Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Nakumbuka wakati tupo form 2 pale azaboy...walikuja wageni wazungu....sasa si unajua wazee tupo Chimbo...sasa kuna madogo walikuwa kama wamepishana viswahili....sasa wakati wanarushiana maneno...Mara wageni wakatokea wakiwa na ticha mmoja hivi...mzungu mmoja akawauliza what is the matter..??..
dogo mmoja akajibu....matter is anything that have weight and occupie space....ikabidi wazungu waendelee na shuhuli zao...
 

ha ha ha ha ha ha ha.
ha ha ha ha ha ha ha ha

mkuu kumbe hata shule tumesoma moja ?
 
ZANAKI tunaingia advance kwenye orientation course sasa kwenye kwenye kujitambulishakuna mdada akasema "my name is eliza i come from here here"
 
Tuliwahi kusafiri na Mstahiki Meya wa jiji Fulani hapa Tanzania (jina kapuni) kwenda kwenye mkutano wa kimataifa huko UK (London) sasa kumbe yeye sijui hakuambiwa au alifurahia per diem tu kufika kule waandaji wakawa wanamkumbusha kuwa unapaswa ku-chair one of the session katika mkutano duuh mstahiki meya akaniomba nimsaidie nikamuambia kwa wakati huo ndo nitakuwa nawasilisha pepa (mada) pengine waliamua kumteua yeye maana tunatoka nchi moja iwe rahisi kuni-introduce daah jamaa alipoona haina jinsi ilibidi asepe kiaina hakuonekana kwenye ile session duuh ikabidi nimuombee udhuru nika-act kama session chair kisha nikawasilisha mada/pepa. Sasa baadae jioni namuona kwenye msosi namuuliza mstahiki ulikuwa wapi akadai alibanwa na tumbo la kuhara
 

Hahahhahaha duh
 
Form one hiyo pale Mwanza...demu mmoja alisema " my headmaster is headmistress!" Akiwa very comfortable kabsaaa. Then hapo hapo kwenye question tag..njemba akakurupuka " you took my book, tooknt you?" Ahahahahahha kiingereza hiki!?
 

hahahahaha umetisha mkuu
 
ha ha ha aha aha aha aha. jamii forum raha sana
 
Mdogo wangu aliandika essay ya kwanza katika kiingereza na kunipa nisahihishe ndipo nikakutana na hii line: "...my first of my girl friend is when I meet her in the night of the moon of July 31, 1992 when my friends and me go to disco toto..."

Nikashikwa na kizunguzungu na kumuuliza alikuwa anamaanisha nini.

Akanijibu: ...demu wangu wa kwanza nilikutana naye usiku wa mwezi July 31, 1992 wakati nilienda disco toto na washikaji..."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…