Sikubaliani na pendekezo la Waziri wa Fedha kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa arudishwe kwenye mshahara wake wa awali

Sikubaliani na pendekezo la Waziri wa Fedha kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa arudishwe kwenye mshahara wake wa awali

Nimefuatilia hotuba ya Bajeti ya mwaka 2022/2023 na kwenye kipengele kinachosema kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa basi arudi kupokea ule mshahara aliokuwa anapokea kabla ya uteuzi. Hili ni pendekezo.

Binafsi sikubaliani kabisa na pendekezo hili. Mhe. Waziri usije ukaleta vurugu hapa nchini. Nchi hii tunapendana. Utakuta wengi wanaotumbuliwa ni uonevu.

Wabunge hili ni pendekezo mkatae kwa asilimia mia moja.
Umeleta hoja ya ovyo kabisa. Ni sawa na kusema waziri akitumbuliwa aendelee kulipwa mshahara wa uwaziri ilhali si waziri tena!!! Kila mtu alipwe kupingana na kazi yake.
 
Unakuta kwa mfano mtumishi ni Principal Officer anayepata mshahara wa TGS H6 then anateuliwa kuwa Mkurugenzi ambaye mshahara wake say ni LSS 3. Ina maana huyu Mkurugenzi siku ukurugenzi wake ukitenguliwa Mwigulu anapendekeza arudi kupokea TGS H6 yake, asiendelee na huo wa ukurugenzi.
Ni sawa kabisa, hatuwezi kulipa zaidi ya mtu mmoja katika nafasi ileile. Kila mmoja alipwe kulingana na nafasi yake kiutendaji.
 
Yani mfano kama mtu alikuwa mwalimu akateuliwa kuwa DED anakuwa anakula M 3 na malupulupu kibaoooo.Sasa ikatokea paaap akatenguliwa basi anarudi kwenye laki 7 badala ya M 3
Na hii itaongeza uwajibikaji sio kubweteka kama ilivyo sasa
 
Umeleta hoja ya ovyo kabisa. Ni sawa na kusema waziri akitumbuliwa aendelee kulipwa mshahara wa uwaziri ilhali si waziri tena!!! Kila mtu alipwe kupingana na kazi yake.
Usichanganye kazi ya utumishi wa uma na uwaziri. Utumishi mtu anapanda kwa utaratibu maalum, halafu umshushe mtu cheo na mshahara
 
Kwa hiyo kama Katibu mkuu ameondolewa kwenye nafasi yake aendelee kulipwa mshahara wa ukatibu mkuu??
Huyo mtu sijuianatetea maslahi ya nani. Hiyo si mishahara hewa hapo kutumbuliwa kutakuwa na maana gani .ama urefu wa kamba ndo unaathirika tu
 
Nimekuelewa una maanisha hata ikitokea mtumishi amepandishwa cheo abakie kwenye msahara wake wa zamani. Ndo unamaanisha hivyo?Acha ubinafsi kwenye Mali za walipa kodi. Usiangalie jambo kwa upande mmoja, maisha ni shilingi
 
Tatizo linaanza mwalimu anapoteuliwa kuwa DED.
Yani mfano kama mtu alikuwa mwalimu akateuliwa kuwa DED anakuwa anakula M 3 na malupulupu kibaoooo.Sasa ikatokea paaap akatenguliwa basi anarudi kwenye laki 7 badala ya M 3
 
Ni lazima ufikie cheo gani cha utumishi ili ukidhi kuwa katibu mkuu wa wizara??
Usichanganye kazi ya utumishi wa uma na uwaziri. Utumishi mtu anapanda kwa utaratibu maalum, halafu umshushe mtu cheo na mshahara
 
Ili kupunguza songombingo wateue wenye vyeo vya juu kabisa ndo wawe wakuu wa idara na huo mshahara wa cheo cha juu uwe sawa na mshahara anaolipwa mkuu wa idara. Kwa hiyo akitumbuliwa bado atalipwa mshahara huo huo wa daraja lake. Maana mtu anaweza kupata uteuzi na madaraja yake yasipande kutokana na kwamba mshahara wake wa uteuzi ni mkubwa zaidi ya kile cheo cha juu kabisa. Sasa ukitumbuliwa ina maana arudi kwenye lile daraja ambalo huenda hakuendelea kupandishwa kutokana na kupata uteuzi.​
 
Unakuta kwa mfano mtumishi ni Principal Officer anayepata mshahara wa TGS H6 then anateuliwa kuwa Mkurugenzi ambaye mshahara wake say ni LSS 3. Ina maana huyu Mkurugenzi siku ukurugenzi wake ukitenguliwa Mwigulu anapendekeza arudi kupokea TGS H6 yake, asiendelee na huo wa ukurugenzi.
Mshahara kwa sasa huwa unabaki ule ule ila marupurupu ndiyo yanaondoka.
Binafsi naona wangeacha mana italeta conflict kwenye sheria na kanuni za kiinua mgongo na mafao ya uzeeni. Sasa hivi kikokotoo kinazingatia mshahara wa mwisho ambao mtu anapokea ili kuamua kiinua mgongo kiweje.
Au wangeweka scale mpya yenye punguzo la asilimia fulani kwa wote wanaotenguliwa.
Shida yetu kubwa ni kuwa kila Rais anapoingia, hubadilisha nafasi zote za uteuzi kitu ambacho hakuna ulazima, hivyo husababisha unakuwa na Serikali mbili za kulipa mishahara, ya pili ile ya waliokas benchi baada ya kuwatengua. Wengine hutenguliwa ili aingie mwengine kiurafiki, uswahiba wa kisiasa na mara nyengine rushwa.

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
Eeh..i
Nimefuatilia hotuba ya Bajeti ya mwaka 2022/2023 na kwenye kipengele kinachosema kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa basi arudi kupokea ule mshahara aliokuwa anapokea kabla ya uteuzi. Hili ni pendekezo.

Binafsi sikubaliani kabisa na pendekezo hili. Mhe. Waziri usije ukaleta vurugu hapa nchini. Nchi hii tunapendana. Utakuta wengi wanaotumbuliwa ni uonevu.

Wabunge hili ni pendekezo mkatae kwa asilimia mia moja.
Inamaana wale wote walikuwa wanatenguliwa na jpm waliendelea kulipwa mishahara ileile..
duh hii inchi bado tunasafari ndefu..
 
Back
Top Bottom