SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

Wakiambiwa wao ni wazembe wawekewe point, Wanaandamana ona sasa wanavo ua watanzania wa watu.
Polisi/Traffic wanatoweka barabarani usiku labda iwepo operation hivyo hata hofu ya kukatwa points kwa madereva ni mchana zaidi.

Halafu kuna uwezekano dereva mzembe akatenga bajeti (rushwa) ya safari nzima na asikatwe hata point.
 
Mkuu, barabara zingekuwa nzuri hizo ajali zingepungua sana. Mfano barabara zingekuwa zimetenganishwa kwa namna ambayo magari ya upande mmoja na upande mwingine hayakutani hata iweje, hata dereva aweje,ajali za magari kugongana uso kwa uso ambazo ndo nyingi zisingekuwepo. Hata hii ajali iliyotokea leo isingetokea. Nchi ambazo madereva ni wastaarabu bado wamejenga barabara ambazo magari ya upande mmoja na upande mwingine hayakutani hata iweje, kwanini sisi ambao madereva hawajastaarabika bado tunajenga barabara nyembamba?.
Wenye akili watakuelewa
 
Akili za ccm siku zote ni kukandamiza upande dhaifu hata kama hauna kosa
Swala la ajali sio la ccm wala chadema.
Hapo wamesema CHANZO CHA AJALI DEREVA WA LORI KUJARIBU KUYAPITA MAGARI YALIO MBELE YAKE.
kama wewe kweli dereva unatakiwa uovatake magari mangapi?na katika HALI GANI?.
Mimi nawaangalia tu mtakufa sana
 
Mkuu unataka kumlaumu waziri Tena,,?
Kwa pressure Ile angefanya Nini ?
Waziri aliita wasanii wastukane tuliongea nn ?
SISI watanzania Kuna mda ni wanafki sana,
Hata waziri alikubali kwa sababu pressure ilikuwa kubwa,wamiliki wa mabasi Wanafasi serikali na pia wana pesa ,mzigo unabaki kwetu sisi.
Hii ajari ni dereva ameovertake,,,

Yan RTO au jeshi la polisi lisimamie dereva asiovatake HEB tuwe serious ,mfano tuu wakati ana overtake hao abiria walichukua hatua Gani?
.humhum jamii forum kundi kubwa lilipiga makofi Madereva wasikatwe point .haya ndo majibu ya mtihani

Wapumzike kwa amani
Abiria wa wapi? Aliyeovertake ni dereva wa lori, aliingia upande usio wake!
 
CHANZO CHA AJALI DEREVA WA LORI KUJARIBU KUYAPITA MAGARI YALIO MBELE YAKE.
Mkuu CHANZO CHA AJARI NI BARABARA NYEMBAMBA kwanini hamtaki kusema ukweli anayapita magari ya upande gani na kwanini akiyapita akutane na gari lingine uso kwa uso? Kwanini wasitengeneze njia nne au nane kama mbezi-kibaha ambapo yakwenda hayakutani na yakurudi
 
Swala la ajali sio la ccm wala chadema.
Hapo wamesema CHANZO CHA AJALI DEREVA WA LORI KUJARIBU KUYAPITA MAGARI YALIO MBELE YAKE.
kama wewe kweli dereva unatakiwa uovatake magari mangapi?na katika HALI GANI?.
Mimi nawaangalia tu mtakufa sana
Umejibu kama vile unaishi mbinguni!
 
Kwa hyo kama barabara nyembamba umewakuta wenzako mbele wewe unatanua kulia uwapite ili ukae mbele Yao?hayaaa.
Ni kweli barabara inachangia ila si unawaona wenzio wapo mbele yako lakini.hivi utatumia spidi kiasi gani mpaka uwapite ukae mbele?
Hyo ajali mpaka moto umewaka na kuyaunguza alikuwa kwenye spidi gani mpaka wapate ajali na moto utokee tuwaze wote
 
Mkuu, barabara zingekuwa nzuri hizo ajali zingepungua sana. Mfano barabara zingekuwa zimetenganishwa kwa namna ambayo magari ya upande mmoja na upande mwingine hayakutani hata iweje, hata dereva aweje,ajali za magari kugongana uso kwa uso ambazo ndo nyingi zisingekuwepo. Hata hii ajali iliyotokea leo isingetokea. Nchi ambazo madereva ni wastaarabu bado wamejenga barabara ambazo magari ya upande mmoja na upande mwingine hayakutani hata iweje, kwanini sisi ambao madereva hawajastaarabika bado tunajenga barabara nyembamba?.
Ukiachana na ajali za uso kwa uso,kuna malori yanaharibika na kuachwa barabarani bila triangle tena kwenye kona hivyo hata njia hizo ajali zitakuwepo tu usiku kwa uzembe wa madereva.

