SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

1. Miundombinu sahihi.
2. Kufuata sheria za barabarani.
3. Kuhakikisha vyombo vya usafiri viko katika hali inayotakiwa.
4. Kuwa na askari wa usalama barabarani wanaotimiza wajibu wao.
5. Matumizi ya teknolojia eg kamera za usalama, vifaa vya kugundua kama dereva ametumia pombe etc.
Solution ni moja tu four lanes basi
 
Hata wakijipanga, bado hio sio suluhisho. Kwanza Polisi wenyewe ni wadau wa Ajali barabarani -unakumbuka juzi Senkenke?. Halafu tena Moro - Dom hapo kwenye tukio si wameRIP polisi watatu?
Dereva anaendesha gari huku ana visungura kichwani, Kajifukiza jani pendwa, anastress za familia au anasinzia kwenye uskani halafu eti ajali haina kinga!!!. Kuzilaumu barabara haina mashiko kwa hoja kwamba kwani huyo dereva ni yeye tu amepita hapo?
Kuilaumu serikali napo bado sio hoja ya msingi sana kwa sababu Dereva amesomea kazi hiyo na kupewa leseni.Hizo alama za barabarani ni visaidizi tu.
Mkuu, serikali ikichukua hatua,ajali zitap
Namba 3 hapo hujui kama gari inaweza kufeli break mkuu...
Ifeli hata kama gari ilikuwa imara na haina shida yoyote na limefanyiwa maintenance ipasavyo?
 
MORO AGAIN.
Chanzo Cha ajali dereva wa Lori kutaka kuya ova take magari yaliyopo mbele yake.
Wakikataa point wanalalamika.
Sina huruma na madereva
 
ajali nyingi kwa nchi kama zetu, miundo mbinu, uzembe na rushwa ni sababu kuu za ajali,
hivyo kwa nchi zilizoweka mkazo kwenye hayo mambo, wana afadhari sana kuliko sisi,...
Sawa mkuu
 
Hata wakijipanga, bado hio sio suluhisho. Kwanza Polisi wenyewe ni wadau wa Ajali barabarani -unakumbuka juzi Senkenke?. Halafu tena Moro - Dom hapo kwenye tukio si wameRIP polisi watatu?
Dereva anaendesha gari huku ana visungura kichwani, Kajifukiza jani pendwa, anastress za familia au anasinzia kwenye uskani halafu eti ajali haina kinga!!!. Kuzilaumu barabara haina mashiko kwa hoja kwamba kwani huyo dereva ni yeye tu amepita hapo?
Kuilaumu serikali napo bado sio hoja ya msingi sana kwa sababu Dereva amesomea kazi hiyo na kupewa leseni.Hizo alama za barabarani ni visaidizi tu.
Serikali inahusika mkuu,,mfano sijawahi kuona dereva hapa Bongo wanapimwa kujua kama wametumia pombe au madawa yanayoweza kuvuruga ufahamu wao. Je wangekuwa wanapimwa ajali ngapi zingepungua?. Barabarani kuwe na kamera ukifanya kosa mwanzoni kabisa unanaswa kabla hujasababisha ajali,ajali ngapi tungezuia?. Miundombinu iwe mizuri ajali ngapi tungezuia?. Haya yote ni wajibu wa serikali na haiwezi kukwepa lawama.
 
Mkoa wa Morogoro na Taifa tumekumbwa na simanzi kubwa kufuatia ajali mbili mbaya za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Oktoba 9, 2026, na kusababisha vifo vya jumla ya watu 32 na majeruhi zaidi ya 37.

Ajali ya kwanza na yenye maafa makubwa zaidi ilitokea majira ya saa 4:30 usiku huko Mkambarani kwenye barabara ya kuelekea Dar es Salaam, ikihusisha basi la abiria la kampuni ya Drim Line (T 672 DLT) lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya na lori la Scania (T 902 EGN) lililobeba mbao. Magari hayo yaligongana uso kwa uso na kuwaka moto mkubwa ulioteketeza miili ya marehemu, ambapo watu 28 walipoteza maisha (abiria 27 wa basi na mtu mmoja kwenye lori) huku watu 37 wakijeruhiwa vibaya kwa moto na fractures na kukimbizwa hospitalini baada ya uokoaji wa usiku kucha uliohusisha vikosi vya Zimamoto.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi unaonyesha ajali hii ilisababishwa na uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine bila tahadhari.

