kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ni jambo zuri sana sisi wapenzi wa Simba kwenda wengi kwenye tamasha letu la Simba day. Ukweli kuujaza uwanja kuliko Yanga walivyofanya ni njia nyingine sahihi ya kutibu sonona iliyotokana na timu yetu kufanya vibaya ndani ya uwanja dhidi ya Yanga kwa misimu 2 mfululizo.
Kujaza huku kwa uwanja mapema kunachagizwa na Yanga kushindwa kuujaza uwanja kutokana na kulewa furaha za mafanikio msimu uliopita, viingilio vikubwa na tamasha kupangwa katikati ya mwezi watu hawana hela, na matumaini mapya ya usajili mzuri uliofanywa na uongozi wa simba. Wachezaji wa simba walishindwa kutupa furaha ndani ya uwanja na Sasa tunakwenda kuwakopesha imani zetu tena kwa msimu ujao.
Angalizo hapa ni moja tu kwa uongozi, bench la ufundi na wachezaji wa simba kuwa wasifurahie sana mashabiki kuujaza uwanja, taabu kwao itakuwa kubwa sana kama timu isipofanya vizuri tena kiwanjani.
Vinginevyo hongera sana Simba kwa kujitokeza kwa wingi kukata tiketi mapema.