelea ila baada ya hapo haikuulizi tena: Ni wapi nimekosea? kali linux Allency Mjamaa1
CODE:
def input_figure():
number_1 = int(input('Enter number 1: '))
sign = input('Enter mathematical operation: ')
number_2 = int(input('Enter number 2: '))
return number_1, sign, number_2
def add_fun():
a, b, c = input_figure()
if b == '+':
print('sum:', a + c)
elif b == '*':
print('prod:', a * c)
elif b == '-':
print('diff:', a - c)
elif b == '/':
if c != 0:
print('div:', a / c)
else:
print('Cannot divide by zero!')
else:
print('Invalid mathematical operation!')
choice = input('Continue? (Yes/No): ').strip().lower()
if choice == 'yes':
add_fun()
else:
print('Nice day!')
add_fun()
*******************************************************************************************************************
Mimi ni mpenzi wa coding sana. Nimeamua nianze kusoma programming na nimechagua kuanza na python nipambane nayo hata mwaka mzima niifanyie kazi kabla ya kuamia kwingine baada ya kuitumia tumia.
Stratergy yangu ni kusoma kidogo kidogo na kuelewa vitu kisha kuvifanyia mazoezi. Kwa sababu nina majukumu na nakuwa busy sana, nimeamua kila siku nitatenga saa 2 hadi 3.
Leo ni siku ya tatu narudia kufanyia mazoezi niliyoyasoma kabla ya kusonga ili nijipe muda kuelewa zaidi kabla ya kuongeza mambo: Nimeandika code kadhaa ikiwa mojawapo ni hii niliyopaste hapa ambayo ni mfano tu wa kujifunza. Code ninazoandika si kutoka sehemu yoyote ila ninawaza jambo na kujaribu kuliandikia code nione kama litafanya kazi kama nilivyotaraji:
Natumai wababe humu mtanipatia mwongozo pia.
Hii ni programu, mtumiaji akifungia itamwomba user na password. Lazima username na password ifanane na hizo nilizoziweka kwenye programu (ni kwa majaribio tu najua in real life haziwezi kuwa hapo).
Kama kimoja kisipofanana itamrudisha aweke upya (nataka niendelee iwapo atajaribu mara 3 basi ijifunge kwa muda)
Akipatia, itampeleka kwenye sehemu ya kuweka matokeo. Ambapo kama average itazidi 60, itamtaja mwanafunzi kwa jina na kusema amefaulu kwa wastani husika, ikiwa chini, itamtaja kwa jina na kusema hakufaulu kwa wastani husika. Kisha itamuuliza kama anataka kuweka matokeo ya mwanafunzi mwingine, akisema ndiyo itarudia tena kumdai jina la mwanafunzi, darasa, na matokeo ya kila kipindi. Akisema hapana, basi itamwambia kwaheri na kuishia hapo.
*** Bahati mbaya nikiipost hapa inaondoa Indentation sijui shida nini naona codes zote zinaanzia kwenye level mmoja.
def welcome():
print('KARIBU KATIKA UKURASA WA MATOKEO')
def invalid():
print('UMEKOSEA! JARIBU TENA')
def login_message():
print('Inaingia...')
def credentials():
userName = 'mway09'
passWord = '1995'
return userName, passWord
def login():
welcome()
userName, passWord = credentials()
while True:
username = input('Weka jina: ')
password = input('Weka nenosiri: ')
if username == userName and password == passWord:
login_message()
break
else:
invalid()
login()
def welcome2():
print('MATOKEO PLATFORM')
def add_results():
welcome2()
while True:
std_name = input('Jina la mwanafunzi: ')
std_class = input('Darasa la mwanafunzi: ')
a = int(input('Historia: '))
b = int(input('Jiografia: '))
c = int(input('Hisabati: '))
d = int(input('Kiingereza: '))
y = a + b + c + d
average_score = y / 4
if average_score >= 60:
print(std_name + ' wa darasa la ' + std_class + ' amefaulu mtihani kwa wastani wa ' + str(average_score) + '.')
else:
print(std_name + ' wa darasa la ' + std_class + ' ameshindwa mtihani kwa wastani wa ' + str(average_score) + '.')
break
choice = input("Ungependa kuongeza mwanafunzi mwingine? (ndiyo/hapana): ").strip().lower()
if choice == "ndiyo":
add_results()
else:
print('Kwaheri!')
break
add_results()
Ukipenda jiunge program ya Software Engineer kwa mwaka mmoja bado wana sajili.
ALX Africa - Power Your Future in Tech
ALX is a leading technology training provider, built to accelerate the careers of young Africans through the technology and professional skills that enable them to thrive in the digital economy.
www.alxafrica.com