Simba na Yanga ni ngao ya kupumbaza wananchi wasifuatilie mambo muhimu ya nchi

Halafu unatoka kazini wanakuja kukupiga mzinga ila kuanzia asubuhi ni Simba na Yanga.
Kwahiyo wanapata wapi hata pesa za kununua jezi za simba na yanga ikiwa hao mashabiki hawana kazi wanapiga vizinga?
 
Mkuu kweli kqbisa,nipo manispaa fulani hapa,yani nimeenda mjn leo kila kijiwe mayele mayele, mara sacko. Sacko mqra kocha wa simba mara mzungu daa.
Ila mkuu hiyo ni burudani kama burudani zengine na sijawahi kusikia mtu kaacha kufanya kazi au kutunza familia yake kisa anashabikia au kujadili simba na yanga.
 
Mkuu mimi nawashangaa sana wao wanataka muda wote na watu wote wajadili siasa tu.
 
England zipo, spain zipo, France , italy, germany, dunia nzima zipo,
Basi sie peke yetu ndio tusiwe nazo?
Kisa tu baadhi ya watu wana uchungu na maisha?
Acheni hizo hapa tunapita tu unataka kun'ganga'nia na maisha tuuuu bila starehe kidogo?bila simba na yanga hakuna tanzania
 
Ongezea sahvi na mambo ya kina mondi konde nandy na wengineo
Kila siku mnazinduliwa matamasha
Wabongo wengi sahv akili zao ni kuwafatiliaaa wao tu

Ova
Mkuu huo ni upande wa burudani sasa mlitaka iwaje labda?
 
Nchi ulizozitaja watu wa Nchi hizo wanashabikia timu zinazotoka maeneo yao sio eti nchi nzima watu wanashabikia timu mbili tu !! Huko ulaya hakuna kitu kama hicho !!
 
Mpira umebaki kua kitu kinacho wapa furaha watanzania wengi, ukijikuta unajua Sana kukosa kosoa unapotea wanao wanabaki omba omba,
 
Kwahiyo mtu anayejadili mpira huwa hajadili masuala mengine zaidi ya mpira tu?
 
Jamaa hawataki burudani kabisa wao wanataka watu wote na muda wote wajadili siasa tu.
 
“Yote tuliyofanya ni kuwapa mkate na burudani nao wakatupatia uhuru wao”. Hadrian.

Burudani nyingi tu ni mikakati ya watawala kuwapumbaza wananchi wasifuatilie mambo ya msingi, hasa siasa za nchi zao.

Huu mtego unafanya kazi vizuri zaidi kwa watu masikini na wajinga.
 
Kwenye hizo nchi watu wanaangilia michezo, wanaenda kwenye matamasha ya muziki, sanaa utamaduni ila wakimaliza wanaendelea na mambo mengine yanayowahusu.

Huko huwezi kukuta wanapigiana makelele na kufanya jokes za mpira muda wote kama hapa.

Lakini pia wao hata wangejikita kwenye mipira, tayari wemeshafanya maendeleo makubwa sana kwenye nchi zao sehemu zote.
 
Huu ndio ujinga mwingine. Mfumo wenyewe wa mpira wa Tanzania una tija kidogo sana kwenye maendeleo kwa sababu Simba na Yanga zimehodhi sekta nzima lkn hata zenyewe mpaka sasa hazijaweza kujenga hata viwanja vidogo tu vya mazoezi, zahanati au mgahawa useme wanatoa ajira au huduma. Ni kelele na blah blah tupu.
Nchi ulizozitaja watu wa Nchi hizo wanashabikia timu zinazotoka maeneo yao sio eti nchi nzima watu wanashabikia timu mbili tu !! Huko ulaya hakuna kitu kama hicho !!
 
Hakika
 
Umeonge jambo moja kuwa sana lakini kwa akili za watu wengi hapa Tanzania hawatakuelewa. Maana wao wanafikiri mpira ni mchezo kama mchezo na burudani.

Lakini mchezo huu unaweza kubeba ajenda ovu nyuma yake na kwa sababu watu wamepofushwa hawawezi kuona.

Hongera sana nafarijika kuona bado kuna watu wanaweza kufikiria ndani ya Tanzania wewe ni mmoja wa wateule wachache.
 
Kenya kulikuwa na timu mbili FC Leopard na Gor mahia,zilitumika na serikali kuwapumbaza wananchi baada ya KANU kutolewa madarakani hazina tena mvuto
 
Mkuu jitahidi kuandika kwa usahihi, huku ukizingatia matumizi ya koma, nukta,kuacha nafasi na herufi kubwa. Maana ni aibu kwa uandishi huu, au ww ndio hao mnaojadili mipira siku nzima
 
Asantee mkuu hapa sijaona kasoro ndio mana umeelewa nilichomanisha Ila Kama ningeandika maombi ya kazi ningekesha kuirudia barua yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…