SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

Ukisikiliza maelezo ya mashuhuda lawama zote kwa dereva wa lori kuingia upande usio wake, sasa basi kwa maana hiyo

Kwanza madereva wahojiwapewe elimu lakini pia licha ya ubovu wa bara bara, barabara nyingi tz ni ndogo mno yaani nyembamba. Isipokuwa zile za kuingia baaadhi ya miji
ni kweli mkuu,... miundo mbinu yetu ni mibovu na uzembe juu,...lazima ajali zitumalize
 
  • Thanks
Reactions: Lax
unaona sasa na hapo ndipo shida ilipo, linapokuja swala la usalama hakupaswi kuzungumzika kwani it cost life bali inapswa kuwa ni amri ambayo kila dereva afwate, ubovu wa br siyo chanzo kikuu cha ajali tanzagiza, chanzo kikuu ni low iq, kiburi pmj na umimi, sehemu kubwa ya madereva hawazijui sheria ya br. let alone hata kuzifwata na kwa kuwa mna kiburi ni swala la muda kabla kila mtu hajafikiwa pia na hawa ma-low iq drivers br. siku umekaa kijiweni unapata moja baridi lori la mchanga linaacha njia linazoa kila kitu na kila mtu wote tutaangamia sababu ya kiburi na jeuri ...
Ha ha ha nacheka kwenye msiba! Jana nimeona truck semi trailer hapo ALI Mwinyi road limeacha njia limeingia fence ya chuo cha ustawi wa jamii hadi ndani!
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Ni majonzi kupoteza wapendwa wetu kila siku kutokana na ajali za mara kwa mara za barabarani

Ni wito wangu kwa madereva wote kuongeza umakini wawapo barabarani

Ajali za barabarani tunaweza kuzipunguza kama sio kuzimaliza kabisa iwapo kila mmoja wetu ataheshimu alama za barabarani na kuendesha kwa tahadhari

Mungu awape uponyaji wa haraka majeruhi wote na azipumzishe roho za marehemu wetu mahali pema 🙏🙏🙏
 
  • Thanks
Reactions: Lax
75% ya ajali Tz ni uzembe wa madereva.

hata zaidi ya hapo kwanza halafu kingine ni kiburi, ujuaji na "unajua mimi ni nani" syndrome plus kuna serikali ambayo inataka kumfurahisha kila mtu badala ya kufanya mambo sahihi ili kuokoa maisha ya watu, uamuzi sahihi kwa siku zote huwa unpopular lkn kama unataka kufanya maamuizi kwa kusikiliza emotions za watu hawawezi kuongoza nchi na kutatua matatizo ya watu na ndicho kinachoendelea tanzagiza.

juzi kati waziri mzima mwenye dhamana ya usalama wa raia anakwenda kupoteza muda kuwa lectured n low iq driver ambaye anakataa point system kwamba arudishiwe points zake wakati points alipewa kwa kuvunja sheria za br. lkn anagoma na anatetewa na watanzagiza lkn likija kutokea la kutokea wanaanza kushangaa tumefikaje hapa, utasikia jamani ajali zitatumaliza, yeah zitamaliza watu ndiyo ...
 
Wkati Serikali inatengeneza kanununi kuwabana madereva waligoma na mkawashangilia na kuwapongeza mkiwaunga mkono kukataa kubanwa, haya sasa hata mwezi bado wameshaanza kuuwa abiria
Ni vile hujaona ule msululu wa magari katika barabara ya morogoro au unafanya kusudi au waleta ushabiki au vyote kwa pamoja

Malori hiyo barabara ni mengi sana na barabara ni njia moja kwa kila upande kama wa mbele akienda kwa speed ya 20km/h hapo utaunga tera hadi mnafika maana hamna hata nafasi ya ku-overtake

Nahisi nguvu tungezielekeza kwa serikali waweke barabara mbadala ya malori
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Wote mnaowalaumu madereva hasa kwa njia ya moro bado hamjasafiri na bus kwenda mikoani au kuja dar msululu ni mkubwa sana

Siku nimesafiri na new force Yani ili kidogo itembee walau ikabidi ipitie njia mbadala ya vumbi lakini njia kuu haipitiki ni mwendo wa malori mwanzo mwisho

