Sikujua, kumbe Bakhresa anakopa mikopo ya riba kwenye benki za biashara

Juzi nilienda kwa mwamposa waislamu ndo walikua wengi wakipata uponyaji
 
Kuna baadhi ya project nchi hii huruhusiwi kufanya bila kukopa benki za Biashara, ni Lazima.

Zipo benki za kiisilamu ambao hao hao matajiri wanatumia.

Pia hizo hizo benki za Biashara kama NBC wana sharia bank, huwezi jua anakopeshwaje.
Ukuna ulazima wa kukopa benki bhana
 
Dini aiwezi kumzui mtu kuwa tajiri kama ndivyo watu wengi wanakopa mikopo benki na kwenye vikoba lakini bado wako na ukata wa kipato tu riba ni dhuruma ni wizi ujambazi,dini inayo zuiya riba ni 1tu ndio kusema mafukara nchii wako kwenye hiyo dini tu?
Duuh kwahiyo kwa uelewa wako wewe mtu kukopa kwa riba ndio kuwa tajiri
 
Tatizo lako unajitia kujua kumbe ujui lolote,nani kahukumiwa hapa?maimamu kazi yao kunukuu maandiko mfano riba pombe banghe uzinzi nk ni haramu wakisema hivyo wamehukumu?
Hayo mane ya maimamu ndio furaha masikioni kwetu wewe kaahukohuko kanisani huku kwetu nafasi yako haipo
 
Watu wanakosoa dini kama wanavyokosoa ujinga mwingine uliopo kwenye jamii, kwani watu wa dini ni kina nani hadi wasikosolewe wewe ndio uache kusikiliza wakosoaji, komaa kushikilia dini yako kwa sababu watu hawataacha kukosoa hadi mwisho wa dahari
 
Bakhresa sio reference ya Uislam, iwe kweli kakopa Bank au laa hiyo haina uhusiano wowote na katazo la Uislam kwny masuala ya riba

athari za riba hivi sasa zipo wazi kuliko miaka ya mwanzo ya katazo hili
Kweli kabisa mtaani kwangu kuna nyumba zaidi 10 zitapigwa mnada na benki vikoba navyo kila kukicha vinasafisha viumba via watu mafukara kuwanyanganya thamani za ndani
 
Kupigwa ilikuwa haki yake sababu alileta ushenzi kwenye mkusanyiko wa dini pia ufahamu kuwa serikali haina dini
 
Nilidhani ustadhi ni wale watu wa dini wasiojihusisha na riba kumbe ni mdau mzuri wa benki za biashara.

Ninapenda Bakhresa afanye kuwaelimisha wale wenye misimamo mikali tuwe na taifa endelevu.
Hakuna tajiri mkubwa asiyekopa nimefanya kazi makao makuu NMB na NBC ,najua nachokiandika.Biashara haina dini
 
Kama kapuuza msiende kwenda kuomba michango ya ujenzi wa misikiti au madrasa au kufuturishwa Ramadhani au kuomba asaidie wahitaji na kupanga foleni akitokea iwe msikitini ,nyumbani au barabarani au popote kuzitendea haki nafsi zenu
Kwani wameja kuomba kwako,mungu alie kuumba ndio maana kukufanya kuwa mnyonge fukara kama angekupa utajiri watu tungeishi kwa shida sana
 
Hawa watu wa ilimu ya kukariri huwa Wana shida Sana.
🔹 Unakuta wanasema kuimba ni haramu lakini Sala zao zote zinafanyoka kwa Kuimba kuanzia adhana ile ni melodic kabisa hata wanavyotamka zile sura walizokariri kuanzia alfatiha ni kwa njia ya kuomba na sauti ni ile ile kama ya Gregorian chant ya wakatoliki.

Kadhalika Wana kwaya zao ambazo huimbwa na watoto wadogo au wanaume wazima huitwa kwa jina la kiarabu QASWIDA lakini ni majina tuu hazina tofauti na kwaya za wakristu . Maana kwenye kwaya sio maneno tunayoangalia Bali ni sauti zinazoimbwa kwa pamoja kwa kufuata sheria za muziki.

🔹 Kwenye suala la kukupa mikopo ya riba unaweza kushindana nao mpaka kesho wanakuambia wanakopa kwenye Benki zao zisizo na riba wakati lazima mkopo uliokopa urejeshe na garama. Whether in terms of money or bidhaa. Hiyo ndio kwenye biashara ya fedha inaitwa interest tunapofanya fedha kama commodity. Hata hivyo hizo Benki za mfumo huo zipo nyingi bongo na zingine wanamiliki wao lakini mbona waamini wao tunabanana kwenye taasisi za riba kama ya kule ni nafuu na Haina riba? Elimu, elimu ,elimu
 
Nilidhani ustadhi ni wale watu wa dini wasiojihusisha na riba kumbe ni mdau mzuri wa benki za biashara.

Ninapenda Bakhresa afanye kuwaelimisha wale wenye misimamo mikali tuwe na taifa endelevu.
mambo ya mikopo binafsi we unayajiaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…