SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

Kuna picha imetumwa hapa ya barabara za Texas, tuwe nazo kama hizo.
Mtasema wale wameendelea sana hizi hapa kenya yani kutoka Nairobi hadi Kiambu kuna njia ya hivi
199533.jpg

Hii picha imepigwa na Kenya Roads hapa ni kiambu wanatanua zaidi hii barabara kutoka njia sita unazoziona kuwa nane
 
Breki tia maji tia maji ndo ubovu wenyewe wa magari naosemea.
Umewahi kuwa dereva?
Dereva anaweza kutoka na gari Tunduma hadi kwa mafundi wa malori Mikumi akiwa na breki hafifu mno

Ungekuwa umewahi kuishi Tanangozi au Ilula hizi zingekuwa sio story zako maana ni maisha ambayo ungeishi

Mwendo kasi, overtaking kwenye hivi vibarabara viwili, humps, na ubovu wa barabara zilizo nyingi ndio chanzo cha ajali mengine majaliwa tu
 
Huo udhaifu wa trafiki nani anashughulikia? Sio serikali ?.
Uko sahihi - ni Serikali. Serikali unao wajibu wa kuwasimamia Watumishi wa Umma ili watekeleze majukumu yao ipasavyo na kwa usahihi.
Na unaposema tulinganishe barabara za kijijini unachekesha mkuu. Yaani tulinganishe kibovu na kibovu zaidi ili tujipe moyo kwamba tuko vizuri.
Sichekeshi mkuu. Ninyi mlioko huko Tanzania mnashindwa kututambua na sisi tulioko huku Tanganyika yan ni kama kusema aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Tulicho nacho huku ndicho tunachweza kukitumia na kukilinganisha na kwengine. Ninyi msisahau hii nchi ni yetu sote na matamanio ya uwepo wa barabara nzuri zaidi na zaidi ni yetu sote. Serikali ndo hiyo tunaijua sote.
Tanzania barabara ni za hovyooo kuliko neno hovyo lenyewe. Na hata huko kijijini barabara zilitakiwa ziwe za kueleweka,hakuna sababu inayohalalisha wananchi wa kijijini kuwa na barabara za hovyoo.
Naam! Comparatively, Nchini Tz, barabara za vijijini ni mbovu mno ukilinganisha na zile za maeneo ya mijini. Ingelipendeza zaidi barabara za vijijini kuimarishwa kwanza kabla ya zile za mijini ili kuweka walau uwiano ulio
sawa.
 
Barabara ya mji mkubwa ni nyembamba ajali zitaendelea kutokea tu kwa wingi hadi mkikibali uhalisia.

Barabara nyembamba humo humo SUV, malori , mabasi n.k unategemea nini.
 
Umewahi kuwa dereva?
Dereva anaweza kutoka na gari Tunduma hadi kwa mafundi wa malori Mikumi akiwa na breki hafifu mno

Ungekuwa umewahi kuishi Tanangozi au Ilula hizi zingekuwa sio story zako maana ni maisha ambayo ungeishi

Mwendo kasi, overtaking kwenye hivi vibarabara viwili, humps, na ubovu wa barabara zilizo nyingi ndio chanzo cha ajali mengine majaliwa tu
Mkuu, hayo mazoea eti" unaweza kutoka hapa hadi hapa ukiwa na breki mbovu mnoo" ndo yanaleta ajali. Hata huyu dereva wa lori sio mara yake ya kwanza kuovertake sehemu ya hivyo, ila kwa sababu ni mazoea alijipa moyo na matokeo yake ndo ajali. Na usisahau ile ajalai iliyotokea Sekenke hivi karibuni chanzo ilikuwa breki kufeli. Hata hapa tunavyoongea kuna dereva anafanya kosa barabarani kimazoea na ajali haitokei. Tukitaka usalama,lazima tufuate sheria zote sio kupotezea zile ambazo zinaleta ajali chache.
 
Uko sahihi - ni Serikali. Serikali unao wajibu wa kuwasimamia Watumishi wa Umma ili watekeleze majukumu yao ipasavyo na kwa usahihi.

Sichekeshi mkuu. Ninyi mlioko huko Tanzania mnashindwa kututambua na sisi tulioko huku Tanganyika yan ni kama kusema aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Tulicho nacho huku ndicho tunachweza kukitumia na kukilinganisha na kwengine. Ninyi msisahau hii nchi ni yetu sote na matamanio ya uwepo wa barabara nzuri zaidi na zaidi ni yetu sote. Serikali ndo hiyo tunaijua sote.

Naam! Comparatively, Nchini Tz, barabara za vijijini ni mbovu mno ukilinganisha na zile za maeneo ya mijini. Ingelipendeza zaidi barabara za vijijini kuimarishwa kwanza kabla ya zile za mijini ili kuweka walau uwiano ulio
sawa.
Basi mkuu tusiseme barabara hizi ni nzuri hizi ni mbaya, barabara zote ni mbaya hakuna za kueleweka sio mjini sio kijijini.
 
Ume reply tu ama kuna kitu ulitaka kukirekebisha maana sioni hoja yako
Hoja yangu ni kukereka kwa kusema ni Ukoloni i.e. we didn't have a choice tulipangiwa na kama ni lawama basi zielekezwe kwa wakoloni ilhali kama taifa tuna umri wa 65 yrs tuko huru kufanya yetu kama tutakavyo lakini bado tunawatamka Wakoloni.
 
Basi mkuu tusiseme barabara hizi ni nzuri hizi ni mbaya, barabara zote ni mbaya hakuna za kueleweka sio mjini sio kijijini.
Ni kweli kama tukiweka kipimio(Yard stick) kimoja. Sisi humu ndani tujue tu kwamba kwa hoja ya barabara; tunazidiana tu kwa viwango vya ubaya/ubovu
 
Hii Kali,bus kusababjshiwa ajali na Lori maana tumezoea kinyume chake.

Ajali za uso kwa uso wakati wa ku-overtake ndiyo huwa mbaya zaidi sababu dereva unakuwa unaamini bado inawezekana kutoboa hivyo unazidi kukanyaga mafuta unajikuta kisahani umekifuta ndiyo unaumana.

NB:Majeruhi walioungua kutoboa ni majaaliwa kwa uzoefu tulioupata kutokea ajali ya Lori la mafuta pale Msamvu.
 
Mkuu, hayo mazoea eti" unaweza kutoka hapa hadi hapa ukiwa na breki mbovu mnoo" ndo yanaleta ajali. Hata huyu dereva wa lori sio mara yake ya kwanza kuovertake sehemu ya hivyo, ila kwa sababu ni mazoea alijipa moyo na matokeo yake ndo ajali.
ku overtake ni mazoea au ni sheria yani unafundishwa kabisa ku overtake na unapewa sheria?

ndio maana nilikuuliza wewe ni dereva au la! 😃
Na usisahau ile ajalai iliyotokea Sekenke hivi karibuni chanzo ilikuwa breki kufeli. Hata hapa tunavyoongea kuna dereva anafanya kosa barabarani kimazoea na ajali haitokei. Tukitaka usalama,lazima tufuate sheria zote sio kupotezea zile ambazo zinaleta ajali chache.
Kufeli breki hakusababishwi na ubovu wa gari, gari lako unaweza kulinunua leo hii na likafeli breki.

Kuna sababu kadhaa za kwanini breki hufeli mojawapo ni kuzidisha uzito, components za breki kupata joto kushinda uwezo wake, mfumo wa hewa wa gari n.k
 
Barabara ya morogoro ina malori hatari mabasi yenye route ndefu yanapata tabu sana kwenye barabara hiyo
 
Back
Top Bottom