Ni kweli madereva wanakuwaga na makosa ila hiyo route ni changamoto aisee
 
chanzo kikuu cha ajali tanzagiza wala siyo ubovu wa br. bali ni madereva ambao hawaelewi/hawataki kuheshimu sheria za br. aidha hawazijui au wanazipuuzia, pili kiburi, ujeuri na umimi kila mtu mjuaji akisimamishwa na askari anarusha ngumi kafanya kosa lkn hakubali, tatu low iq wanashindwa kuelewa logic ya askari kujificha kwenye kichaka kurekodi mwendo wa gari, wanataka askari akae mahali ambapo watamuona ila pale ambapo hawamuoni hawataki ajifiche sasa hiyo ni low iq na sehemu ndooogo saaana ndiyo labda br. lkn siyo chanzo kikubwa, chanzo kikubwa ni kiburi, umimi na low iq ya wanotumia br. ...
Mkuu, barabara zingekuwa nzuri hizo ajali zingepungua sana. Mfano barabara zingekuwa zimetenganishwa kwa namna ambayo magari ya upande mmoja na upande mwingine hayakutani hata iweje, hata dereva aweje,ajali za magari kugongana uso kwa uso ambazo ndo nyingi zisingekuwepo. Hata hii ajali iliyotokea leo isingetokea. Nchi ambazo madereva ni wastaarabu bado wamejenga barabara ambazo magari ya upande mmoja na upande mwingine hayakutani hata iweje, kwanini sisi ambao madereva hawajastaarabika bado tunajenga barabara nyembamba?.
 
Mkambarani kwenye barabara ya kuelekea Dar es Salaam

Mkambarani umetoka zako Kingolwira unaitafuta Mikese, hili eneo moja tamu sana kunyoosha goti huku ukiwa unatazama mashamba ya katani...

Dereva asiyemzoefu hiki kipande kuna ama kuchochora au kukutana na mtu uso kwa uso kwa sababu barabara inavutia mno kukiwasha...

Kuna siku nikiwa natoka zangu Moro mchana kweupe kuna Hilux 2.4L GD-6 tulikuwa wote tunatia wese pale Puma Msamvu, yenyewe ikaondoka ikaniacha. Baadaye kabla ya kufika Mkambarani nikakutana na jam kubwa kishenzi, ikabidi nipite pembeni kwenye mashamba ya mikonge, mbele kidogo naikuta imekula mzinga Mkambarani hapo uso kwa uso na ndio imesababisha hiyo jam, na jamaa aliyekuwa anaendesha kazima pale pale (tulikuwa wote Puma pale)...
 
hata zaidi ya hapo kwanza halafu kingine ni kiburi, ujuaji na "unajua mimi ni nani" syndrome plus kuna serikali ambayo inataka kumfurahisha kila mtu badala ya kufanya mambo sahihi ili kuokoa maisha ya watu, uamuzi sahihi kwa siku zote huwa unpopular lkn kama unataka kufanya maamuizi kwa kusikiliza emotions za watu hawawezi kuongoza nchi na kutatua matatizo ya watu na ndicho kinachoendelea tanzagiza.

juzi kati waziri mzima mwenye dhamana ya usalama wa raia anakwenda kupoteza muda kuwa lectured n low iq driver ambaye anakataa point system kwamba arudishiwe points zake wakati points alipewa kwa kuvunja sheria za br. lkn anagoma na anatetewa na watanzagiza lkn likija kutokea la kutokea wanaanza kushangaa tumefikaje hapa, utasikia jamani ajali zitatumaliza, yeah zitamaliza watu ndiyo ...
Mkuu unataka kumlaumu waziri Tena,,?
Kwa pressure Ile angefanya Nini ?
Waziri aliita wasanii wastukane tuliongea nn ?
SISI watanzania Kuna mda ni wanafki sana,
Hata waziri alikubali kwa sababu pressure ilikuwa kubwa,wamiliki wa mabasi Wanafasi serikali na pia wana pesa ,mzigo unabaki kwetu sisi.
Hii ajari ni dereva ameovertake,,,

Yan RTO au jeshi la polisi lisimamie dereva asiovatake HEB tuwe serious ,mfano tuu wakati ana overtake hao abiria walichukua hatua Gani?
.humhum jamii forum kundi kubwa lilipiga makofi Madereva wasikatwe point .haya ndo majibu ya mtihani

Wapumzike kwa amani
 
  • Thanks
Reactions: Lax
MORO AGAIN.
Chanzo Cha ajali dereva wa Lori kutaka kuya ova take magari yaliyopo mbele yake.
Wakikataa point wanalalamika.
Sina huruma na madereva
Kwahiyo watembee kama konokono hadi wanafika maana njia nzima ni msululu na njia ni mbili pekeake
 
