Sikuona sababu ya kumtenga mke mkubwa wa Ndugai msibani

Ndio marehemu alikueleza kuwa hizi ndio sababu za kuachana mke wake wa kwanza?
 
Yote hayo mhusika alikuwa anayajua na alikuwa msimamizi wa hizi Sheria, kwanini yeye asingepigania haki mapema? Bunge sio lakulaumiwa itakuwa huyo ndiye aliyetambulishwa na muhusika , sasa mnampangia marehemu jamani wakati yeye ndiye alikuwa akipata furaha yake wandugu?

Ukiachwa siku kaondoka hata msiba sihudhurii kabisa maana wanakunanga kama mtu ulikuwa unampenda Lilia kwako basi.
 
Unasimama kudai nini? Utapinga kuwa baba Yako hakuoa mwanamke mwingine? Utaonekana kituko wewe na huyo mama Yako hapo msibani
Hata wewe shangaa, yaani badala yakudai chako mapema eti mtu kafa ndiyo nipeleke kwato? Mie hata msibani siendi, kama hakunipenda akiwa hai hapo kalala atanipenda? Aende salama tu, kama kulia nitamlilia kwangu basi.
 
Aibu zakujitafutia
 
munajikusanyia dhambi za bure kwa uzushi wenu
 
Huyo wa pili ana ndoa nae? Mwenye ndoa ndiye mwenye haki zote kisheria.
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tz, kuna aina tatu (3) za ndoa hapa Tanzania:-
1. Ndoa za Kidini.
2. Ndoa za Kiserikali.
3. Ndoa za Kimila, hapa hakuna Cheti Cha Ndoa kinachotolewa na Serikali.

Ndoa zote hizo ni halali kwa mujibu wa Sheria.
Katika muktadha huo, naweza kusema (kujibu swali lako) kwamba, ndiyo, huyo mke wa pili alikuwa na ndoa na marehemu Job Ndugai.

Aidha, ndoa tafsiri yake siyo cheti bali ni muunganiko wa hiyari Kati ya mume na mke.
Vile vile, nchini Tanzania uwepo wa ndoa Kati ya mume na mke hauthibitishwi kwa kuwepo kwa cheti Cha ndoa tu peke yake, hata ushahidi wa Mazingira wa Watu hao kuishi pamoja kwa muda fulani pia ni uthibitisho tosha wa kwamba Watu hao ni Wanandoa.
 
Mshauri mwingine huyu! Hebu waache watu waishi maisha yao.
 
Hujielewi!
 

Msaada wa kupata video clips za maelezo ya mke mkubwa kuwa walifunga ndoa na Ndugai mwaka 1988 kama alivyosema mtoto mkubwa wa Ndugai ambaye video clip imeondolewa sehemu hiyo
 
Kutengana sio kuachana
Ni kweli kabisa kwamba Kutengana siyo Kuachana. Lakini huyo Mwanamke wa kwanza hawezi kurudi tena kwa mumewe eti kwa ajili ya kufuata Mali tu ambazo kimsingi hajawahi kushiriki katika kuzichuma Mali hizo. Kurudi kwa mumewe inaruhusiwa, lakini angefanya hivyo wakati mumewe huyo akiwa bado yupo hai au Kama angerudi kwa ajili ya kufuata Mali ambazo yeye huyo Mwanamke amezitolea jasho lake katika kuzichuma Mali hizo. Hawezi kurudi Sasa hivi wakati mumewe tayari amefariki. Kitendo chake Cha kutaka kurudi kwa mumewe marehemu kwa wakati huu ni uthibitisho wa wazi kabisa kwamba huyo mama ni tapeli na dhulumati, anataka kudhulumu Mali za marehemu ambazo kimsingi yeye hajashiriki katika kuzichuma. Hivyo, kitendo chake hicho Cha kutaka kurudi kwa mumewe wakati huu kinaonyesha wazi kabisa kwamba ANA NIA OVU huyo Mwanamke ya kutaka kudhulumu Mali za Marehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…