Tutajie hizo silaha za Nato zilizoonyesha uwezo mdogo.
'Javelin' ndio kiboko ya vifaru ya Warusi, vingi vimeishia kugeuka vyuma chakavu hapo Ukraine.
T14 Armata
India mwezi huu imechochea program yake ya kuongeza idadi ya fighter jets zisizozidi 114 kwa gharama ya dola bilioni 20 za Marekani. Kati ya ndege tano top contenders hakuna ndege ya Urusi. Ndege mbili za Boeing ya Marekani, Dassault Rafale ya Ufaransa, Lockheed Martin ya Marekani, Saab ya Sweden, consortium ya Europe wametinga na Eurofighter Typhoon yao. Russia imeleta Su-35 na Mig-35 zao ila hazipewi nafasi kubwa ingawa ndio zina bei ndogo zaidi.
India wana ndege za Urusi nyingi na wanaachana nazo taratibu, hata hii stealth Su-57 walianza nayo kipindi inaitwa PAK FA ila wakajiondoa baada ya gharama kupanda, specs kuwa tofauti na delays, wakaiacha Russia yenyewe. Mwaka 2019 waliagiza Dassault Rafales 36 baada ya mgogoro wa mpakani na China kwenye eneo la Ladakh. Kwanini hawakuongezea idadi ya Su-30MKI tena ambazo Hindustan pale India inaweza tengeneza components nyingi kulingana na mkataba maana MKI ni modification ya India tu. Rafale inapewa nafasi kubwa zaidi
India mwaka huu wamepiga chini mkataba wa kuongeza Kamov Ka-31 helicopters 10 za Urusi kwa ajili ya Navy yao, wakati huo procurement ya helicopters za Marekani inafanyiwa kazi. Kati ya ndege 114 hizo za future program India wanataka navy jet kwa ajili ya aircraft carrier yao. Kwahiyo hapo Russia hana chake, hapo kuna contenders wawili: Dassault Rafale na Boeing Super Hornet.
Tuachane na India ambayo ndio top Russian weapons importer duniani, twende kwa Egypt ambayo ndio top Russian weapons importer in Africa na Middle East, na wana ndege aina nyingi sana wanachanganya hawa sijui huwa wanawezaje maintenance. Egypt wana Rafales baada ya kuzipima dhidi ya Mig-29 wakagundua Mig-29 (ambazo waliagiza ziwe modified zije Mig-35 ila wakapewa Mig-29M2) na PESA radar yake haizidi Rafale. Na wamepunguza order quantity ilimradi wasivunje mkataba waliosaini 2018 kununua Su-35.
Indonesia mwaka jana iliachana na ndoto za Sukhoi wakati ilishatenga hela ikachukua Boeing F-15 kwa sababu hiyohiyo ya PESA radar kwenye karne hii.
Algeria ambayo ni ya pili kwa kununua silaha za Urusi hapa Afrika imeachana na Su-35 kisa PESA radar mwaka huu huu. Watu wanataka AESA wewe unawaletea Erbis-E radar ambayo ni PESA leo 2022 wanunua ndege wakae nazo miaka 30, wakitaka modifications uwapige hela tena.
Mikoyan ilianza hivihivi haifanyi investment kwenye modifications na new weapons systems, sasa naona na Sukhoi inaelekea ukouko. Hao wanunuaji wa hizo silaha wako wapi?
Kwanza nani kaona St. Petersburg Economic Forum iliyofunguliwa leo? Hawa team Moscow ukute hawajui hata uwepo wake wakati ndio Davos ya Urusi, viongozi waliokuwepo leo ni kina Armenia, Kazakhastan, Belarus na Mtaliban alikuwepo. Uache biashara na Canada ukafanye na Taliban si utaishia kuwauzia majambia