Simba Bob Junior wa Serengeti apinduliwa na kuuawa

Simba Bob Junior wa Serengeti apinduliwa na kuuawa

SAD NEWS…

Taarifa ya kifo cha Simba maarufu huko Serengeti ajulikanae kama Bob imezistua Nyoyo za Watu wengi Duniani ambao walifanikiwa kumuona Simba huyo ambae alikuwa kipenzi cha Watu kwa kuwa hakuwa na tabia za kujificha wala kukwepa Camera.

Bob alikutwa na umauti baada ya kundi la Simba Watatu kumvamia na kutimiza Lengo lao la muda mrefu la kuuangusha utawala wa Bob na kusimika ufalme wao porini hapo.

Simba hao Watatu ambao Bob aliwalea tangu wakiwa wachanga inasemekana walishafanya mapinduzi mara kadhaa ya kutaka kuuangusha utawala wa Bob lakini mara zote walikutana na upinzani mkali na hata kukimbizwa maeneo hayo.

Bob ambae alikuwa mtemi na mtawala wa eneo la Namiri aliongoza Simba wa eneo hilo kwa kipindi kirefu sana na alikwepa mapinduzi ya aina mbalimbali kwa vipindi tofauti huko Mashariki ya Serengeti.

Utawala wa Bob ulikuja baada ya kumpindua na kumuua Baba yake ambae alikuwa maarufu pia kwa Watalii Duniani ambae alifahamika kama C-Boy.

Umauti ulimkuta C-Boy mwendo wa Jioni pembezoni mwa Mto Ngare Nanyuki ambapo wakiwa wawili tu Bob alifanikiwa kufanya mapinduzi hayo tukufu na kuumaliza utawala wa Baba yake.

Pumzika kwa amani Bob.
Vita ulivipigana na mwendo umeumaliza.

View attachment 2549829
View attachment 2549828
View attachment 2549827
Stori nzuri na taarifa ya kusisimua!
 
Mbwa, paka hawajui wrong and right? Fuga halafu uwachunguze tabia zao utagundua.

Halafu kwa hadithi za biblia ufahamu wa mema na mabaya ulikuja baada ya kula tunda, sasa kwa ulichosema inamaana Kabla ya kula tunda binadamu alikuwa kama mnyama sababu hakujua wrong and right? Kuna kitu hakiko sawa.
Kabla ya kula tunda kulikua hamna kufa na mbingu zilikua extended hadi huku duniani, katika uumbaji wanyama waliumbwa kwa neno la Mungu while binadamu alumbwa kwa neno na kuwekewa Roho ya Mungu ndani yake
 
Kweli aise, ndiyo maana kuna video, nguruwe anashambuliwa na mamba, bwawani, unaona anafanikiwa kutoka bwawani, anakimbia mita nane tu, anaingia tena bwawani.
 
Hao Simba waliofanya mapinduzi haramu, wajue kuwa wana kesi ya Uhaini inawakabiri.
Hao Simba waliompindua na kumuua Bob-Simba inabidi wawekewe vikwazo na jumuia za kimataifa kwani utawala wao ni haramu na hautambuliki. Full stop!
 
Kabla ya kula tunda kulikua hamna kufa na mbingu zilikua extended hadi huku duniani, katika uumbaji wanyama waliumbwa kwa neno la Mungu while binadamu alumbwa kwa neno na kuwekewa Roho ya Mungu ndani yake
Tafsiri ya kutokujua mema na mabaya ni nn? Mtu asiyejua mema na mabaya anafananaje?
 
Kweli aise, ndiyo maana kuna video, nguruwe anashambuliwa na mamba, bwawani, unaona anafanikiwa kutoka bwawani, anakimbia mita nane tu, anaingia tena bwawani.
Hahaha. Unajaribu kusema nn?
 
Hao ni simba brothers, hao siku zote huishi pamoja, lakini lijapo swala la baba na vijana wake wa kiume kamwe huwa hawaishi pamoja.
Watoto wa Simba wakikua, lile dume (baba yao) huwafukuza wakajitegemee, lakini majike huwa hawafukuzwi.
Wale watoto wakishapata nguvu huko ndipo hupanga kuja kufanya mapinduzi ya kumuua baba yao.
Kuna Coalition za Simba dume mpaka sita fuatilia documentary mbali mbali mkuu,,wanaishi pamoja, wanawinda pamoja na wanateka ngome pamoja
 
Kuna Coalition za Simba dume mpaka sita fuatilia documentary mbali mbali mkuu,,wanaishi pamoja, wanawinda pamoja na wanateka ngome pamoja
Mdugu huwa wanaishi pamoja
Issue wakifika umri fulani lazima baba yao awafukuze otherwise atawaua.
Ukiina wamekuwa wengi sehemu moja basi ujue kilichotokea ni wale waliofukuzwa kutoka familia tofauti hujikuta wanatangatanga wenyewe with no experience au ngu thabiti za kuwinda. Hawa wakikutana huwa hawafukuzani bali huungana na kuishi pamoja ingawa ni very rare case
 
Uko sahihi kabisa kwa hilo..Lakini pia kuna wengine mfano kama Mapogo brothers waliotawala sehemu kubwa ya Kruger national park Afrika kusini na coalition zingine kibao unakuta ni madume kadhaa yanayokua pamoja na kushirikiana kwa Kila kitu...
 
Back
Top Bottom