Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 14,421
- 30,962
duh... ajali haina kinga mkuu
Misemo ya kijinga hii.
duh... ajali haina kinga mkuu
Mfano kwenye hiyo ajali polisi walipokea rushwa kutoka kwa dereva wa gari lipi?Hao Polisi wawe na weledi kwanza, waache kupokea rushwa na kuonea watu then ndo tuongee.
Inasikitisha sana, masikini wanakufa vifo vibaya sana kwa sababu hawawezi kupanda ndege au SGR.
hakuna maandalizi dhidi ya kifo,....Kila mtu ajiandae
Hahahhhhh tuendelee kuchukua tahadhari mkuu.Misemo ya kijinga hii.
Be prepared..knowing anytime unaweza kwenda.ni kujiandaa Kwa lolotehakuna maandalizi dhidi ya kifo,....
let say nakufa kesho,...nijiandae na nn??Be prepared..knowing anytime unaweza kwenda.ni kujiandaa Kwa lolote
Inasikitisha sana.Mkoa wa Morogoro na Taifa tumekumbwa na simanzi kubwa kufuatia ajali mbili mbaya za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Oktoba 9, 2026, na kusababisha vifo vya jumla ya watu 32 na majeruhi zaidi ya 37.
Ajali ya kwanza na yenye maafa makubwa zaidi ilitokea majira ya saa 4:30 usiku huko Mkambarani kwenye barabara ya kuelekea Dar es Salaam, ikihusisha basi la abiria la kampuni ya Drim Line (T 672 DLT) lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya na lori la Scania (T 902 EGN) lililobeba mbao. Magari hayo yaligongana uso kwa uso na kuwaka moto mkubwa ulioteketeza miili ya marehemu, ambapo watu 28 walipoteza maisha (abiria 27 wa basi na mtu mmoja kwenye lori) huku watu 37 wakijeruhiwa vibaya kwa moto na fractures na kukimbizwa hospitalini baada ya uokoaji wa usiku kucha uliohusisha vikosi vya Zimamoto.
Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi unaonyesha ajali hii ilisababishwa na uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine bila tahadhari.
Ajali ya pili ilitokea mapema kidogo majira ya saa 12:45 jioni ya Alhamisi huko Miti Bora, Dumila (Wilaya ya Mvomero) kwenye barabara kuu ya kuelekea Dodoma, ambapo gari la Jeshi la Polisi lililokuwa na askari waliokuwa doria liligongana na lori lingine la Scania. Ajali hii ilisababisha vifo vya watu 4, wakiwemo askari polisi watatu na raia mmoja, huku askari wengine kadhaa wakijeruhiwa.
Kwa sasa, majeruhi wote wanapatiwa matibabu ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Andrew Kantimbo, akitoa wito wa tahadhari kwa madereva huku uchunguzi zaidi wa kisheria ukiendelea.
Sikuwepo mkuu,siwezi kujua. Ila huwa tunawaona madereva wanavyopokea rushwa tena kuna wakati wanalazimisha, wanaona ni haki yao,usipotoa unaandikiwa faini na huna pa kushtaki.Mfano kwenye hiyo ajali polisi walipokea rushwa kutoka kwa dereva wa gari lipi?
Hivi hizi ajali ni mpaka nchi zingine ni hivi 😢
Una watoto?let say nakufa kesho,...nijiandae na nn??
Hiyo serikali ingekuwa kweli ina nia ya kupunguza ajali ingejenga kwanza barabara za kueleweka sio huu uozo tunaouita barabara.nini kitafanyaika sasa? serikali wakitaka kujaribu kuzipuguza kwa kuwabana madereva kwamba warudi shuleni wanagoma na watanzagiza wanawasapoti maderava against askari br. wengine wakishikwa wanakataa wanaanza kuwashambilia askari kwa mangumi kwamba wao ni "madaktari bingwa" na hawapswi kuguswa na "form 4 failure" i.e police.
ni ngumu sana, dereva wa basi wa tanzagita analalamika kwamba akitoka dar-kgm leseni yake itakuwa imeshajaa points hivyo ni lazima serikali wawarudishie points zao na anatetewa na watanzagiza mpaka siku unaenda zako likizo na familia yako unaendesha kwa kufwata sheria basi au lori inaovertake na kukandamiza na kuua familia nzima halafu tunarudi hapa kuuliza maswali magumu tena ...
Madereva hawawezi kujisimamia hata siku moja, wana ujinga mwingi sana barabarani..!!Mara wanalalamika polisi wengi barabarani
Wakiachwa tena wanalalamikiwa askari kuwa hawawasimamii yaani.