Halafu ikitokea dharura gari linatakiwa lirudi lilikotoka unafanyaje hizo njia za uelekeo mmoja?
 
wakiwemo askari polisi watatu na raia mmoja, huku askari wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Mkoa wa Morogoro na Taifa tumekumbwa na simanzi kubwa kufuatia ajali mbili mbaya za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Oktoba 9, 2026, na kusababisha vifo vya jumla ya watu 32 na majeruhi zaidi ya 37.

Ajali ya kwanza na yenye maafa makubwa zaidi ilitokea majira ya saa 4:30 usiku huko Mkambarani kwenye barabara ya kuelekea Dar es Salaam, ikihusisha basi la abiria la kampuni ya Drim Line (T 672 DLT) lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya na lori la Scania (T 902 EGN) lililobeba mbao. Magari hayo yaligongana uso kwa uso na kuwaka moto mkubwa ulioteketeza miili ya marehemu, ambapo watu 28 walipoteza maisha (abiria 27 wa basi na mtu mmoja kwenye lori) huku watu 37 wakijeruhiwa vibaya kwa moto na fractures na kukimbizwa hospitalini baada ya uokoaji wa usiku kucha uliohusisha vikosi vya Zimamoto.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi unaonyesha ajali hii ilisababishwa na uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine bila tahadhari.

Ajali ya pili ilitokea mapema kidogo majira ya saa 12:45 jioni ya Alhamisi huko Miti Bora, Dumila (Wilaya ya Mvomero) kwenye barabara kuu ya kuelekea Dodoma, ambapo gari la Jeshi la Polisi lililokuwa na askari waliokuwa doria liligongana na lori lingine la Scania. Ajali hii ilisababisha vifo vya watu 4, wakiwemo askari polisi watatu na raia mmoja, huku askari wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Kwa sasa, majeruhi wote wanapatiwa matibabu ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Andrew Kantimbo, akitoa wito wa tahadhari kwa madereva huku uchunguzi zaidi wa kisheria ukiendelea.

1. mwenyezi Mungu wa Rehema awape pumziko jema wote waliofariki katika ajali ya bus na lori
2.mwenyezi Mungu ampe pumziko jema raia aliefariki kwenye ajali hapo Mti Bora wilaya wa Mvomero
3.Katika ajali hiyo hiyo ya Mtibora,Mvomero Ebaba mwingi wa rehema tunashukuru kwa hao watatu tunasema ahsante kwa kidogo
 
Umejibu kama vile unaishi mbinguni!
endeeleni kutetea ujinga na watawamaliza sana.
Ukweli usemwe hauwezi kuovatake magari zaidi Ya Moja .ovatake pale unapoona mbele ni salama ndivyo mwalimu wangu alivyonifundisha.sasa kama unaona kutoka iringa mpaka dar ni mbali unawahi una haraka.l kinachofatia Ndo hicho RIP
 
1. mwenyezi Mungu wa Rehema awape pumziko jema wote waliofariki katika ajali ya bus na lori
2.mwenyezi Mungu ampe pumziko jema raia aliefariki kwenye ajali hapo Mti Bora wilaya wa Mvomero
3.Katika ajali hiyo hiyo ya Mtibora,Mvomero Ebaba mwingi wa rehema tunashukuru kwa hao watatu tunasema ahsante kwa kidogo
Kuna namna machungu yamepungua baada ya kusikia hao watatu
 
..tunazoita barabara kuu ni nyembamba mno zilipaswa kuwa barabara za mitaani.

..barabara zote kuu zinapaswa kuwa za njia mbili kila upande, au zaidi.

..ajali za uso kwa uso zimekuwa zikitokea kwa miaka mingi na chanzo chake tunakijua lakini tumejizima data.
 
Ukiachana na ajali za uso kwa uso,kuna malori yanaharibika na kuachwa barabarani bila triangle tena kwenye kona hivyo hata njia hizo ajali zitakuwepo tu usiku kwa uzembe wa madereva.

