SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

Hata kuendesha magari tuliiga kwao,sisi ilikuwa ni miguu tu
Wao upande wa dereva ni kushoto sisi ni kulia wapi na wapi cha kufanya iwe hivyo wajenge barabara ya malori tu kuipusha ajali kama hizo moro inaogoza kwa ajari zinazohusisha malori na hio ndio sababu kuu malori yanapita njia moja na magari ya kawaida msongamano mkubwa sana
 
Serikali inahusika mkuu,,mfano sijawahi kuona dereva hapa Bongo wanapimwa kujua kama wametumia pombe au madawa yanayoweza kuvuruga ufahamu wao. Je wangekuwa wanapimwa ajali ngapi zingepungua?. Barabarani kuwe na kamera ukifanya kosa mwanzoni kabisa unanaswa kabla hujasababisha ajali,ajali ngapi tungezuia?. Miundombinu iwe mizuri ajali ngapi tungezuia?. Haya yote ni wajibu wa serikali na haiwezi kukwepa lawama.
Mkuu, unataka kuniaminisha kwamba hujaona vile vifaa ambavyo dereva hutakiwa kuvipumulia ambavyo hubaini uwepo wa matumizi ya pombe? Kuna kifaa cha speed detector, lakini pia kuna mawasiliano ya simu walkie-talkie na raia wema wanashirikishwa kutoa Taarifa kwa vyombo vya Usalama barabarani kuhusu mwenendo usioridhisha wa dereva au chombo cha moto barabarani. Zote hizo ni juhudi za Serikali lakini tuaishia kuwalaumu bodaboda na kuyafumbia macho magari ya tairi nne.
Miundo mbinu iliyopo sio mibaya kivile cha msingi ni dereva ajue kwamba miundo mbinu iliyopo si ya yeye kujiachilia lazima achukue Tahadhari muda wote akiwa barabarani.
 
Kivyetuvyetu sio lazima tuwaige wao
Umewahi kusikia project ya express eay ya Kibaha to Chalinze? Kama ndio umeanza kuisikia toka mwaka gani?

Ujenzi wa barabara mpya achilia mbali tu "Ya malori" hauwezekani Tanzagiza hadi kizazi chako cha 100

Dom to Iringa Babati to Singida Mwanza to Musoma Musoma to Sirari Dar to Mtwara kote hamna barabara na hela ya kujenga hawana
 
Mkuu, hivyo vifaa vikogo wapi? Mfano usiku watu wakiwa wanatoka kula bata, ushaona wapi dereva anasimamishwa kupima kama amaetumia pombe? Hata dereva wa private car?. Mi sijawahi kuona. Na kuhusu miundombinu usiseme sio mibaya miundombinu ni ya hovyoooooooooooo*1000.
 
Wao upande wa dereva ni kushoto sisi ni kulia wapi na wapi
upande wa kuendeshea gari ni ukoloni kama ulivyo ukoloni mwingine tulifata utaratibu wa Uingereza na uliwekwa na wao wenyewe hakuna mtanzania aliamka akasema driving side yetu ni hii
cha kufanya iwe hivyo wajenge barabara ya malori tu kuipusha ajali kama hizo moro inaogoza kwa ajari zinazohusisha malori na hio ndio sababu kuu malori yanapita njia moja na magari ya kawaida msongamano mkubwa sana
NEVER
 
Wao upande wa dereva ni kushoto sisi ni kulia wapi na wapi cha kufanya iwe hivyo wajenge barabara ya malori tu kuipusha ajali kama hizo moro inaogoza kwa ajari zinazohusisha malori na hio ndio sababu kuu malori yanapita njia moja na magari ya kawaida msongamano mkubwa sana
Kuna picha imetumwa hapa ya barabara za Texas, tuwe nazo kama hizo.
 
Umewahi kusikia project ya express eay ya Kibaha to Chalinze? Kama ndio umeanza kuisikia toka mwaka gani?

Ujenzi wa barabara mpya achilia mbali tu "Ya malori" hauwezekani Tanzagiza hadi kizazi chako cha 100

Dom to Iringa Babati to Singida Mwanza to Musoma Musoma to Sirari Dar to Mtwara kote hamna barabara na hela ya kujenga hawana
Huu ujenzi ujikite morogoro hadi dar tu maana ndio hua kuna msongamano mkubwa wa malori kutoka bandarini yakifika dodoma hua yanagawanyika yanakwenda mikoa mbalimbali
 
upande wa kuendeshea gari ni ukoloni kama ulivyo ukoloni mwingine tulifata utaratibu wa Uingereza na uliwekwa na wao wenyewe hakuna mtanzania aliamka akasema driving side yetu ni hii

NEVER
Sasa kama wanapewa imu na bado hawaelewi sheria za barabarani wajenge njia ya malori wafanye upanuzi tu waweke na taa za barabarani
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Huu ujenzi ujikite morogoro hadi dar tu maana ndio hua kuna msongamano mkubwa wa malori kutoka bandarini yakifika dodoma hua yanagawanyika yanakwenda mikoa mbalimbali
Unaijua njia ya dom hadi igunga?

