Simba SC, kwa mpira huu kazi ipo

Utulivu wa mchezaji ndio ubora wenyewe. Mchezaji unapata nafasi unabutua tu. Nafasi za kibu kwa mchezaji mtulivu kuna goli na assist.
 
Ndio mjue hatukuwa na mwalimu, pre season ya kutosha alafu bado tunacheza kutegemea vipaji! Hata kupanga timu ni tatizo! Simba watafute mwalimu wa viwango ambaye anaweza kusoma wachezaji haraka na kujua namna ya kuwatumia.

Simba ina timu bora kuliko zote lakini makocha hawajui wafanye nini na zile talent.
 
Tuwe na kiasi mpira ni burudani sio vita,mpira una kupanda na kushuka tumekuwa bora miaka minne mfululizo tukichukuwa ubingwa na kila kombe la ndani,elewa hatuwezi kuwa bora miaka yote tuvumilie muda mwingine ukiona panapovuja ndio unapoziba.
Sawa,lakini bila ugomvi binafsi wa Mo ,Chama asingeondoka!
 
Si comment mtasema Mimi shabiki wa Yanga kwa kuwa Nina Furaha moyoni hata nikimiss kujaza katumbo kwa vichps sijali
πŸ’šπŸ’šπŸ’šπŸ’šπŸ’š Zam kwa ZamπŸ’›πŸ’›πŸ’›πŸ’›πŸ’›πŸ’›
 
Mechi 4.. Pointi 8..
Droo 2, Ushindi 2..
Cleansheet 4.. Magoli ya kufunga 2....

Si twakimu mbaya ila ukilinganisha na Uto tunaonekana hatujui....

Ndio mtabeba mkuu ukumbuke mmepiga mechi 4 tu bado mechi 30 kwahiyo bado mapema
 
Tulieni nyie simba ni bonge la team raha inakuja wacha kocha aje kuanza kazi kuone moto wake
 
Ndio mtabeba mkuu ukumbuke mmepiga mechi 4 tu bado mechi 30 kwahiyo bado mapema
Labda huko mbele gari lichanganye na Uto waanze kuharibu.... Japo sioni kwa Uto kuanza kupoteana kwa msimu huu....
 
Tuwe na kiasi mpira ni burudani sio vita,mpira una kupanda na kushuka tumekuwa bora miaka minne mfululizo tukichukuwa ubingwa na kila kombe la ndani,elewa hatuwezi kuwa bora miaka yote tuvumilie muda mwingine ukiona panapovuja ndio unapoziba.
Sio kwa mashabiki wa nchi hii, muda mfupi ujao utaanza kusikia kuna mgomo, wachezaji hawajalipwa, kuna watu wanatufanyia fitna n.k.

Hizi ni changamoto za kawaida ambazo ndio zitakazokufanya kesho uwe bora zaidi ya leo.
 
unajua team imebadilika ghafla inategemea long passes na crosses..maskini ya Mungu wachezaji pia wako under pressure sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…