Halafu ikitokea dharura gari linatakiwa lirudi lilikotoka unafanyaje hizo njia za uelekeo mmoja?
Ukiwa na jeshi la usalama barabarani lenye weledi, hayo mambo ya malori kuachwa hovyo barabarani hayatakuwepo na madereva watakuwa makini zaidi. Mfano mzuri ni Rwanda, maaskari wao hawatanii. Pia sasahivi kuna teknolojia,huwezi kuweka maaskari kila mahali, ila camera zinaweza kuwepo. Hii inasaidia kuona dereva anaefanya makosa kabla hajasababisha madhara. Sasa Na hilo la mwisho,barabara ziboreshwe na watu wameongea sana kuhusu barabara za ajabu tulizonazo
 
hizi ni siasa jamii imemezeshwa ,

kuna ajali mbili zimetokea, kuna basi la mkoa watu 28 wameondoka
Pole kwa raia wote,ila wauaji wakutwe na chakuwakuta.
 
Kwa hyo kama barabara nyembamba umewakuta wenzako mbele wewe unatanua kulia uwapite ili ukae mbele Yao?hayaaa.
Ni kweli barabara inachangia ila si unawaona wenzio wapo mbele yako lakini.hivi utatumia spidi kiasi gani mpaka uwapite ukae mbele?
Hyo ajali mpaka moto umewaka na kuyaunguza alikuwa kwenye spidi gani mpaka wapate ajali na moto utokee tuwaze wote
Ushawahi kusafiri kutoka dar-mbeya? Maana hapa naweza jadiliana na mtu ambae hata njia yenyewe haijui

Njia nzima imejaa malori na speed ya malori inafahamika labda liwe halina mzigo ila kama limemanda mzigo ni chini ya 40km/h. Sasa wewe kama dereva wa bus utaenda na hiyo speed utafika lini?

Ndio maana tunasema njia ndio tatizo

Hyo ajali mpaka moto umewaka na kuyaunguza alikuwa kwenye spidi gani mpaka wapate ajali na moto utokee tuwaze wote
Lakini pia katika hiyo ajali lililo kuwa na kasi ni bus maana lilikuwa kwenye njia yake, kwa inavyoonekana dereva wa lori ndio alikuwa aki over take na alikuwa katika mwendo mdogo ndio maana kawahi kubamizwa na bus

Kama unaelewa hapo ni kuwa kusingekuwa na msululu wa malori huyo dereva wa lori asingesababisha vifo vya hao wa kwenye bus, na mara nyingi njia hiyo ajali Huwa kati ya lori na bus hivyo basi ni vyema itanuliwe malori yapite barabara yao na magari mengine barabara yao ili kupunguza au kuondoa ajali za malori na mabus
 
Swala la ajali sio la ccm wala chadema.
Hapo wamesema CHANZO CHA AJALI DEREVA WA LORI KUJARIBU KUYAPITA MAGARI YALIO MBELE YAKE.
kama wewe kweli dereva unatakiwa uovatake magari mangapi?na katika HALI GANI?.
Mimi nawaangalia tu mtakufa sana

..wembamba wa barabara umechangia hapo.

..barabara ingekuwa njia mbili kwenda mbili kurudi ajali nyingi za ku-overtake zingepungua.
 
Ushawahi kusafiri kutoka dar-mbeya? Maana hapa naweza jadiliana na mtu ambae hata njia yenyewe haijui

Njia nzima imejaa malori na speed ya malori inafahamika labda liwe halina mzigo ila kama limemanda mzigo ni chini ya 40km/h. Sasa wewe kama dereva wa bus utaenda na hiyo speed utafika lini?

Ndio maana tunasema njia ndio tatizo

Lakini pia katika hiyo ajali lililo kuwa na kasi ni bus maana lilikuwa kwenye njia yake, kwa inavyoonekana dereva wa lori ndio alikuwa aki over take na alikuwa katika mwendo mdogo ndio maana kawahi kubamizwa na bus

Kama unaelewa hapo ni kuwa kusingekuwa na msululu wa malori huyo dereva wa lori asingesababisha vifo vya hao wa kwenye bus, na mara nyingi njia hiyo ajali Huwa kati ya lori na bus hivyo basi ni vyema itanuliwe malori yapite barabara yao na magari mengine barabara yao ili kupunguza au kuondoa ajali za malori na mabus
Kwa hyo huyo dereva kapata ajali akiwa na speed ya 40?
Mimi Sina tatizo na NJIA ni kweli NJIA ya morogoro NJIA Moja ni tatizo.lakini hyo sio sababu ya kufanya makosa.
Unagharimu maisha ya watu.
Yaani ukiangalia umbali wa safari ndo unasababisha dereva kutokuwa Malini tutazidi kuwapoteza.
Kuovatake ina ruhusiwa ila unaovatake wapi na vipi.
 
Back
Top Bottom