SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

Dah!!! Ajali za barabarani ni janga kuu kwa taifa, pole sana kwa wafiwa hakika maisha ya mwanadamu ni mafupi na yasiyotabirika

NB: ijapokuwa ajali hutokea ulimwenguni pote lakini katika nchi yetu ukiacha overtaking maeneo yasiyo sahihi pia miundombinu ni changamoto kuu barabara finyu, mashimo mengi...

Mungu atupe mwisho ulio mwema

😭😭😭😭😭
 
Serikali ikisema madereva wakatwe point, wanatishia kugoma.lakin ukweli ni kua madereva wasasa hawana umakini, haswa hawa wamalori, mtu anaendsha gar ameshakula dabo Kiki, na anasaga mrungi. Unadhan ataheshimu sheria? Pili anajua mweupe akimshika anamdakiza buku mbili bhasi. Acha watuue
 
Mnazungumzia askari gani wakati na wao watatu wamekufa na hawasemi ni uzembe wa nani. Tunawajua askari wakiwa barabarani wanavyoendesha utafikiri wao wana miili ya chuma, wanaovateki hovyo wakiamini magari yatawapisha hata km hakuna uwezekano, mtu mweusi ni km nyani tu hakuna ustaarabu ht kidogo.
 
Jeshi la Polisi Waanzishe kikosi cha kukagua mwendokasi wa madereva, kuondoa magari yaliyoharibika barabarani, na mtu gari likiharibika atakiwe kisheria mbali ya kuweka triangle au majani barabarani basi mwenye chombo atakiwe kupiga simu kwa polisi patrol kuliondoa haraka barabarani au kikosi cha patrol wafike haraka kuliondoa na kumtoza gharama ya kulivuta / kukiondoa chombo kilichoharibika barabarani.


Hata kama polisi wakifanya patrol lakini hawawezi kuwa kila sehemu gari ilipoharibika kwa wakati. Gari inapoharibika, dakika tano tu ni muhimu sana.
Tujiulize nchi zilizoendelea kama za Marekani ya Kaskazini, Ulaya, Japan, Australia na China kwa kuzitaja kwa uchache wana vikosi vya doria vya usalama wa njia kuu / highway patrol iwe vipi nchi ya Tanzania ishindwe na kukosa kuona umuhimu wa kikosi cha doria cha usalama wa barabara kuu ?

Bonus Scene : Always On Patrol I Heavy Rescue : 401

Law enforcement on the 400 series highways is a massive task. The Ontario Provincial Police responds to calls big and small - all of them vital to making the highways safer.
Source : Discovery Canada
 
Mkoa wa Morogoro & Pwani!RPC NA RTO wanastahili ,kupangiwa majukumu mengine!
Askari hawako serious hata kidogo!
.... Kiongozi, hebu fafanua kidogo kwa muktadha wa ajali ya basi na lori, polisi walipaswa kufanya nini kwa mfano ili kuzuia hiyo ajali isitokee? Unless unazungumzia mambo mengine kwa ujumla wake.
 
Changamoto

MWENYEZI MUNGU uwaguse wengine wasiangukie kwenye ajali kama hizi
 
.... Kiongozi, hebu fafanua kidogo kwa muktadha wa ajali ya basi na lori, polisi walipaswa kufanya nini kwa mfano ili kuzuia hiyo ajali isitokee? Unless unazungumzia mambo mengine kwa ujumla wake.
Naunga mkono hoja. Sijui kama alitaka hao Mapolisi wakaendeshe hayo magari? Huo ni uonevu.
 
1. Miundombinu sahihi.
2. Kufuata sheria za barabarani.
3. Kuhakikisha vyombo vya usafiri viko katika hali inayotakiwa.
4. Kuwa na askari wa usalama barabarani wanaotimiza wajibu wao.
5. Matumizi ya teknolojia eg kamera za usalama, vifaa vya kugundua kama dereva ametumia pombe etc.
 
Reactions: Lax
Polisi wa Tanzania wawe na weledi kama huu mkuu??.
 
Naunga mkono hoja. Sijui kama alitaka hao Mapolisi wakaendeshe hayo magari? Huo ni uonevu.
May be polisi wajipange njia nzima kila baada ya hatua 10 pande zote za barabara all the way from Dar to Mbeya; 24/7.
 
Changamoto

MWENYEZI MUNGU uwaguse wengine wasiangukie kwenye ajali kama hizi
Mungu afanye nini mkuu?. Atujengee barabara nzuri?. Atushike mikono tusiendeshe vibaya?. Aturekebishie magari yetu mabovu ?. Wajibu wetu tusimpe Mungu jamani, kashatupa akili tuzitumie.
 
Tatizo unashangaa hilo suala la kukatwa point linachukuliwa kama chanzo cha rushwa, ukikataa kutoa rushwa unakatwa point na huna pa kushtaki. Nchi wanazokata point askari hachukui rushwa wala haonei mtu, unakatwa kihalali.
 
Wanaosimamia usalama ndio wanaokufa kwa ajali
Ajali zingine za kulazimisha
 
Reactions: Lax
May be polisi wajipange njia nzima kila baada ya hatua 10 pande zote za barabara all the way from Dar to Mbeya; 24/7.
Hata wakijipanga, bado hio sio suluhisho. Kwanza Polisi wenyewe ni wadau wa Ajali barabarani -unakumbuka juzi Senkenke?. Halafu tena Moro - Dom hapo kwenye tukio si wameRIP polisi watatu?
Dereva anaendesha gari huku ana visungura kichwani, Kajifukiza jani pendwa, anastress za familia au anasinzia kwenye uskani halafu eti ajali haina kinga!!!. Kuzilaumu barabara haina mashiko kwa hoja kwamba kwani huyo dereva ni yeye tu amepita hapo?
Kuilaumu serikali napo bado sio hoja ya msingi sana kwa sababu Dereva amesomea kazi hiyo na kupewa leseni.Hizo alama za barabarani ni visaidizi tu.
 
Namba 3 hapo hujui kama gari inaweza kufeli break mkuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…