Ajali ya pili ilitokea mapema kidogo majira ya saa 12:45 jioni ya Alhamisi huko Miti Bora, Dumila (Wilaya ya Mvomero) kwenye barabara kuu ya kuelekea Dodoma, ambapo gari la Jeshi la Polisi lililokuwa na askari waliokuwa doria liligongana na lori lingine la Scania. Ajali hii ilisababisha vifo vya watu 4, wakiwemo askari polisi watatu na raia mmoja, huku askari wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Kwa sasa, majeruhi wote wanapatiwa matibabu ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Andrew Kantimbo, akitoa wito wa tahadhari kwa madereva huku uchunguzi zaidi wa kisheria ukiendelea.

Ningeishauri serikali ijenge barabara ya malori tu malori yawe yanapita huko sio mchanganyiko hapo morogoro malori ni mengi sana kosakosa za kutosha nashukuru Mungu mimi bado mzima
 
Na zaidi ya hapo. Gari likiwa bovu likapinduka hapo four lanes inazuiaje?
Gari likiwa bovu hakuwezi kusababisha likapinduka hata siku moja! Ila uendeshaji mbaya unaweza kusababisha likapinduka

Sasa gari lina breki tia maji tia maji unaenda mwendo wa kishandu unategemea nini?

Ajali za Tanzania nyingi ni za uso kwa uso au gari moja kulikwepa lingine kutokana na overtaking ya hatari na kujikuta lipo porini chali
 
Mkuu, serikali ikichukua hatua,ajali zitap
Serikali ilishachukua hatua na bado itaendelea kuchukua hatua zaidi matumizi ya tochi, matumizi ya kubaini ulevi, Ukaguzi wa magari, magari kuweka speed governors n.k. n.k. Lakini liacha ya juhudi zote hizo ajali ndo kwanza zimeshamiri ikiwa ni pamoja na malalamiko kutoka kwa wasafiri na madereva. Cjui waTz wanataka wabebwe kwa mbeleko gani.

feli hata kama gari ilikuwa imara na haina shida yoyote na limefanyiwa maintenance ipasavyo?
 
Ningeishauri serikali ijenge barabara ya malori tu malori yawe yanapita huko sio mchanganyiko hapo morogoro malori ni mengi sana kosakosa za kutosha nashukuru Mungu mimi bado mzima
199532.webp

Hii ni Texas hawana njia ya malori peke yake jiulize hapa ajali ya uso kwa uso inawezekana vipi kutokea?
 
Gari likiwa bovu hakuwezi kusababisha likapinduka hata siku moja! Ila uendeshaji mbaya unaweza kusababisha likapinduka

Sasa gari lina breki tia maji tia maji unaenda mwendo wa kishandu unategemea nini?

Ajali za Tanzania nyingi ni za uso kwa uso au gari moja kulikwepa lingine kutokana na overtaking ya hatari na kujikuta lipo porini chali
Breki tia maji tia maji ndo ubovu wenyewe wa magari naosemea.
 
Serikali ilishachukua hatua na bado itaendelea kuchukua hatua zaidi matumizi ya tochi, matumizi ya kubaini ulevi, Ukaguzi wa magari, magari kuweka speed governors n.k. n.k. Lakini liacha ya juhudi zote hizo ajali ndo kwanza zimeshamiri ikiwa ni pamoja na malalamiko kutoka kwa wasafiri na madereva. Cjui waTz wanataka wabebwe kwa mbeleko gani.
Mkuu, serikali imechukua hatua zipi kama hatua ya muhimu zaidi ya kuweka miundombinu mizuri hadi sasahivi bado haijafanyika??. Barabara ya Singida -Arusha imejaa mashimo kama madimbwi halafu unasema serikali imechukua hatua??.
 
Back
Top Bottom