Siku ya Wanawake Duniani isitumike kutengua maandiko ya vitabu vitakatifu

Siku ya Wanawake Duniani isitumike kutengua maandiko ya vitabu vitakatifu

endeleeni kutunisha misuli, ila vipigo vitawahusu sanaaa
 
Vitabu vimemfanya mwanamke kuwa chini ya mwanaume, sasa kuna ulazima mwanamke nae apambanie haki yake, kuna wanawake wengi wenye akili na maarifa kuliko wanaume wengi, wanayo haki ya kuwa juu ya wanaume kama wamewazidi akili na maarifa.

vitabu vimemfanya mwanamke kuwa chini hivi ni vitabu vya mungu unajua hilo. kwa hiyo unataka tv za binadamu ndio zimpandishe mwanamke
 
super women wametajwa na mungu ndani ya quraan nao ni 4 tu je unawajua nitakutajia wawili nawe umalizie wawili 1: mariam mama yake issa bin mariam (yesu) wa pili mke wa farao au firauni nawe malizia
 
Mama wewe ni moja ya wanawake wenye akili sana.

Mwanamke yeyote anaelilia haki sawa hawezi kuishi hata na hawara. Ataishia kutumika tu sababu ya kiburi wanachopewa na Serikali na Wanaharakati haramu wa 50/50.

Ukiwa Mwanaume ukishabukia haki sawa nakuona punguani sana, tena uliebobea.
Kabisa
 
Men you are the PRIZE narudia tena Men you are the PRIZE...akili kumkichwa ni hayo tu kwa leo
 
Kuna hii kitu yetu inaitwa siku ya wanawake, kuna hii kitu inaitwa super woman na kuna hii kitu tumeanzisha inasema mwanamke ni kichwa cha familia.

Wanawake kuna sehemu tumetumbukizwa shimoni na wapigania haki za wanawake na bila kujijua tumejaa viburi na sasa tunajitokeza adharani kudai sisi kwa asilimia kubwa ndio tunalisha familia.

Wanawake wengi wenye mentality kwamba wanalisha familia ndoa zao zimeyumba na watoto wapo taabani kimalezi kwa sababu tu walezi wamepishana.

Dini zipo na zinaeleza vyema lipi jukumu la mwanamke ila kwa kasi tuliyonayo imetufanya twende kinyume kabisa na maandiko, tukipata nguvu kidogo tu ya uteuzi au kupata kamtaji kwetu tayari ni agenda yakuwaumiza wanaume. Wanaume wakituchoka wakaondoka hapo ndipo tunajua sisi kamwe hatuwezi kuwa kichwa cha familia.

Tukubali tukatae tunapaswa kuishi na wanaume kama vichwa vya familia na sisi ni mkia. Tukijitutumua na hadithi za super woman tutaishia kutumiwa na makundi ya wanaume huku tukiwa tunakwama kwenye malezi. Tuwaheshimu waume zetu regardless ya vyeo vyetu na madaraka au fedha zetu.

I'm not thinking of superwoman rather gifted woman.
Sanamu yako iwekwe pale Dodoma pembeni ya sanamu ya Nyerere na siku yako ya kuzaliwa iwe mapumziko ya kitaifa.
 
Akili na maarifa pekee hayatoshi kumfanya mwanamke akawa juu ya mwanaume, sababu Historia imeandika juu ya wanawake walio kuwa na sifa za wanaume ila walikuwa chini ya wanaume. Ujuu wetu sisi Wanaume dhidi ya Wanawake ni silika na hii ndiyo inaainisha majukumu.

Mwanamke apambanie haki yake ipi na umejuaje kama hiyo ni haki yake ?

