Coping Strategy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2014
- 439
- 387
bangi usinizingue kihivyo simuachi huyu kimwana.kivipi nimkazie jicho wakati bint kasimama.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
bangi usinizingue kihivyo simuachi huyu kimwana.kivipi nimkazie jicho wakati bint kasimama.
Huo ndio ubunifu ninao usemea mimi.hana ubunifu wowote.
kama wewe sio msomaji wa vitabu vya kiswahili basi utaamini kuwa Huyo jamaa ni mbunifu, lakini kila anachokiandika kilishaandikwa na akina Andanenga.
jiulize ni msemo wake upi au methari au nahau iliowahi kuwekwa kwenye kumbukumbu kuwa hii ni Brand ya Fareed?
Huwezi ku copy bila kutafuta sana.[emoji14] [emoji14] Sawa, ila mimi sio shabiki kabisa wa fid q na nimezungukwa na raia za kutoka Arusha kibao wasiomkubali maana wale ndio awampendi sana jamaa maneno yao ni yale yale jamaa anacopy anacopy , ila mimi sijawahikubali ilo kusema jamaa sio mzuri kisa anacopy..Heshima kwake [emoji122] [emoji122]
Hebu nielekeze ngoma za huyo jamaa unayemkubali maana hata simjui, vp anamzidi ChindoSonga mwenyewe anamkubali Fid Q
Wanashangaa kuona ng'ombe anakula nyasi halaf anatoa maziwaHupaswi kumwamini muongo hata kama akiongea ukweli.
Humu leo sijui kama patatosha!
Nimekuwa nikijaribu kudigest sifa ambazo wadau wengi wamekuwa wakimpatia msanii Fid Q, kwamba ni mtu makini, mwenye upeo wa hali ya juu.. Kiukweli nimejitahidi sana kuamini lakini leo acha tu nizitendee haki instincts zangu za muda mrefu..
Si kweli. Fid hana hiyo gene!
Mwaka jana mwanzoni, huko Marekani alitokea mtoto wa miaka 14 aliyebuni saa ambayo ilikuja kudhaniwa ni bomu hivyo kumkamata na kumtia kizuizini kwa masaa kadhaa kabla ya kubainika kuwa ni saa tu isiyo na madhara na baadae kuitwa Ikulu na Rais Obama kupongezwa kuwa ni genius.
Nilichopenda kwenye mkasa huo, ni jibu la mwalimu wake pale alipoulizwa kuhusu 'ukipanga' wa huyo mtoto na anajisikiaje kufundisha mwanafunzi genius darasani kwake.
Alisema hivi, "Namjua vizuri Ahmed, sio mwanafunzi genius kama inavyodaiwa, ila ana jitihada sana ya kusoma na kujifunza. Jitihada zake ni zaidi ya wanafunzi wote ninaowafundisha".
Sasa hii ni kama ambavyo Fid anatajwa kuwa genius kutokana na uandishi wa tungo zake. Kwamba anafikiria sana na ni kichwa kuliko wasanii wote. Niseme ukweli, binafsi sikuwahi kuona hivyo, bali nimekuwa nikimwona kama msanii anayejitahidi sana kujifunza kuliko wasanii wengine. Hapa tusichanganye.
For someone to be genius, ni lazima awe innovative! Lazima aache impact. Ni bora nikamfagilia MwanaFA angalau yeye ameacha misemo mingi kwenye lugha ya Kiswahili.
Kituko hiki hapa sasa..
Nikki wa Pili alipouliza swali kuhusu kwanini vichaa hawaongozi kuugua kipindupindu licha ya kula vyakula vichafu, Fid anajibu ni suala la Kisaikolojia. Eti, akili yako ukiiambia kwamba nikila hiki chakula kichafu nitaugua, utaugua kweli. Na ukisema sitougua, hutougua. Hivyo vichaa hawana hiyo time ya kujua kama ni kichafu ndio maana hawaugui. Nilichoka.
Huo ni mfano mmoja tu. Mwingine nitajazia kadri mada hii itakavyoendelea.
Poleni kwa kusoma mkeka!
Sorry kama nimekoti vbaya hii iwaendee wale wote wanaomponda Fid QIlo jibu la kwangu au ulikuwa upo usingizini wakati unajibu.??