Sikuwa na mpango wa kuwa na Mtoto wa nje lakini huenda ikawa hivyo

Sikuwa na mpango wa kuwa na Mtoto wa nje lakini huenda ikawa hivyo

Kuoa makapi inahitaji moyo sana🤣🤣halafu mahari upigwe pesa ndefu.

Kijana demu kama kachezewa hana thamani na pia ukileta noma ana-backup ya wanaume kibao ,ukizingua anaanza kuwachek ma-ex wake kuwa makini.

Usione watu wanaoa wasichana wadogo ila kupunguza mlolongo wa mahusiano ya nyuma, assume alikuwa na watu hata 5 na je wote kapita nao? hakuna hata aliyepeleka posa kwao we hujiulizi tu!


Msichana ni dhaifu sana mbale ya ma-ex wake walimtoa ushamba kweny mapenzi ,kaa kijanja utakuja kujinyonga..
 
We are sailing the same boat. Nahisi nitaoa mwingine muda siyo mrefu, nilijizuia sana kuwa watoto wa mama tofauti, ila the situation I'm confronting compels me to so be.

Hivi huwaga mnataka kujua history za wapenzi wenu ili iweje unakuta unakazana na kulazimisha uambiwe ukweli

Ukiambiwa ukweli unaanza kuumia… mwisho wa siku munaoa wanawake musiowapenda et kisa ana history nzuri

Heri mwanzo mbaya kuliko mwisho mbaya
 
Bro mtoa uzi kuwa makini wanawake wanatunza siri sana,
Why akuambie???????
Jiulize kwanza hilo bro????

Wewe nae umeshupaliaa mwenzio aachwe

Huyo kaka Kama alikuwa anakomalia aambiwe ukweli ulitegemea nini

Mtu kashampa na mimba aliona anafaa hizo past ni past tu ni afadhari mwanzo mbaya kuliko mwisho mbaya
 
Na hiki ndicho kinachonitesa, nawaza vingi mno akilini mwangu, mpaka nafikia hatua ya kuwaza kuwa jamaa amefaidi usichana wa mwanamke wangu kwa kipindi kirefu akimtumia vile atakavyo, kuliko mimi ambaye nimekaa naye mwaka mmoja kisha kupata ujauzito.

Wewe wanawake wa wenzio uliowatumiaa nani awaoe??

Acha ubinafsi bro
 
[emoji23][emoji23][emoji23] nimechekaa

Ya mwisho nimeipenda hatujadumu tulikulana mara moja hata hivyo sijawah kupenda wewe ndio wa kwanza[emoji1787]

Hata niwe in love kiasi gani siwezi kumwambia new baby ukweli kuhusu ex wangu
Huo ndio utaratibu. Sio unajitafutia matatizo.
 
Wewe wanawake wa wenzio uliowatumiaa nani awaoe??

Acha ubinafsi bro
Sawa lakini sikufanya makosa ya kuishi nao, huku wakinihudumia kwa huduma zinazopaswa kutolewa na mke.
 
Basi hutooa maisha yako yote, sidhani kama yupo mwenye historia nzuri 100% tena kama sio bikra ndo kabisaaa (na nyie historia za sisi kudinywa ndo zinawaumaga as if nyie hamjawahi)
Ukweli ni kwamba mwanamke ndiyo hupaswa kujilinda, na ndiyo maana familia nyingi zinahakikisha mtoto wa kike analindwa vyema, kamwe hawezi kuwa sawa na mwanamme.
 
Bado nawaza aliwashwa nini hadi ayaseme hayo, jinga kweli.

Kikao kilishaamua kama bikra ilishaondoka na pikipiki basi yeye ndio wa pili na huyo wa kwanza hata hamkudumu saaaana. Na wala haujawahi penda kama unavyompenda yeye.
Mrs. ERoni

Nakupungia mkono
 
Sawa lakini sikufanya makosa ya kuishi nao, huku wakinihudumia kwa huduma zinazopaswa kutolewa na mke.

Sawa muache kaoe huyo ambae ana history nzuri

Ila ukikutana na Kama sisi hatutokuambia chochote kuhusu ex na utatuoa baada ya watoto 3 ndio unasikia habari zangu labda niliwahi kuwa najiuzaa kimboka au nilikuwa natembea na waume za watu navunjaa ndoa zao

Kiufupii Hakuna kosaa hapo ukizingatia mlikuwa hamjuanii
Hayo ni maisha tu yapo tunayaona wadada wengi tu wanaishi kinyumba na wapenzi wao wanaachana wanaolewa na wenginee
 
muache kabisa mkuu hakufai huyo ni mmbea kama ameshindwa kuificha hiyo siri yake atatoa zako nyingi sana hasa ile ya kujamba kila unapofikia mwisho. Kulikua na haja gani ya kukwambia huyo dada ndo zake namjua sana anaitwa mainda mtumie boda akamfaulishe ukirudi usimkute shubamit
 
Ulimsamehe kimya kimya kwali alikukosea kutokuwa bikra?? Je wewe umemuoa kwa ndoa hadi umsamehe kutokuwa bikra au mnazini tuu??