Maarifa na akili ya Mwanamke anatakiwa aitumie nyumbani katika kulea na kusimamia mali za mume na kumshauri, ila Mwanamke kutska kuwa jui ya Mwanaume ni kwenda kinyume na asili na ni kujitafutia matatizo kama wanayokutana nayo leo hii, japo wanajidai ni hamnazo.
Hakuna asili ya mwanamke kuwa chini ya mwanaume huo ni upuuzi wa mavitabu yaliyotungwa kumbana mwanamke na tamaduni kandamizi , akili na maarifa ya mwanamke anaweza fanya apendavyo ikiwemo kuwa juu ya mwanaume bila taabu yeyote , ni suala la kuamua tu kile apendacho
 
Huo kuwa juu ya Mwanaume,Usuper Woman,sijui kichwa cha familia na upuuzi mwingine unaofanana na huo utaufanya ukiwa kwa Baba yako Mzazi.
Unafanyika popote, hayo mavitabu yenu na tamaduni mfu , zimepitwa na wakati
 
Hapana hawaoi. Wanalipa ili kumpa mwanamke heshima na utu wake katika ndoa yake asionekane kama aliuzwa au alilipiwa pesa.

Pili, wanafanya vile kama shukurani kwa familia ya mwanaume kumpokea binti yao na kumfanya sehemu ya familia na kuishi nae....

Sent using Jamii Forums mobile app
Anaelipa mahari ndio muoaji ,ahahahhaa unatetea ujinga , INDIA wanawake ndio wanaolipa mahari ndio waoaji hao acha porojo
 
Mwanamume by nature anapenda kutawala na kuheshimiwa. Mwanamke ukidhani umemcontrol mumeo ndani, jua wazi kabisa kwa 100% huko nje keshatafuta mchepuko ambao unamthamini na kumuheshimu hata kama hauhongi pesa ile kisawasawa kwa sababu za kiuchumi
 
Hakuna asili ya mwanamke kuwa chini ya mwanaume huo ni upuuzi wa mavitabu yaliyotungwa kumbana mwanamke na tamaduni kandamizi , akili na maarifa ya mwanamke anaweza fanya apendavyo ikiwemo kuwa juu ya mwanaume bila taabu yeyote , ni suala la kuamua tu kile apendacho
Una matatizo ya akili. Mjinga huwa nampa amani.

Na wewe tunga tuone, kama kweli vitabu hivyo vimetungwa na binadamu. Ukiwa unaandika mambo hakikisha una elimu nayo na ukiombwa ithibati uweze kutupa.

Nakuacha na swali hili "Kitabu gani kimetungwa na sifa ya utunzi wa kitabu ni zipi ?".
 
vitabu vimemfanya mwanamke kuwa chini hivi ni vitabu vya mungu unajua hilo. kwa hiyo unataka tv za binadamu ndio zimpandishe mwanamke
Vitabu haviwezi kutupangia tulio hai cha kufanya, unamfanya mwanamke kuwa chini halafu unasema kitabu cha Mungu? tutampuuza kwa hili
 
Una matatizo ya akili. Mjinga huwa nampa amani.

Na wewe tunga tuone, kama kweli vitabu hivyo vimetungwa na binadamu. Ukiwa unaandika mambo hakikisha una elimu nayo na ukiombwa ithibati uweze kutupa.

Nakuacha na swali hili "Kitabu gani kimetungwa na sifa ya utunzi wa kitabu ni zipi ?".
Vitabu vimetungwa na binadamu tena mwanaume, ndio maana akamfanya mwanamke kuwa chini yake, sasa unataka maelezo gani !!!
 
Vitabu vimemfanya mwanamke kuwa chini ya mwanaume, sasa kuna ulazima mwanamke nae apambanie haki yake, kuna wanawake wengi wenye akili na maarifa kuliko wanaume wengi, wanayo haki ya kuwa juu ya wanaume kama wamewazidi akili na maarifa.
Maisha yetu wanadamu yapo katika mifumo,na mfumo pekee ambao kiukweli tukiufuata utaleta amani ni Mfumo wa kidini.Turejee Dini zinasemaje baasi.Japokuwa kuna wanawake pia waliozaliwa na Internal hormones nyingi za Baba zao,hawa huwezi kuwaambia kitu kirahisi kwa sababu Naturally mna kitu inafanana Internal. Lakini kwa Mwanamke mwenye hormone za kike nje na ndani kama huyu mtoa Mada basi lazima utulivu uwepo katika siku zako unazosubiri kifo.
 
Dini ndio adui namba moja wa mwanamke, hakuna marejeo hapo
 
Back
Top Bottom