Pale kuna Manyoni, Sekenke na Shelui unapajua vyema au wewe sio msafiri?
 
Wito kwa madereva hasa malori, Mabasi na Daladala mgomo wa kwanza uwe kufata sheria za barabarani, waoneshe umma changamoto zilizopo kwa kufata sheria barabarani hakuna kuwahisha watu wala mizigo wiki moja inatosha
 
Mkuu, hivyo vifaa vikogo wapi? Mfano usiku watu wakiwa wanatoka kula bata, ushaona wapi dereva anasimamishwa kupima kama amaetumia pombe? Hata dereva wa private car?. Mi sijawahi kuona.
Huo utakuwa ni udhaifu wa Polisi Traffic mtu binafsi. Ni kweli muda wa uck huwa hawaonekani mara nyingi lakini Taratibu zinawataka wawepo.
Na kuhusu miundombinu usiseme sio mibaya miundombinu ni ya hovyoooooooooooo*1000.
Inategemea unalinganisha na miundo mbinu ya wapi. Kama ukibahatika kuja huku vijijini utazifahamu barabara mbovu na zinapitisha magari makubwa yanayosomba mazao (nafaka na mifugo) na kusambaza bidhaa nyingi za biashara.
 
Huu ujenzi ujikite morogoro hadi dar tu maana ndio hua kuna msongamano mkubwa wa malori kutoka bandarini yakifika dodoma hua yanagawanyika yanakwenda mikoa mbalimbali
T1 ndio yenye msongamano mkubwa wa malori! Hivyo basi kila mkoa unaopitiwa na highway hiyo ziwekwe 4 lane.

Mkoa wa Mbeya wameshaanza kujenga, ifanyike hivyo kwa mkoa wa Morogoro, Iringa na Songwe.
 
Huo utakuwa ni udhaifu wa Polisi Traffic mtu binafsi. Ni kweli muda wa uck huwa hawaonekani mara nyingi lakini Taratibu zinawataka wawepo.

Inategemea unalinganisha na miundo mbinu ya wapi. Kama ukibahatika kuja huku vijijini utazifahamu barabara mbovu na zinapitisha magari makubwa yanayosomba mazao (nafaka na mifugo) na kusambaza bidhaa nyingi za biashara.
Huo udhaifu wa trafiki nani anashughulikia? Sio serikali ?. Na unaposema tulinganishe barabara za kijijini unachekesha mkuu. Yaani tulinganishe kibovu na kibovu zaidi ili tujipe moyo kwamba tuko vizuri. Tanzania barabara ni za hovyooo kuliko neno hovyo lenyewe. Na hata huko kijijini barabara zilitakiwa ziwe za kueleweka,hakuna sababu inayohalalisha wananchi wa kijijini kuwa na barabara hazijulikani zimetoka sayari gani.
 
Halafu points zikitakiwa kukatwa wanaweka mgomo
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mkoa wa Morogoro na Taifa tumekumbwa na simanzi kubwa kufuatia ajali mbili mbaya za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Oktoba 9, 2026, na kusababisha vifo vya jumla ya watu 32 na majeruhi zaidi ya 37.

Ajali ya kwanza na yenye maafa makubwa zaidi ilitokea majira ya saa 4:30 usiku huko Mkambarani kwenye barabara ya kuelekea Dar es Salaam, ikihusisha basi la abiria la kampuni ya Drim Line (T 672 DLT) lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya na lori la Scania (T 902 EGN) lililobeba mbao. Magari hayo yaligongana uso kwa uso na kuwaka moto mkubwa ulioteketeza miili ya marehemu, ambapo watu 28 walipoteza maisha (abiria 27 wa basi na mtu mmoja kwenye lori) huku watu 37 wakijeruhiwa vibaya kwa moto na fractures na kukimbizwa hospitalini baada ya uokoaji wa usiku kucha uliohusisha vikosi vya Zimamoto.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi unaonyesha ajali hii ilisababishwa na uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine bila tahadhari.

Ajali ya pili ilitokea mapema kidogo majira ya saa 12:45 jioni ya Alhamisi huko Miti Bora, Dumila (Wilaya ya Mvomero) kwenye barabara kuu ya kuelekea Dodoma, ambapo gari la Jeshi la Polisi lililokuwa na askari waliokuwa doria liligongana na lori lingine la Scania. Ajali hii ilisababisha vifo vya watu 4, wakiwemo askari polisi watatu na raia mmoja, huku askari wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Kwa sasa, majeruhi wote wanapatiwa matibabu ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Andrew Kantimbo, akitoa wito wa tahadhari kwa madereva huku uchunguzi zaidi wa kisheria ukiendelea.

Kuna haja ya Serikali kufikilia upya juu ya ruhusa yao ya route za usiku haya Ma bus ya habiria aise.
 
Back
Top Bottom