Aiseee,kwa hyo Bora kifo?
Sio kila anae-overtake anakutana na kifo wataka uniambie jana nzima alie overtake ni huyo wa lori pekeake

Suluhisho ni kujenga njia ya malori ili at least magari yaende sio kurundikana safari ya masaa matatu dar-moro waenda hadi masaa sita kwa kumfuata mtu nyumanyuma kwa speed ya kono kono
 
Wote mnaowalaumu madereva hasa kwa njia ya moro bado hamjasafiri na bus kwenda mikoani au kuja dar msululu ni mkubwa sana

Siku nimesafiri na new force Yani ili kidogo itembee walau ikabidi ipitie njia mbadala ya vumbi lakini njia kuu haipitiki ni mwendo wa malori mwanzo mwisho

Ni kweli madereva wanakuwaga na makosa ila hiyo route ni changamoto aisee
Hili suala la barabara nyembamba huwa wanajifanya hawalioni.
 
Sikuwepo mkuu,siwezi kujua. Ila huwa tunawaona madereva wanavyopokea rushwa tena kuna wakati wanalazimisha, wanaona ni haki yao,usipotoa unaandikiwa faini na huna pa kushtaki.
Na kuhusu weledi,kitendo cha magari mabovu kuwepo barabarani ni uthibitisho hao maaskari hawatimizi wajibu wake,ingekuwa maaskari wanatimiza wajibu wao magari mabovu yasingekuwepo barabarani. Hapo bado hatujaja kwenye pikipiki, watu hawavai helmet na polisi wanatazama tu..
ni kweli lakini uhalisia huo upo nusu,
kwa upande mwengine hata dereva naye ni mzigo maana anakubali kuendesha gari bovu,

kwasasa tunaweza zipongeza mamlaka kuweka ugumu kwenye kupata leseni, kwa kuhakikisha kila mtu anahudhuria chuo cha udereva , lakini hii haitoshi mitihani bado ipo chini ya kiwango sana,

Yani concept inayokuepo ni kwamba kila aliyelipa ada inabidi afaulu test na kupata leseni, mwanafunzi mwenyewe anatamani abebwe na apate leseni uzoefu ataipata mbele ya safari, walimu nao wanamtazamo huo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupunguza mzigo wa kufundisha vizuri gari pamoja na sheria za barabarani. Halikadhalika trafiki anaekufanyisha test anajua hapa kuna wazembe wamekuja hawajaiva tutapiga hela tu, na pia atleast hawa wamekuja kwa njia halali wataenda kukomaa na kua wazuri tu.


Nimeshindwa kupata bandiko fulani kwa haraka lakini ni bandiko la muda mrefu sana pata miaka 8 -10 pale facebook page ya RSA - mabalozi wa usalama barabarani hawa, changamoto walizozieleza kwenye bandiko lile lile hadi leo hazijaisha


Test ya kuandika kweli inaweza kua na maswali 5 au 10 ? yanatosha haya kumpima dereva kama ameelewa kanuni mbalimbali na alama za barabarani?, road test?

hapa chini hii ni South Korea emu angalia Test zao, written test, Skill test, Road test. dereva anatakiwa kutoboa zote tatu hizo ndo ahesabike kafaulu ili apate leseni, na tutambue hii ni basic driving hujafika kwenye Malori au Mabasi. Bongo hii tutafika lini magari yenyewe ya ufundishaji yanachangamoto na karibu kila mwaka yanakaguliwa.

je tupo tayari wote kuanza kubadilika na kuona ajali tunaweza zipunguza kwa ktatua vipengele vyake kimoja kimoja? 1. dereva , 2. chombo , 3. miundombinu

View: https://www.youtube.com/watch?v=toeQMsY9w9o&list=LL&index=4
 
Hili suala la barabara nyembamba huwa wanajifanya hawalioni.
Bila kutanua barabara hiyo njia itasababisha vifo vingi sana malori ni mengi sana hiyo njia utatamani ugairishe safari kama wasafiri na bus yan ni mwendo wa konokono hadi mnafika labda kama hivyo dereva ajitoe ufahamu apitie vichochoroni au a overtake kwa kujilipua maana njia nzima yamejazana si usiku si mchana
 
Back
Top Bottom