Nisamehe mkuu lakini umeleta mfano usio na uhusiano wa vita ya Ukraine. Urusi ilipata wateja tangu miaka mingi kati ya nchi ambazo hazina pesa au ambazo hazitaki kutumia pesa nyingi mno. Kumpata Uturuki kulikuwa nafasi ya pekee kutoboa mstari wa ulinzi wa NATO - maana mfumo wa S 400 hautatumiwa kupiga ndege za Kirusi.
Kwa nini Waturuki walinunua? Sababu si ubora wa SS 400 juu ya mifumo mingine, sababu ni siasa. Erdogan alikasirika kuhusu Marekani kulinda Waislamu wa Gülen ambao anawashtaki kuwa magaidi.
Swali langu lilikuwa hii: kama ninakuelewa vema, unafikiri kwamba nchi nyingi zinanunua sasa silaha za Urusi kutokana na ubora ulionekana Ukraine. Hapo niliomba ulete mifano na takwimu.
Kinyume siamini ni kweli. Hakuna silaha bora za Urusi kushinda nchi za NATO (kifaru bora walichotengeneza Armata 14, haiko hali halisi kwa sababu walishindwa kutenegeneza idadi ya maana).
Hasa silaha ambazo zinatumia tekinolojia ya kisasa kabisa, kuna matatizo kwa sababu walitegemea vipuli kutoka nje - ambazo hazifiki tena kwa urahisi kutokana na vikwazo. Hapa tunaona wanatumia mara kwa mara makombora ya zamani hivyo wana matatizo ya kulenga vema (mfano ile supameket waliyopiga, badala ya kiwando kando lake).