Na kinachokufanya urindime hasira ni yeye kuishi na mtu kabla hamjajuana seriously dude?? Labda kama unataka kupita hivi baada ya kumpa mimba ndio unamtafutia sababu.

Kumpa adhabu kama nani wewe?? Acha kujipa uMungu kujiona unamtawala simply because ni mpenzi wako na umempa mimba, eti adhabu ndogo khaaa aiseee. Mpe pole yake kwa aina ya mpenzi, baby dady aliyempata
Sijipi uMungu mtu, kufanya mapenzi siyo tatizo kubwa kwangu na ndiyo maana hilo halikuniumiza, kwani hata mimi nimetembeza kichapo sana kwa mabinti wengine, tatizo lililopo hapa ni mwanamke ambaye mimi ndiyo niliyemchagua kuwa Mama wa familia yangu, kuwa na historia ya kuishi na mwanamme, nielewe vizuri, ukiishi na mwanamke maana yake huduma unazopewa kama mme amewahi kutoa kwa mwanamme mwingine tena kwa miaka miwili, aisee inauma sana.
 
Sijipi uMungu mtu, kufanya mapenzi siyo tatizo kubwa kwangu na ndiyo maana hilo halikuniumiza, kwani hata mimi nimetembeza kichapo sana kwa mabinti wengine, tatizo lililopo hapa ni mwanamke ambaye mimi ndiyo niliyemchagua kuwa Mama wa familia yangu, kuwa na historia ya kuishi na mwanamme, nielewe vizuri, ukiishi na mwanamke maana yake huduma unazopewa kama mme amewahi kutoa kwa mwanamme mwingine tena kwa miaka miwili, aisee inauma sana.

Ubinafsii huo usingempa mimba basi umchunguzee

Yaaani wanaume waajabu sana kwanza kwanini upate mtoto kabla ujaoa una haribu tu future ya mdada wa watu ndio maana mnarogwaa
 
Ubinafsii huo usingempa mimba basi umchunguzee

Yaaani wanaume waajabu sana kwanza kwanini upate mtoto kabla ujaoa una haribu tu future ya mdada wa watu ndio maana mnarogwaa
Daaah.
 
Unajipa presha bure,maisha hayahitaji u seriazi haya,TAKE IT EASY SIR.
 
Wakuu kwema,

Moja kwa moja kwenye mada, katika maisha yangu nilijitunza sana ili kuhakikisha sizai hovyo na mwanamke ambaye sitamuoa na nihakikishe napata mwanamke sahihi kwangu na kwa mstakabali mzima wa familia yangu (watoto).

Katika harakati za maisha nimefanikiwa kukutana na dada, ambaye kwa mwonekano wa nje Angefaa sana kuwa mke wangu na mama wa watoto wangu, nikiri kuwa nilimpenda sana, bila shaka hata yeye kanipenda sana, kwa ufupi kaja kwangu nimeendelea kula mzigo dada kabeba ujauzito na anaelekea kujifungua.

Juzi hapa nikiwa kitandani nawaza mambo ya dunia, kwa upole na kwa hekima ya hali ya juu kaniingizia jambo ambalo ukweli limenitoa kwenye reli.

Kwa kutanguliza msamaha na kwa unyenyekevu wa hali ya juu kanieleza kuwa pindi akiwa chuo kuanzia second year hali ya maisha ilikuwa ngumu sana kwa upande wake kutokana na wazazi kutomtimizia mahitaji ya msingi (fedha ya chakula) kwani alisomeshwa na wazazi .

Hivyo kutokana na hali hiyo ilipelekea kuhama hosteli na kwenda kukaa kinyumba na mwanachuo mwenzake (mwanamme) mpaka kumaliza chuo kisha akaachana naye, huyo jamaa alikuwa na boom, hivyo basi kutokana na hali hiyo jambo hilo amekaa nalo moyoni kwa muda mrefu ila ameshindwa kuvumilia anaomba msamaha na kunisihi nimuamini katika maisha yake yote.

Niseme tu kwamba sijaongea chochote mpaka sasa, nimekosa cha kumjibu na hapa moyo wangu unarindima hasira isiyo na mfano, chakula hakipandi na nahisi kupaliwa na kila kiingiacho kinywani kwangu, kila adhabu nayowaza nahisi ni ndogo kwake.

Wakuu wenye hekima na busara naomba mawazo yenu, maake nahisi mi nimefika ukomo wa kuwaza zaidi ya kutaka kufanya maamuzi magumu na ya ovyo.

Sasa mambo ya adhabu yanatoka wapi tena mkuu kwa mtoto wa mwenzio.Nadhani ameamua kukwambia ukweli.angeweza kukaa kimya na mambo yangesonga

kama mmekutana katika utu uzima,amefunguka cv yake kamili.Tuwe ni watu wa kutowadhalilisha wenzetu as if sisi ni watakatifu kabisa.Kumbuka na wewe mambo yako ya hovyo uliyokwisha yafanya kabla yake
 
Back
Top Bottom